Dada yangu ni Mama Yangu

Page 94

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
5,204
15,198
Ikiwa Leo ni siku ya Mama duniani, kila mmoja wetu angelipenda kumshukuru na kumjalia kheri mama yake mzazi/ mlezi katika mengi aliyomtendea kwa upendo usiokwisha. Wengine pia huwaombea tulizo la mioyoyo wote waliokwisha tangulia mbele ya haki.

Naam, vivyo hivyo namuombea Baraka tele na maisha marefu dada yangu. Ndiyo, dada yangu ni mama yangu. My sister is my mother.

Ilikuwa ni siku ya furaha sana kumpata mtoto wa kiume 'Compact'. Lakini, ilikuwa pia ni siku ya huzuni kuondokewa na Mama kipenzi.
Siku angali nazaliwa, ni siku ambayo mama yangu alipoteza maisha dakika chache tu baada ya kunitua katika Ulimwengu huu.

Wakunga wetu wa jadi, walijitahidi sana kuyaokoa maisha ya mama pamoja nami. Lakini, ilifika hatua kuwa ni lazima mmoja angeliondoka ama wote kwa ujumla. Ndiyo, mimi nilipona huku mama akiondoka. Ndivyo ambavyo ilikuwa, huzuni iliizidi furaha ya siku tajwa.

Kwa kutambua kuwa hakuwa na muda mrefu zaidi kuendelea kuwepo kutokana na hali yake kuwa mbaya sana, punde baada ya kunitua alinikumbatia kisha kunipa jina. Utaitwa Compact, Dakika chache baadaye alikata roho na kuzimika kama kibatari kilichokwisha mafuta. Ndiye, nilimpoteza mama. Aliondoka huku nikiwa sijaligusa hata ziwa lake na kulitia mdomoni. Hakika ni siku mbaya sana kuikumbuka.

Taratibu zote za kumpumzisha katika nyumba yake ya milele zilifanyika, kutokana na taratibu zetu kesho yake mchana tu baada ya kujifungua, alipumzishwa katika nyumba hiyo ya milele. Ndipo jukumu zito lilipowadia la kumtunza kiumbe changa kilichobaki. Je, ni nani angeliwajibika katika kumtunza Compact?

Jukumu hili lilimuangukia Dada yangu. Kifungua mimba wa familia. Alikuwa na miezi mitatu tu punde baada ya kujifungua. Alikuwa na mtoto mdogo lakini alikuwa anahitajika kujichukulia majukumu mengine makubwa zaidi katika umri wake wa miaka kumi na saba tu. Kuhakikisha Compact anakuwa mzima na kudunda katika maisha haya mapya ya Ulimwengu.

Kutokana na majukumu hayo, ilimlazimu kumuachisha mwanaye kunyonya ili mimi nijipatie nafasi ya kupata maziwa ya kutosha kutokana na Ukweli kuwa asingeliweza kunyonyesha wote kwa wakati mmoja. Mwanawe wa miezi mitatu tu aliachwisha nyonyo la mama yake mzazi, ili tu mtoto mwingine apate kulinyonya na kushiba. Hakika, ni mapenzi ya ajabu. Mtoto wake alianza kulishwa maziwa ya ng'ombe pamoja na uji mwepesi huku mimi nikiyafurahia maziwa matamu na ya moto kutoka katika ziwa la dada yangu.

Ilikuwa ya siku, miezi na hata miaka. Katika maisha yangu ya kukua, siku zote nililitambua kuwa Dada yangu ndiye mama yangu mzazi, huku nikitambua kuwa mpwa wangu alikuwa ni pacha wangu. La Hasha!. Alikuwa ni dada yangu. Baada ya kulitimiza mwaka mmoja, dada yangu sasa analipaswa kwenda kwa mumewe. Kuijenga familia yake. Kuiacha familia ya mama yake ambaye yeye ndiye aliyebeba majukumu yote ya mama. Sasa watoto walipaswa kujihudumia wenyewe.

Kuondoka kwake, ilimpasa aniache na aondoke na mwanae pekee. Lakini, haikuwa hivyo. Alinichukua pamoja nami na kwenda kuanza maisha mengine mapya ugenini. Tulikua pamoja, nikimuita mama na yeye akiniita mwanae.

Baadae nilianza shule kisha kuhitimu elimu ya Msingi. Mara kadhaa tulikuwa tukipatembelea nyumbani kuwajulia hali ndugu. Baba (huku nikimuita babu) alikuwa akija, na kutujulia hali pia. Sasa nimeanza kidato cha Kwanza. Mara zote nilisoma katika shule za kulala (boarding), kuanzia msingi mpaka sekondari.

Sikuwahi kufikiria kama yule hakuwa mama yangu. Sikuwahi kuitambua tofauti yeyote kwa mapenzi yake yasiyokwisha. Sikuelewa tofauti ya majina yaliyopo kati yangu na mpwa wangu. Niliwahi kumuuliza, akanipiga chenga na kupuuzia.

