Dada yangu atapata haki Kisheria baada ya talaka?

Dada yangu atapata haki Kisheria baada ya talaka?

Kabisa....
Na si tu kuacha mali...kuishi na mtu mzinzi for 12 yrs.... kama kathubutu kumwambia aondoke ni mangapi ashamwambia?

Inawezekana miaka yote mwanamke huyu anavumilia manyanyaso matusi dharau na pia anahatarisha maisha yake....

Wengi wanajibu kinadharia na si kiuhalisia.... sio rahisi kiasi hicho kama watu wanavyochukulia.

Ulivyo muuliza swali hili nimekaa on line kuona atajibu nini! unajua hapa kwenye key board ni rahisi kumshauri mwenzio aache mali wakati alishiriki miaka yote na akaweka nguvu zote kuzitafuta na mumewe kuzitafuta!

Nimejiuliza kweli ni kama ingekuwa ni ndugu yake angesema hayo?
 
Kabisa....
Na si tu kuacha mali...kuishi na mtu mzinzi for 12 yrs.... kama kathubutu kumwambia aondoke ni mangapi ashamwambia?

Inawezekana miaka yote mwanamke huyu anavumilia manyanyaso matusi dharau na pia anahatarisha maisha yake....

Wengi wanajibu kinadharia na si kiuhalisia.... sio rahisi kiasi hicho kama watu wanavyochukulia.
Mimi huwa sipendi kumshauri mtu adai talaka au atoe talaka lakini linapo kuja swala la afya ya mtu hakika hakuna ushauri mwingine zaidi ya kushauri kuachana na ndoa!

Unajua watu wanafikiri ndoa ni gereza kiasi kwamba wako tayari kuhatarisha afya zao kama huyu dada alivyo fanya!

Kama kweli hii ni habari ya kweli hakika huyu dada anatakiwa kukimbilia hospitali kupima afya kabla ya kuanza process zote!

Kwa hali yoyote atakayo kutwa nayo ni lazima akubali kusonga mbele asikubali kurudi nyuma kuendelea na huyu jamaa!

Katika mazingira kama haya sidhani kama kuna ushauri mwingine zaidi ya huu! Ni unafiki kumwambia mtu aendelee kuvumilia katika hali kama hii!
 
Na mimi nina mtazamo kama wako mkuu, sema ni wachache wa kuelewa unachoongea. Sijui atoto, Heaven Sent, Eli79 wanasemaje manake sijawasoma kwenye uzi huu

Niliwaiga kusema ni bora uendelee kuwa nyumba kubwa kuliko kuachika na kwenda kuwa nyumba ndogo
My kaka mito niliona mention yako but now kwenye simu hata siioni. Anyway I will just give my opinion (sorry kwa mgazeti)

Me nachoamini hakuna mahusiano yanayodumu pasipo uvumilivu. Ingawa binadamu tumeumbwa pia na uvumilivu wenye kikomo. Kuna mahali Inafika kwa akili tu za kibinadamu unaona kabisa hapa siwezi tena kuendelea.

Mie kwenye suala la uvumilivu najitahidigi kidogo as Najua hakuna aliye mkamilifu na hakuna maisha yasiyo na challenges za hapa na pale. But pale napoona situation, mahusiano au kitu ni a big threat kwa afya yangu au my piece of mind. Then uvumilivu wangu huwa unaishia hapo hapo. Kukaa ndani kusubiri mtu aniletee magonjwa yake kisa kuhangaika kwake, naomba Mungu aniepushie mja wake.

Hakuna kitu kigumu kama kumshauri mtu abreak up/ divorce. Kwa sababu issue inaweza ikawa rahisi kwangu but kwa mwingine ikawa ngumu. Na kama tunavyojua kutoa ushauri ni rahisi sana as wewe haupo kwenye viatu vya muhusika. It happened na mimi nilishawahi kuapa kwamba mwanaume akinifanyia tu hivi nampiga chini, but ukute nilifanyiwa, sikumpiga chini but mwishowe mwenyewe ikabidi tu aniache tena kinguvu khaaa.

Siku hizi rate ya uvumilivu inapungua, unlike hapo zamani ambapo mama alikuwa tegemezi tu akisubiri kila kitu kwa baba. Kwa hiyo hata mtu akifanywaje utasikia siwezi kuondoka kwa sababu tu ya wanangu. But sasa hivi wanawake wanapiga kazi, akiona stress zimezidi anaona khaa mbona hata nikiondoka naweza kutunza wanangu vizuri, why ndoa igeuke kaburi?.

