Dada zangu chukueni hizi nasaha

Dada zangu chukueni hizi nasaha

mind ur business

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Posts
416
Reaction score
419
NASAHA 5 KWAKO BINTI YANGU

1. Binti yangu huenda unafikiri wanaume waoaji wenye mipango thabiti watakuoa kwasababu ya sura au umbile lako tu. Tabia, staraha, hekima, akili ya Maisha, utulivu na lugha ndivyo vitashawishi wewe kupata mume.

2. Binti yangu wakati unafanya mambo yako yawe ya kujenga au kubomoa kumbuka umri wako haubaki hapo hapo, mavuno yako ya Kesho yanategemeana na unavyoishi Sasa. Kuna siku utavuna furaha au kilio mwanangu, Mimi baba yako nitafurahi sana ukivuna furaha

3. Binti yangu huenda Kuna watu tayari wamekudanganya eti huu ndiyo muda wa kujirusha na kula bata eti kisa siku za kuishi ni fupi. Mwanangu huu siyo wakati wa kujirusha na kula bata, huu ni muda wa kufanya mambo ya maana na kujitafuta ili ujue Mungu kakupa kitu gani kwa ajili ya watu wengi.

"Usiweke akili yako katika kuwaza siku yako ya kufa labda imekaribia, waza ni kwa namna gani utafikia ndoto zako mwanangu. Kufa kupo tu, siku ikifika Mungu atakutwa, Ila hakikisha kabla hajakutwaa unaishi vyema"

4. Binti yangu najua unatamani Sana uwe na boyfriend, uwe na mume, nisikilize mwanangu haja ya moyo wako Mungu anaijua. Usitumie Nguvu kupata hivi vitu, acha wakati uamue mwanangu

5. Binti yangu ikiwa hujaolewa na unatamani siku moja uolewe Basi hakikisha huwadharau wanaume wote unaokutana njiani bila kujali wakoje au hawana mvuto. Mume wako atatoka miongoni mwa hao ukutanao njiani. Huwezi jua ni Nani Mungu atamnyofoa katikati yao ili aje Kuwa mume wako, waheshimu wote.

6. Usipende hela Sana, kwani pesa sio kila kitu ktk maisha zinaisha.
Pesa hutafutwa, penda pesa za kutafuta kwa mikono yako sio za wanaume, ipo siku zitakutokea puani

[emoji2398]Dec, 2022
------------------------------------------------------------------------
 
Hiyo namba 6 hakuna mwanamke anaweza kuizingati....

Wanawake wote wa Sasa wanapenda hela ,na wanatamaa Sana na maisha mazuri ambayo hawajayatafuta ,mwisho wa siku wanaishiwa kudanganywa na kupigwaa mashine tu ...
 
Back
Top Bottom