Wakati nimemaliza mitihani ya kidato cha pili na kurejea nyumbani, mama alinitaarifu siku siyo nyingi tungeliwatembelea kule nyumbani. Siku imewadia, tukafunga safari na kuondoka. Tulipokelewa vema tu.
Siku ya pili yake kulikuwa na kikao cha kifamilia. Naam, kikao ambacho ningeliambiwa kuwa huyo hakuwa mama yangu bali dada yangu.

Mzee aliongea mengi kisha akanambia, kuna jambo ambalo hulijui na leo ungelipaswa ujue. Nilimuangalia dada yangu akiinama. Nilitambua kuwa analia machozi. Ndipo akanitambulisha kuwa huyo alikuwa ni dada yangu tu, wala siyo mama. Sikuliamini maneno hayo, lakini iliwabidi kwenda kunionyesha alipolazwa mama. Mara nyingi tumekuwa tukifika hapo, na kuelezwa kuwa ni sehemu alipolazwa bibi. Leo nangaliambiwa siyo bibi bali ni mama. Hakika haikuwa siku nzuri hata kidogo kwangu. Nililia kulikopitiliza.

Hakika nisingeweza kuhisi tofauti kwa mapenzi yale aliyokuwa nayo dada yangu juu yangu. Nilimpoteza mama lakini nilimpata mama.

Hapakuwepo na hata picha moja kunionyesha mama halisi alivyofanania. Cha ajabu ni kuwa, sura yake niliijua kabla. Siku naambiwa, alikuwepo mama yangu mdogo ambaye niliambiwa alifanana sana na mama. Sura yake hii ilifanana sana na sura ambayo imekuwa ikinitokea ndotoni, hata kabla ya kutambulishwa kwake. Hakika, Mungu ni wa ajabu.

Naam, kwa siku hii muhimu napenda kumshukuru sana dada yangu. Mapenzi yake hakika hayapimiki na nachelea kusema alivaa vazi vema zaidi ya mama katika malezi yake kwangu. Hakika wewe ni Mama yangu. Una nafasi kubwa sana katika maisha yangu, mosi kama dada na zaidi kama Mama. Ahsante sana kwa yote. Mungu akujalizie maisha marefu zaidi hapa duniani. Niendelee kuwa nawe katika kipindi kirefu. Niendelee kuhisi pendo lako lisilokwisha....

Pumzika kwa amani mama, uliondoka lakini uliniachia mama mwingine.

Happy Mama's Day to you my sister, Neema.

My Sister is my Mother.
 
V
Ikiwa Leo ni siku ya Mama duniani, kila mmoja wetu angelipenda kumshukuru na kumjalia kheri mama yake mzazi/ mlezi katika mengi aliyomtendea kwa upendo usiokwisha. Wengine pia huwaombea tulizo la mioyoyo wote waliokwisha tangulia mbele ya haki.

Naam, vivyo hivyo namuombea Baraka tele na maisha marefu dada yangu. Ndiyo, dada yangu ni mama yangu. My sister is my mother.

Ilikuwa ni siku ya furaha sana kumpata mtoto wa kiume 'Compact'. Lakini, ilikuwa pia ni siku ya huzuni kuondokewa na Mama kipenzi.
Siku angali nazaliwa, ni siku ambayo mama yangu alipoteza maisha dakika chache tu baada ya kunitua katika Ulimwengu huu.

Wakunga wetu wa jadi, walijitahidi sana kuyaokoa maisha ya mama pamoja nami. Lakini, ilifika hatua kuwa ni lazima mmoja angeliondoka ama wote kwa ujumla. Ndiyo, mimi nilipona huku mama akiondoka. Ndivyo ambavyo ilikuwa, huzuni iliizidi furaha ya siku tajwa.

Kwa kutambua kuwa hakuwa na muda mrefu zaidi kuendelea kuwepo kutokana na hali yake kuwa mbaya sana, punde baada ya kunitua alinikumbatia kisha kunipa jina. Utaitwa Compact, Dakika chache baadaye alikata roho na kuzimika kama kibatari kilichokwisha mafuta. Ndiye, nilimpoteza mama. Aliondoka huku nikiwa sijaligusa hata ziwa lake na kulitia mdomoni. Hakika ni siku mbaya sana kuikumbuka.

Taratibu zote za kumpumzisha katika nyumba yake ya milele zilifanyika, kutokana na taratibu zetu kesho yake mchana tu baada ya kujifungua, alipumzishwa katika nyumba hiyo ya milele. Ndipo jukumu zito lilipowadia la kumtunza kiumbe changa kilichobaki. Je, ni nani angeliwajibika katika kumtunza Compact?

Jukumu hili lilimuangukia Dada yangu. Kifungua mimba wa familia. Alikuwa na miezi mitatu tu punde baada ya kujifungua. Alikuwa na mtoto mdogo lakini alikuwa anahitajika kujichukulia majukumu mengine makubwa zaidi katika umri wake wa miaka kumi na saba tu. Kuhakikisha Compact anakuwa mzima na kudunda katika maisha haya mapya ya Ulimwengu.

