Dada yangu anataka kutumia cheti changu

Dada yangu anataka kutumia cheti changu

lady cnta

Member
Joined
Jan 29, 2018
Posts
71
Reaction score
69
Wabari wapendwa.

Nipo kwenu kwa wadau wa Elimu kuomba ushauri.

Nina dadaangu wa damu kabisaaa ambae amekua akini sarport ktk masomo yangu, yaani amekua akinisaidia kwa kila kitu, kwanzia mambo ya ada na mengine mengi tu.

Sasa tatizo linakuja dadaangu anataka aende kusoma chuo ila atumie Cheri changu cha Academic cha 4m 4.
Huku akijua mm nasoma chuo cha serikali nipo mwaka wa tatu yeye anataka apply chuo cha private, nikamuuliza huoni tatizo kutumia Nina langu namm bado nasoma hv necta wakiona Jina moja linatumika mala mbili kwenye database yao si nitafutiwa mitihani?,

Anasema hawawezi mind coz wanao apply ni wengi alafu anatumia chuo cha private na tupo mikoa tofauti.

Wakuu hembu naombeni ushauri hii kitu haita niletea shida, maana yy anadai mbona wapo watu wengi anawafahamu wametumia vyeti vya ndugu na wapo wanafanya kazi, wengine wameajiriwa na selikali.

Huyu dadaangu alimaliza Form four miaka hiyo, lakini alifeli mitihan yke, na sasa anabiashara zake Ila anataka akasomee business administration ili aweze kusimamia vizuri biashara zake.

Ushauri wenu wakuu, sitafutiwa mitihan
 
Mwambie aache tamaa

Kama anaweza kukusuport kwa kila kitu anachohangaikia ni nini,aendeleze biashara zake maisha yasonge
 
Mwambie mwanzo Wa vyeti feki ni kama hivyo mnavyo taka kufanya, mbeleni mtajiletea matatizo.
 
Zama zimebadilika mkuu, acha kabisa hii kitu
 
Usirogwe kabisa pamoja na upendo aliokufanyia dunia tulio kuwa nayo sasa usijaribu. Hiyo namba ikiingizwa tu TCU/NACTE itapiga hodi yenyewe hadi NECTA na itakuweka pabaya. Kama anataka aangalie njia nyingine za kujifunza atafanikiwa asipige short cut. All the best.
 
Back
Top Bottom