Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,768
- 41,009
Salama wandugu, hii ni sehemu ya tatu ya mada zile tano; hii ya leo ni kujibu mojawapo ya hoja zinazohusiana na kashfa... nitaendeleza wazo baadaye, ikimpendeza Mungu.
[/CENTER]
Na. M. M. Mwanakijiji
Uibuaji na Uumbaji wa Kashfa Una Kikomo
Tunashuhudia pia jambo jingine la kushangaza na kusikitisha. Wale waliozoea kuishi kwa kashfa bila kashfa hawawezi kuishi wakazoea! Tangu Rais Magufuli aingie madarakani tumeshuhudia jitihada kubwa ikifanyika kuibua kashfa mbalimbali. Lengo kubwa ambalo liko wazi la kujaribiwa hili ni kuonesha kile ambacho wakosoaji wa Magufuli wanakiita kuwa ni “CCM ni ile ile”. Huu mtaji wa “CCM ni ile ile” una nguvu yake na ukweli wake.
Lakini kuna lengo jingine nyuma ya hili; nalo ni kumtikisa na hata kuifanya serikali ya Magufuli ianguke. Ni vizuri turudi nyuma kidogo.
Ndani ya miezi hii sita tu tayari zimejaribiwa kashfa kadhaa; na bado hazijamganda Magufuli: Hizi ni baadhi tu ya kashfa hizo zilizojaribiwa kuibuliwa au kuumbwa:
• Kashfa ya Uchaguzi wa Zanzibar
• Kashfa ya Januari Makamba
• Kashfa ya Kuwawajibisha Watendaji Wabovu a.k.a Utumbuaji Majipu
• Kashfa ya Kashfa ya Ununuzi wa Nyumba za Serikali
• Kashfa ya Kuteua Watendaji
Wanasiasa – ndani ya chama tawala au nje yake – huweza kutumia kashfa kama nyenzo ya kusababisha serikali ifanye mabadiliko makubwa n ahata ianguke. Kwenye nchi ambazo demokrasia imekomaa kashfa hufanya serikali zisidumu madarakani kwa muda mrefu. Ni muhimu kuzingatia ukweli huu tunaposikia kashfa mbalimbali. Upande mwingine kashfa kwa kiongozi yeyote zinapaswa kuifundisha serikali kuwa iko kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na si vinginevyo.
Jambo jingine la kuzingatia ni ukweli kuwa kashfa huwa hazikomi. Karibu serikali zote duniani zikikaa muda mrefu madarakani huanza kukutwa na kashfa; na sababu yake iko wazi tu – madaraka makubwa huharibu vikubwa. Ni kwa sababu hiyo wale waliozoea “CCM ile ile” wanajua na kutarajia tu kuwa lazima kutakuwepo kashfa nyingine kwani tayari tumekuwa na kashfa nyingi tangu IPTL katikati ya miaka ya tisini hadi leo kashfa zimekuwa kama sehemu ya maisha ya kisiasa ya nchi yetu.
Hata hivyo, ujio wa Magufuli unauliza swali ambalo wengi wanataka kuona jibu lake; je, atafanya nini na kashfa kubwa, je kashfa kubwa ndani ya serikali yake atazishughulikia vipi. Sasa, kwa sisi ambao tunaamini nia na uwezo wa dhati wa Magufuli kuleta nidhamu ni rahisi kusema jambo ambalo wengine wanaweza wasilione au kuamini – Magufuli hatovumulia kashfa.
Hata hivyo, hadi hivi sasa hatari inayoonekana ni baadhi ya wapinzani na vyombo vya habari kujaribu kuumba kashfa kiasi kwamba huko mbeleni kashfa ya kweli inaweza ikatokea na watu wakaona tu ni kama habari ya “mtoto aliyelia mbwea anakuja!”.
Jambo jingine linaloendana na hili ni ukweli kuwa wanaojaribu kuumba au kuibua kashfa hizi (ziwe za kweli au za kulazimisha) wanataka kuondoa kuaminika (credibility) ya Magufuli na watendaji wake. Kwa sababu kama Magufuli hatoaminika kama ambavyo ambaye aliyemtangulia alivyopoteza kuaminika katika vita dhidi ya ufisadi kutawapa wapinzani mtaji mwingine wa kisiasa kuelekea 2020 kuwa “CCM ni ile ile” na “tuliwambia hawawezi hawa”.
Hii ni bahati nasibu mbaya; ni bahati nasibu ambayo ni vigumu mno kuona mtu atashinda vipi. Tatizo la kutaka kuonesha kutoaminika kwa Magufuli ni kuwa wale wanaosimama leo kuonekana wanapiga vita ufisadi na wana uchungu sana ndio wao wenyewe waliopoteza kuaminika kwanza baada ya kuamua kula matapishi yao na kulala kitanda kimoja na ufisadi! Jinsi walivyoshikana mikono na chembe za ufisadi (elements of corruption) ndugu zetu hawa siyo tu wamepoteza kuaminika ni kuwa ni vigumu sana kuweza kuaminika tena! Utawaamini vipi tena?
Hata kama wanayosema yana chembe za ukweli ni vipi watu wataamini kuwa wanamaanisha kweli na kwamba ikifika uchaguzi wa 2020 wale wale ambao wanawataja leo kuwa ni viongozi wabovu na mafisadi wakawa ndio wabeba bendera wao na wao wakizungusha mikono nyuma yao kama wanamazingaombwe?!
Lakini tatizo kubwa ni kuwa – na hili nitalieleza vizuri makala inayofuatia – upinzani unategemea uchafu na madudu ya CCM ili usimame; ni jambo moja kuonesha kuwa CCM ni chama kilichopotoka kikiwa madarakani kama wengi tulivyofanya na ambao bado tunaamini – kwani bado hatujaona mabadiliko yake – lakini ni jambo jingine kabisa kupanga mipango na bajeti kutegemea uchafu na upotofu huo! Kwa sababu, upotofu na uchafu utakapoanza kusafishwa au kuondolewa hoja ya “CCM ni ile ile” itakufa!
Na hatari yake chini ya mtu kama Magufuli tunaweza kwenda kuwa na chama cha siasa chenye nguvu kubwa sana kama cha Kikomunisti cha China! Vyama vingine vya siasa vitaweza kujikuta vinakuwa ni vya pembezoni (peripheral parties) na sauti yake ya kwenda mapango!
Na ni rahisi kutabiri sana kuwa tunaweza kushuhudia watu wengine wengi wakirudi CCM hiyo mpya siyo kwa sababu wanakiamini chama kilivyo sasa bali wakajikuta wanamfuata Magufuli kwa miaka yake kumi madarakani kwani yawezekana kuwa ndio muda pekee uliobakia wa kubadili mwelekeo wa taifa letu.
Wazo hili linapaswa kumtisha kila mtu.

- Kashfa ya Sukari
- Kashfa ya Kuingilia Mahakama