Mwisho wa siku unamuacha mtu aamue ni nini anakitaka kwa ajili yake. Wapo waliovumilia na wakaokoa ndoa zao, wapo waliovumilia wakaambulia magonjwa au kufa kwa presha na kuacha watoto wanahangaika. Kwa hiyo mtu alie na Mungu wake ili aonyeshwe kama still kuna kitu cha kuvumilia. Maana kuna muda unaona kabisa hapa hakuna kitu cha kuvumilia .
Mambo mengine huwezi kujua ugumu/ urahisi wake hadi yakutokee. Kwa huyu mama as mumewe ndo kaamua kutoa talaka, unadhani utafanyaje, you can't keep a person who doesn't want to be kept. afate tu sheria ili apate stahiki zake basi maisha yaendelee. Ndo upeo wangu mdogo ulivyowaza kwa sasa
 
Last edited by a moderator:
Umeongea vizuri Heaven Sent na nimekuelewa vizuri. Kwa experience yangu nimeona wanawake wa kutosha tu wakivunja ndoa zake sababu ya uzinzi wa waume zao. Tatizo wakishaachika na wao wanaanza kurukarukaa tu, akibahatika anaishia kuwa nyumba ndogo. So najiulizaga iweje umekataa kuwa nyumba kubwa sababu ya uzinzi wa mumeo, mbona sasa na wewe unafanya yale yale, hadi umekuwa small house sasa??
 
Last edited by a moderator:
Dada yangu ndoa yake ina mgogoro 4 2months, wana 12yrs, ndoa yakikristo, 3kids ke 10yrs, me 8yrs, me 4yrs. chanzo ni uzinzi wamume uliokithiri, anazini na wanafunzi, wanawake wamtandaoni, karibu kila kona anahawara, mara yamwisho dada alifuma sms kwenye simu ya shem, inasema,
''mke wangu nakumiss sana napanga nije tena Arusha tumtafutie Bryan mdogo wake amekua sana, mke huyo akamjibu we mi naogopa usije ukanitelekeza tena.''

Dada akamuuliza kumbe una hawara hadi umezaa nae? Mume kawa mkali anadai dada hana adabu kwanini apekuepekue simu yamumewe? Mke akalia sana mume hajali, sasa hawasemeshani kilammoja anafanya lake, mke anajiendeleza chuo, hutoka asubuhi anarudi jioni kimya, jana kaja kwangu tumeshinda kanisani maombi, kufika kwake ugomvi ukatibuka mume anadai J4 ataenda kumpa talaka mahakamani sababu anakiburi eti watu huishi nawanaume malaya nakuwaheshimu, kwanini ye hamheshimu kaambiwa awaache watoto kwamume, namali zote haziache nizawatoto, mume ataziangalia, dada anataka wanae na mali.

Je, atapewa wanae namali kweli?

1. Mahakama pekee ndo chombo cha kisheria kuvunja ndoa.

NOTE: Kuvunja ndoa maana yake ni MAhakama inatoa TALAKA.
NOTE: Spouse yeyote (me au ke) anaweza kwenda mahakamani kuomba kuvunja ndoa.

2. Ili ndoa ivunjwe, (yaani mahakama iridhike na ushahidi na kutoa TALAKA), inabidi wanandoa wapitie kwanza kwenye Baraza la Usuluhishi la Ndoa (Marriage Reconciliation Board) ili wasuluhishwe kwanza. Suluhu isipopatikana hapo, ndo suala linakuwa referred to Court ambapo huko sasa itafunguliwa kama kesi ya kawaida ya madai, na muombaji-talaka atatakiwa kutoa ushahidi wake as to why anaomba ndoa ivunjwe.

NOTE: Hizo marriage reconciliation boards ni: Baraza la Kata and/or Baraza la Kanisa (hii ni kwa wakristo); BAKWATA (hii ni kwa waislamu)

3. NDOA ikishavunjwa rasmi (yani TALAKA ikitolewa), kuna mambo makuu matatu hufuatia:

(a)
Distribution of Matrimonial Properties - Mgawanyo wa mali za ndoa.
(b) Custody of children - Kwamba ni nani (kati ya baba au mama) atakaa na watoto.
(c) Maintenance of children - Kwamba ni nani (kati ya baba au mama) ataprovide matunzo kwa watoto, bila kujali wanakaa kwa yupi.

NOTE: Hapo kwenye (a), matrimonial properties ni zile mali ambazo zimechumwa/zimepatikana kwa juhudi za pamoja (jointly acquired) ndani ya ndoa yenu, yaani ni zile ambazo zimepatikana kuanzia ile tarehe mlipofunga ndoa rasmi. Hata kama zilipatikana jointly ila kabla ya kufunga ndoa, basi uwe na ushahidi wa kuthibitisha hilo ili upate haki yako.

NOTE: Hapo kwenye (a), sheria inatambua uwepo wa mali binafsi katika ndoa, yaani kila mwanandoa anaweza kumiliki mali zake yeye mwenyewe binafsi, separately na zile mali za ndoa. Mali hizi za umiliki binafsi huwa hazijumuishwi kwenye mgao wa mali za ndoa. So hapo pia ni suala la ushahidi ili usidhurumiwe.