Kutokana na majukumu hayo, ilimlazimu kumuachisha mwanaye kunyonya ili mimi nijipatie nafasi ya kupata maziwa ya kutosha kutokana na Ukweli kuwa asingeliweza kunyonyesha wote kwa wakati mmoja. Mwanawe wa miezi mitatu tu aliachwisha nyonyo la mama yake mzazi, ili mtu mtoto mwingine apate kulinyonya na kushiba. Hakika, ni mapenzi ya ajabu. Mtoto wake alianza kulishwa maziwa ya ng'ombe pamoja na uji mwepesi huku mimi nikiyafurahia maziwa matamu na ya moto kutoka katika ziwa la dada yangu.

Ilikuwa ya siku, miezi na hata miaka. Katika maisha yangu ya kukua, siku zote nililitambua kuwa Dada yangu ndiye mama yangu mzazi, huku nikitambua kuwa mpwa wangu alikuwa ni pacha wangu. La Hasha!. Alikuwa ni dada yangu. Baada ya kulitimiza mwaka mmoja, dada yangu sasa analipaswa kwenda kwa mumewe. Kuijenga familia yake. Kuiacha familia ya mama yake ambaye yeye ndiye aliyebeba majukumu yote ya mama. Sasa watoto walipaswa kujihudumia wenyewe.

Kuondoka kwake, ilimpasa aniache na aondoke na mwanae pekee. Lakini, haikuwa hivyo. Alinichukua pamoja nami na kwenda kuanza maisha mengine mapya ugenini. Tulikua pamoja, nikimuita mama na yeye akiniita mwanae.

Baadae nilianza shule kisha kuhitimu elimu ya Msingi. Mara kadhaa tulikuwa tukipatembelea nyumbani kuwajulia hali ndugu. Baba (huku nikimuita babu) alikuwa akija, na kutujulia hali pia. Sasa nimeanza kidato cha Kwanza. Mara zote nilisoma katika shule za kulala (boarding), kuanzia msingi mpaka sekondari.

Sikuwahi kufikiria kama yule hakuwa mama yangu. Sikuwahi kuitambua tofauti yeyote kwa mapenzi yake yasiyokwisha. Sikuelewa tofauti ya majina yaliyopo kati yangu na mpwa wangu. Niliwahi kumuuliza, akanipiga chenga na kupuuzia.

Wakati nimemaliza mitihani ya kidato cha pili na kurejea nyumbani, mama alinitaarifu siku siyo nyingi tungeliwatembelea kule nyumbani. Siku imewadia, tukafunga safari na kuondoka. Tulipokelewa vema tu.
Siku ya pili yake kulikuwa na kikao cha kifamilia. Naam, kikao ambacho ningeliambiwa kuwa huyo hakuwa mama yangu bali dada yangu.

Mzee aliongea mengi kisha akanambia, kuna jambo ambalo hulijui na leo ungelipaswa ujue. Nilimuangalia dada yangu akiinama. Nilitambua kuwa analia machozi. Ndipo akanitambulisha kuwa huyo alikuwa ni dada yangu tu, wala siyo mama. Sikuliamini maneno hayo, lakini iliwabidi kwenda kunionyesha alipolazwa mama. Mara nyingi tumekuwa tukifika hapo, na kuelezwa kuwa ni sehemu alipolazwa bibi. Leo nangaliambiwa siyo bibi bali ni mama. Hakika haikuwa siku nzuri hata kidogo kwangu. Nililia kulikopitiliza.

Hakika nisingeweza kuhisi tofauti kwa mapenzi yale aliyokuwa nayo dada yangu juu yangu. Nilimpoteza mama lakini nilimpata mama.

Hapakuwepo na hata picha moja kunionyesha mama halisi alivyofanania. Cha ajabu ni kuwa, sura yake niliijua kabla. Siku naambiwa, alikuwepo mama yangu mdogo ambaye niliambiwa alifanana sana na mama. Sura yake hii ilifanana sana na sura ambayo imekuwa ikinitokea ndotoni, hata kabla ya kutambulishwa kwake. Hakika, Mungu ni wa ajabu.

Naam, kwa siku hii muhimu napenda kumshukuru sana dada yangu. Mapenzi yake hakika hayapimiki na nachelea kusema alivaa vazi vema zaidi ya mama katika malezi yake kwangu. Hakika wewe ni Mama yangu. Una nafasi kubwa saba katika maisha yangu, mosi kama dada na zaidi kama Mama. Ahsante sana kwa yote. Mungu akujalizie maisha marefu zaidi hapa duniani. Niendelee kuwa nawe katika kipindi kirefu. Niendelee kuhisi pendo lako lisilokwisha....

Happy Mama's Day to you my sister, Neema.

My Sister is my Mother.

Very touching, yote ni mapenzi ya Mungu.
 
Pole sana mkuu na hongera kwa kumpata dada aliye zaidi ya mama... Amini kila jambo linalotokea Mungu huwa na Makusudi yake.

Pamoja na kumchukua mama lakini alikupa mwingine ambae amekufanya uhisi upendo wa mama, Mshukuru Mungu kwa hilo..

Mama ni nguzo hapa duniani, nampenda sanaa Mamangu jamani.

Happy mother's day....
 
Ahsante Mkuu Sakayo, barikiwa sana.
 
Back
Top Bottom