Applicant
JF-Expert Member
- Feb 12, 2020
- 1,962
- 1,757
Nakumbuka juzi, nilikua nimeenda bank kutoa pesa baada ya kugundua dukani kwangu store imepungua vitu muhimu, kwahiyo nikaenda kutoa salio kidogo ili niweze kwenda kuongeza bidhaa.
Nikaenda bank moja hivi maarufu, nilishangaa kuona hakuna foleni kabisa, nadhani itakua ni kwasababu ya janga hili la corona
Basi nikafika kaunta pale nikiwa tayati nimeshaijaza ile withdrawal sheet na kuitia saini ili niweze kupewa pesa na cashier, nikakamilisha taratibu za kutoa pesa pale bank, dada cashier kwa unyenyekevu mkubwa akanipa kibunda changu nikaondoka zangu (nilifanya kosa kubwa sana kutokuhesabu pesa hiyo siku kwani nina kawaida ya kuzihesabu zote ndio nitoke pale kaunta. )
Wakati nmeshaondoka zangu nimekwenda sehemu ninapotaka kununua bidhaa nikasema ngoja nitoe pesa kwanza maana natakiwa nitoe kiasi kidogo kwa ajili ya matumizi mengine, wakati nachambua pesa, nikakutana na karatasi imeandikwa namba za simu na jina chini, nilipigwa na butwaa sana, moja kwa moja nikajua ni yule dada cashier kaniwekea namba, nikapiga zile namba, kama nilivyodhani ilikua niyeye akaniambia atanitafuta baada ya kutoka kazini amependa tufahamiane zaidi, nilishangaa sana.
Yani kutoa tuu M5 na laki 5 mtu kaniona labda ndio nina maisha mazuri, yani kadata na kiasi kidogo nilichotoa.
Kweli pesa ndio kila kitutafuteni pesa wakuu.