NOTE: Hapo kwenye (b), Kisheria, mtoto mwenye umri chini ya miaka 7, inatakiwa akakae kwa mama. Cha msingi hapa ni kwamba katika kuamua mtoto akakae kwa aidha mama au baba, Mahakama huzingatia zaidi maslahi bora na ustawi wa mtoto (the best interest of the child) mfano uwezekano wa kupata malezi bora ya kimaadili, elimu, n.k. Mfano: mama kama ana tabia za ulevi wa kupindukia, au labda mama huwa ana matatizo ya akili, au labda ni mtu wa kusafiri-safiri sana, au labda ana tabia chafu na ushahidi ukatolewa, basi Mahakama is likely kumnyang'anya/kumnyima mtoto. Pia katika hili, mtoto mwenyewe huulizwa kwamba je anapenda akae na nani.

NOTE: Hapo kwenye (c), kisheria, baba (biological father) ndo mwenye responsibility kubwa katika matunzo ya mtoto/watoto, regardless wanakaa kwa yupi. So, ata kama mahakama ikaamua kwamba watoto wakakae kwa mama, still baba anabanwa kisheria kuprovide full matunzo kwa watoto. Endapo baba hajiwezi kiuchumi ama hajiwezi kivyovyote vile, basi mama pia ana responsibility ya kutoa matunzo kwa mtoto/watoto. So, jukumu la matunzo kwa watoto ni la wote baba & mama.

Mkuu cloudear, hopefully umepata majibu ya hoja yako kwenye maelezo hayo mafupi.

-Kaveli-
 
Last edited by a moderator:
Umeongea vizuri Heaven Sent na nimekuelewa vizuri. Kwa experience yangu nimeona wanawake wa kutosha tu wakivunja ndoa zake sababu ya uzinzi wa waume zao. Tatizo wakishaachika na wao wanaanza kurukarukaa tu, akibahatika anaishia kuwa nyumba ndogo. So najiulizaga iweje umekataa kuwa nyumba kubwa sababu ya uzinzi wa mumeo, mbona sasa na wewe unafanya yale yale, hadi umekuwa small house sasa??

Mahusiano ya michepuko ni kama part time tu ujue. Yanakuwa mahusiano yanayoinvolve interest zaidi za wahusika. Mchepuko ukikuzingua si unautema tu fasta unlike kwenye ndoa. Mind you akiwa mchepuko hapati stress kama anazopata mke wa ndoa. Wao ni mahaba tu, karaha peleka kwa mkeo. So watalaka wengi hawataki kuingia kwenye ndoa kuavoid waliyotendewa na waume zao. Anakuwa part time ya mume wa mtu atimiziwe mahitaji yake ya kimwili basiii.

Halafu kingine kuachana si kitu rahisi as tunavyokidiscuss. It takes time and courage mtu kuanza maisha mapya alone au na watoto wako bila ya mume. Watu kama hawa wasipokuwa na watu wa kuwaongoza basi hawakawii "kujichanganya". Kwa sababu yale maisha mapya wanayoyaanza ni maisha ya upweke na yatachukua muda kidogo hadi mtu aje asimame vizuri. Usishangae mtu kakimbia ndoa kaenda kuwa nyumba ndogo.
 
Mmh basi sawa aisee, khaaa!!
 
yaani wewe mdada huwa nakukubali sana yo so smart, nakusomaga sana na yule bosi wako atoto
 
Last edited by a moderator:
Mmh basi sawa aisee, khaaa!!
My kaka hiyo khaaa hadi nimecheka. Sikiliza sana "majigambo" ya michepuko, utaona kama ina stress. Wao ni wakuenjoy tu .. ukifulia, ukiugua, ukifariki wao haiwahusu, ni kazi ya mkeo
 
My kaka hiyo khaaa hadi nimecheka. Sikiliza sana "majigambo" ya michepuko, utaona kama ina stress. Wao ni wakuenjoy tu .. ukifulia, ukiugua, ukifariki wao haiwahusu, ni kazi ya mkeo

Kumbe ndo maana wengine wamechagua kuwa michepuko tu, mi nilidhani ni kukosa wa kuwaoa kumbe kwa baadhi ni choice, and they are happy with it
 
Last edited by a moderator:
Kumbe ndo maana wengine wamechagua kuwa michepuko tu, mi nilidhani ni kukosa wa kuwaoa kumbe kwa baadhi ni choice, and they are happy with it

Ofcoz my kaka didnt you knew? Kuna anayekosa wa kumuoa kweli? Sema "mtu sahihi wa kumuoa"
 
Kumbe ndo maana wengine wamechagua kuwa michepuko tu, mi nilidhani ni kukosa wa kuwaoa kumbe kwa baadhi ni choice, and they are happy with it
Aaah mbona hiyo lifestyle ni common sana siku hizi. Kuna watu wameamua tu kuwa michepuko na wanaenjoy tu kuwa hivyo
 
Ofcoz my kaka didnt you knew? Kuna anayekosa wa kumuoa kweli? Sema "mtu sahihi wa kumuoa"

Hahaaa point imefika kwa mwenyewe sasa!!! ila nakuaminia dadaangu
 
Back
Top Bottom