Dakika ya 21, mpira unachezwa kwenye goli la timu ya Magufuli(Guli City)

Ki Mun

JF-Expert Member
Oct 6, 2014
3,443
4,386
Naulinganisha uongozi wa Magufuli sawa na mchezo wa soka, sawa na timu ndogo ambayo iliingia Old Trafford kwa kasi ya ajabu lakini kadri muda unavyosonga mbele akina Mkhitaryan, Ibrahimovic na Juan Mata taratibu wameweza kubadili mchezo na hali ya timu ya Guli City ni mbaya mno...:p:p:p

Ukifanya hesabu kwa kuchukua miezi 14 ya uongozi wa sasa wa Magufuli ukaigawa kwa jumla ya miezi 60 ya utawala wake(kama ataepuka majeruhi na akafanikiwa kucheza dakika zote za mchezo) na kisha ukazidisha kwa dk. 90 za mchezo wa soka utaona kuwa sasa ni kama tuko dk. ya 20 ya mchezo, Guli City wako hoi, pamoja na kujaribu kumtumia mchezaji wao kinda Daudi Bashite lakini haonekani kuwa na maarifa ya mchezo na dk yoyote tu atatolewa kwa kadi nyekundu. Mchezaji mwingine mkongwe Harrison Mwakyembe naye ulimi uko nje bila shaka umri unamtupa mkono...hana maarifa wala akili ya kawaida ya mchezo.

Kwa kifupi, kwa sasa ni piga nikupige ndani ya penalty box ya Guli City....ni swala la muda tu kabla hawajapigwa bao au beki na kepteni wao John Kapombe a.k.a Mbuyi Twite hajautumbukiza mpira kwenye goli lake mwenyewe...hii ni timu inayokosa organisation na wanafanya makosa ya wazi, wamepaki basi na beki anagombana hata na mashabiki wanaozomea jukwaani, aibu sana!
 
Alafu mnachekelea? Yani mmeacha mambo ya msingi
mnamjadili Makonda? Mnajua kinachoendelea nyuma ya pazia?

Mwafrika kuelimika ni kazi!
 
Inaelekea mikakati ya dirty money/business architects and beneficiaries alike imefika mwisho.
 
Tatizo timu yenyewe Guli City ina wachezaji wa viwango vya chini sana wasiojua wala kufuata Sheria halali za FIFA wanachojua wao ni kucheza rafu ns mabao ya mkono tuu.
Kama kocha mwenyewe kazi yake ni kuwatia dhakari wachezaji wake,watapata wapi nguvu na maarifa ya kucheza soka?
 
Back
Top Bottom