Dada yangu pitia hapa

Madihani

JF-Expert Member
Apr 30, 2015
6,079
6,911
Kipindi utakapokubali kutoka kimapenzi na mme wa mtu, utakuwa umekubaliana kuwa mwanamke wa daraja la pili. Na siku zote mtu wa daraja la pili ni mtu wa daraja la chini ukilinganisha na daraja la kwanza.

Angalia sasa...kama yupo na wewe na mke wake akapiga simu atamdanganya mkewe kwamba yupo ofisini au katika kikao na hautakuwa na ujasiri wa kuingilia mawasiliano yake. Pia anapokua nyumbani kwake kwa mkewe huwezi kumpigia au hata kumtumia text.

Dada yangu wewe ni mdoli? Anakuchukua kwenu na gari yake anakupeleka katika vyumba vya hotel lakini mke wake amemkabidhi nyumba nzima. Dada yangu shtuka!!

Anakutembelea nyumbani kwako na unamtambulisha kwa rafiki zako na majirani kwamba ni boyfriend wako bila kujua unajizibia nafasi za kupata mtu sahihi wa kuweza kujenga nae maisha. Na mbaya zaidi hupajui hata yeye anapoishi.

Dada yangu mpaka lini utaendelea kujiharibia future yako? Anatoka na wewe out na anakununulia kila aina ya pombe na wakati huo huo hawezi kumruhusu mkewe kunywa pombe ya aina yoyote ile. Akili ya kawaida ikwambie kwamba anafanya hivyo ili ulewe vilivyo na apate wasaa wa kukukandamiza vizuri kitandani.

Dada yangu Je mwili wako ni wa majaribio? Anakupa mimba na anakupa pesa uende ukaitoe lakini mke wake akipata mimba nyumbani ni sherehe na anampa pesa za kuandaa martenity dress na vitu vya mtoto.

Dada yangu kumbuka tayari anayo familia yake, kama ulikua hujui Jamaa huwaelezea marafiki zake yote mnayofanya hotelini, lakini hata siku moja hawezi kuwalezea yale anayofanya na mkewe. Hii inafanya marafiki zake wakuone kama mwanamke wa hadhi ya chini kabisa.

Unazo picha zake katika simu yako na ume save namba yake kwa majina mazuri kama Sweetheart, My love, etc... Lakini picha zako haziwezi kupatikana ktk simu yake na namba yako amei Save kama Fundi Genereta, Fundi gari, Mzibua Chemba.

Unatakiwa ukumbuke kwamba mwanamke asie na akili sehemu zake za siri ndizo zitakazoumia zaidi.

Amka dada yangu unatumika
 
Uzi uko 700 viewers ila replies ni 13 tu na wote wanaume..Iko shida hakuna wakuwatoa kimasomaso?
 
Aiseeee Mimi nilikuwa naupita tuu kwa mbalii kumbe una maneno kuntuu namna hiii aiseeee
 
Mmmh mbona haya tunayajua? Inategemea ni mme wa aina gani acha kabisa ukipata mtu anaejitambua mbona unaenjoy? Kila mtu anapata fungu lake trust me kuna mchepuka unaweza kujali mke wa mje kuliko wa ndani na heshima ikafata mkondo wake, kaya haya yoteeee tunayajua nikipata anaendana na mie akuuuu tunatafunana na nikikuta ni msafiiiiiiii anajariiiii zile type zangu loh sumu ya mwanaume wa hivi wa aina hii lazima iniuwe ahaaaaa
 
Ukweli mtupu waume wa watu hawana mapenzi ya kweli zaidi ya kutafta sehemu ya kutolea hamu zao tu basi
 
Mambo ya Ngoswe, muachie Ngoswe mwenyewe.

Kwani dada yako mtoto?

Kama mtu mzima, anayajua yote hayo, na kaamua kuendelea hivyo, wewe kipi kinakufanya kuingilia maisha yake?

Kila mtu kivyake.

Unataka kumuoa huyo dada yako?

Au wewe ndiye unataka kuwa mchepuko wa mwanamme mwingine?

Kwa nini unashikia bango habari za faragha za watu wazima wenzio?

Tabia mbaya hiyo.
 
Back
Top Bottom