Daktari asahau simu tumboni baada ya upasuaji

Mapengo 17

R I P
Joined
Mar 28, 2014
Posts
1,228
Reaction score
618
Hali ya kustaajabisha yazuka katika hospitali moja uzazi baada ya daktari kusahau simu ndani ya tumbo la mwanamke aliyejifungua kwa njia ya upasuaji nchini Jordan

Daktari mmoja anadaiwa kusahau simu ndani ya tumbo la mwanamke aliyejifungua kwa njia ya upasuaji kwenye hospitali moja ya uzazi iliyoko katika mji mkuu wa Amman nchini Jordan.

Maelezo zaidi yanaarifu kwamba simu hiyo iligundulika kuwa tumboni mwa mwanamke huyo baada ya kuanza kunguruma ndani. Tukio hilo liliwacha wengi vinywa wazi na kufikishwa katika bunge la Jordan, na kuitaka serikali ijiuzulu.

Kwa mujibu wa taarifa za Gulf News, mwanamke anayetambulika kwa jina la Hanan Mahmoud Abdul Karim mwenye umri wa miaka 36, alijifungua kwa njia ya upasuaji katika hospitali ya Amman.

Baada ya kujifungua mtoto wa kiume mwenye uzito wa kilo 4.8 na kurudi zake nyumbani, mwanamke huyo alianza kusikia mingurumo tumboni na kuhisi maumivu.

Papo hapo mwanamke huyo alifikishwa katika hospitali ya serikali ya Amman, na kugundulika kuwa na kitu chenye urefu wa sentimita 7 tumboni mwake baada ya kufanyiwa utafiti.

Baadaye akafanyiwa upasuaji na kutolewa simu kutoka kwenye tumbo lake. Tukio hilo lilizua utata na kufikishwa bungeni na Salim Al Bataynah, na kuitaka serikali ilijiuzulu kutokana na kosa hilo kubwa lililofanyika.

Wizara ya Afya ya Jordan ilifahamisha kutokuwa na taarifa zozote kuhusiana na tukio hilo, na kutangaza kwamba itafanya uchunguzi zaidi.

Chanzo: TRT
 
Kumbe wabunge wenye tabia kama za CHADEMA wako wengi! Yaani daktari asahau simu tumboni kwa uzembe wake.Badala ya mbunge kuomba huyo daktari achukuliwe hatua anaomba serikali ijiuzulu!!! Yale yale ya CHADEMA!!!!!
 
Hahaahahaha hapo serikali sijui inahusika na nini duu
 
Kumbe wabunge wenye tabia kama za CHADEMA wako wengi! Yaani daktari asahau simu tumboni kwa uzembe wake.Badala ya mbunge kuomba huyo daktari achukuliwe hatua anaomba serikali ijiuzulu!!! Yale yale ya CHADEMA!!!!!

wakishamaliza kunywa viroba watakuja kukujibu!!!!!!
 
Siwezi kukubali litumike neno "kusahau" kwa kitu kama simu ya nchi saba tumbon, naweza kuhisi ni njama ya daktari kwa huyo mama!
 
Ilikuwaje akashika simu wakati wa kazi hasa upasuaji?!, na ilikuwaje mpaka akaiweka tumboni kwa mgonjwa hadi kuanza kushona eti kusahau?!, nakataa kuna jambo hapo sio bure
 
Hali ya kustaajabisha yazuka katika hospitali moja uzazi baada ya daktari kusahau simu ndani ya tumbo la mwanamke aliyejifungua kwa njia ya upasuaji nchini Jordan

Daktari mmoja anadaiwa kusahau simu ndani ya tumbo la mwanamke aliyejifungua kwa njia ya upasuaji kwenye hospitali moja ya uzazi iliyoko katika mji mkuu wa Amman nchini Jordan.

Maelezo zaidi yanaarifu kwamba simu hiyo iligundulika kuwa tumboni mwa mwanamke huyo baada ya kuanza kunguruma ndani. Tukio hilo liliwacha wengi vinywa wazi na kufikishwa katika bunge la Jordan, na kuitaka serikali ijiuzulu.

Kwa mujibu wa taarifa za Gulf News, mwanamke anayetambulika kwa jina la Hanan Mahmoud Abdul Karim mwenye umri wa miaka 36, alijifungua kwa njia ya upasuaji katika hospitali ya Amman.

Baada ya kujifungua mtoto wa kiume mwenye uzito wa kilo 4.8 na kurudi zake nyumbani, mwanamke huyo alianza kusikia mingurumo tumboni na kuhisi maumivu.

Papo hapo mwanamke huyo alifikishwa katika hospitali ya serikali ya Amman, na kugundulika kuwa na kitu chenye urefu wa sentimita 7 tumboni mwake baada ya kufanyiwa utafiti.

Baadaye akafanyiwa upasuaji na kutolewa simu kutoka kwenye tumbo lake. Tukio hilo lilizua utata na kufikishwa bungeni na Salim Al Bataynah, na kuitaka serikali ilijiuzulu kutokana na kosa hilo kubwa lililofanyika.

Wizara ya Afya ya Jordan ilifahamisha kutokuwa na taarifa zozote kuhusiana na tukio hilo, na kutangaza kwamba itafanya uchunguzi zaidi.

Chanzo: TRT

None sense
 
Back
Top Bottom