Daktari Bingwa Anena: Sitoona mgonjwa wa Bima ya Afya

tutafikatu

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
3,323
4,620
Daktari bingwa mmoja wa hospitali ya Temeke, jijini Dar es Salaam, mchana wa leo alisikika akiapa kutoona mgonjwa wa NHIF, ati kwa sababu analipwa sh. 5,000/= tu kama consultation fee ya kumuona kila mgonjwa wa bima ya Afya ya Taifa (bila kuhusisha vipimo na dawa).

Wakati huohuo madaktari bingwa wa level yake aliosoma nao chuo, na sasa wanafanya kazi hospitali ya Taifa Muhimbili, wanalipwa consultation fee ya 40,000/= kwa kila mgonjwa.

"Nadhani mimi natumia ubongo wa panzi, NHIF wanasema mimi siwezi kutumia ubongo wangu sawasawa na colleague aliyepo Muhimbili, bora nisione mgonjwa nisije leta madhara bure kwa kinyongo nilichonacho"

Chanzo: Mimi mwenyewe.
 
Aache..uliona wapi mgonjwa kiongozi amelazwa Temeke....Temeke anapokea wagonjwa kutoka Muhoro Bungu Kisiju Bweni na wapi sijui.. Muhimbili tunapokea kutoka Magogoni Oysterbay Mikocheni Mbezi Upanga and more others..
 
Haya ndo mambo nilikuwa namwambia member mmoja, kuwa kazini na kufanya kazi kadiri inavyostahili ni vitu viwili tofauti, binafsi kilichonitoa govt ndio hiki watu elimu iko sawa tena pengine mwengine iko juu, lkin maslahi tofauti kabisa, kazi zile zile kodi ile ile, haya ndo yalikuwa mambo ya kuanza nayo. Unajua ni kwa vile watu hawajui unadhani walimu ckuiz ni kama enzi zetu zile walimu wanakuja usiku shuleni kufundisha? hakuna morali as a result ni kilio ktk elimu, kilio ktk afya kilio kila sehemu. Watu hawana utashi kabisa wapo kwa vile tu hawana alternative.
 
NHIF ni shamba la bibi ambalo watawala wanajifanya hawalioni kabisa ili tusishtuke kua wenzetu hawapandi ila wa kwanza kuja kuvuna hata vikiwa havijakomaa,hongera Dr maana taaluma umeisotea kwenye madawati haujaiokota khaaa 5000 daharau hii sishangai ma-nurse wakitudunga sindano za utosini kwa kinyongo.
 
Aache..uliona wapi mgonjwa kiongozi amelazwa Temeke....Temeke anapokea wagonjwa kutoka Muhoro Bungu Kisiju Bweni na wapi sijui.. Muhimbili tunapokea kutoka Magogoni Oysterbay Mikocheni Mbezi Upanga and more others..
Kwani hao wanaoishi Bungu, Bweni, Muhoro nk hawahitaji huduma bora za afya? Sio watu? nyie wa Osterbay na Mikocheni ndo watu au? Acha dharau mkuu.
 
Mkuu mbona kama hiyo amount ni kubwa??? Kwani mgonjwa wa NHIF Muhimbili kwa maspecialist anatozwa 30,000/= ina maana serikali huwa inaongezea??? Vile vile katika hiyo consultation fee unataka kusema hakuna hata pesa inayoingia serikalini ??? Kwamba pesa yote hiyo huwa anachukua daktari husika???


Nina mashaka na wewe otherwise utoe ufafanuzi wa kina....
 
Nakupongeza Dr jiulize wewe umekaa nae attend kwa dakika 5 nurse anampa huduma mchana ucku asubuhi maslah yake ndo kabisaaaaa yamkini 500. Messenger wa office ya NHIF kanawiri LAZMA HUDUMA ZIDORORE
 
Bima ya Afya, kuna usumbufu kwenye Hospitali za AICC na SELIAN zilizopo Arusha kwamba unapomwona Daktari Bingwa kwa ajili ya Matibabu unapaswa kulipia fedha Taslim badala ya Kadi ya Bima kutumika kwa ajili ya malipo hayo Hii imekaaje?
 
Back
Top Bottom