Dakika 45, ITV na Waziri Lukuvi

Dakika 45, ITV na Waziri Lukuvi

Waziri Lukuvi kasema kweli CDM kazi yao kutunga uongo na porojo kamwambia Dk Slaa apeleke ushahidi wa makaratasi kama yeye anamiliki kitalu

Harafu akipeleka atafanya nini? Atajiuzuru au? Anasema aliomba kwaajili ya shule lkn kibali kimojawapo kinaonyesha aliomba kabla shule haijaungua, mimi namshauri aende mahakamani sababu amesingiziwa ili adai fidia ya kudhalilishwa harafu atajua Dr. Slaa ni nani!
 
Bw. Semunyo wa ITV boresha kipindi chako hiki kwa kuita na upande wa pili wa mawaziri kivuli mfano Mbowe, Lissu, Regia na hata Dr. mwenyewe wa ukweli tusikie wana nini cha kuwaambia Wa tz kwa hizo dakika 45...wa Magamba kila siku wanaboa.

Aulize pia maswali critical ili apate maelezo na ufafanuzi zaidi badala ya kusikiliza tu na kukubali kama mtoto asiye na ufahamu wa kutosha.
 
....hana lolote huyu kihiyo, mwalimu wa chipukizi Ismani na amejaa usangoma tuuu....!!
 
Mrs Lema, Lukuvi kaomba kama kuna mtu ana ushahidi alete zaidi ya hapo ni porojo

alete ushahidi kwani lukuvi kampeleka mahakamani kwa kudhalilishwa???tunataka lukuvi akanyage mahakamani ndo dk apeleke ushahidi..hivi na wewe mbona hujampeleka dk mahakamani si ulimpa siku 7??? 'naongea na riz 1 ongea na mshua'..umeiskia hiyo nyimbo ya izzo bizness???
 
Lukuvi asiwafanye wa Tz wajinga ana sema ana mbao pc 1000 zinazo tikana na cbm 1000 za magogo aliyo jipatia kifisadi Saohil mufindi kwa hesabu za kitaalam za magogo cbm 1 ya gogo ina zalisha cbm 0.33 za mbao kwa hesabu ya cbm 1000 za gogo zina zalisha cbm 330 za mbao kwa hesabu ya haraka pcs 1000 za mbao ni sawa na cbm 35 sasa hapa atuambie cbm 295 za mbao ziko wapi cbm 295 za mbao ni magari takribani 10 ya ujazo wa ton 30 ,inaeleweka wazi viongozi wana jipa vitalu vya miti kisha wanauza kila cbm 1 kwa sh 10000 Lukuvi atakua amejipatia tsh 10000000 kwa cbm 1000 tu za gogo
 
Kwenye kipindi cha dk 45 cha Itv lukuvi amesema ni kweli amevuna magogo sao hill kwa lengo la kupaulia shule ya idodi hoja ya msingi shule ile ni ya ccm wazazi ni kwa nini asiwambee wahusika kisha awakabidhi majukumu ya kupasua kuliko yeye kama lukuvi kupasua au alipasua kama ofisi ya mbunge? Kama ni hivyo kuna vithibitisho vya risit mbna pesa aliyotumia ni ya mfuko wa jimbo itakaguliwa.pia ufisadi uko kwenye mbao ulipewa magogo mangapi maana mbao 1000 sio magogo mengi ya kuandikiwa kibari waziri hapo una 10% mbao nyingi umejinuisha nazo
WANA JF ebu tieni mawazo yanayofikirisha
 
Hawa ITV wameandaa kipindi kuwasafisha mafisadi au ??

Mbona hakuna side ya pili, ilitakiwa waweke na watu wa CHADEMA tusikie pande zote mbili.
Na kwa nini hawaruhus maswali ya wananach kwa simu??
 
hivi hicho kipindi kilishawahi kuwahoji viongozi wa upinzani wa kweli???niliacha kukifatilia baada ya kuona jamaa hana uwezo wa kuuliza maswali ya kupekua ukweli
 
Mrs Lema, Lukuvi kaomba kama kuna mtu ana ushahidi alete zaidi ya hapo ni porojo

Lukuvi anaposema utolewe ushahidi kama yeye anamiliki kitalu/vitalu vya misitu huko Mufindi, ndio kusema anakataa kuwa hamiliki? Wizara ya Maliasili imetoa tamko kuwa Lukuvi pamoja na magamba wenzie akiwemo Chami na Simbachamwene wanamilki vitalu huko Mufindi ; sasa anataka ushahidi gani zaidi ya kauli ya wizara husika?
 
Mimi nawashauri ITV wanapowakaribisha mawaziri kwenye kipindi hiki cha Dkt 45 basi na waziri kivuli anayehusika na wizara ya huyo mheshimiwa aalikwe ili wajibizane kwa hoja. Pili ingefaa na itapendeza hicho kipindi kiwe kinarushwa LIVE badala ya ilivyo sasa ambapo kipindi huandaliwa, kufanyiwa masahihisho na matangazo ya kukitangaza nk. Zamani kulikuwepo kipindi kizuri nadhani kiliitwa "Kiti moto" bila kukosea kikiendeshwa na Pasco Mayala waige kile
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom