Dada yangu anapitia mateso makali sana sababu ya kijana wake kushika Dini hadi imemfanya amekuwa mjinga

Dada yangu 49 years now ameajiriwa kwenye Hospitali Binafsi kubwa sana hapa Dar , ana kijana wake wa kiume ambae ndio alitegemea aje hata aonyeshe njia maana watoto wake wengine ni tia maji wote wanamsumbua huyu ndio alijua atakuja kumfuta machozi, Cha kwaza kijana wakati yupo form six tu walifukuzwa shule yeye na wenzake 4 sababu ya kuanzisha makundi ya kidini yenye misimamo isiyoeleweka na kufanya vurugu, ikabidi Dada amtafutie shule nyingine private kwa garama kubwa kumnusuru.

Dogo akamaliza Advance akaaply Chuo cha udaktari Tanga huko hali ilivyokuwa ngmu maana Baba yake hakuwa na msaada wowote Dada akakopa sh milioni 5 pale kazini kwake kwa ajili ya kumsomesha tena hiyo milioni 5 ilikata ikabidi awe anapambana kuongezea hela sehem nyingine, Dogo akapiga kitabu akamaliza kwa tabu sana.

Mwaka 2020 Dada kwa sababu ni Mkongwe pale kwenye Hosptitali anayofanya kazi akafanya juu chini kumuombea nafasi na moja kwa moja Dogo akapata nafasi ya kuajiriwa kama Daktari

Balaa likaanza Dogo baada ya kujiriwa tu akawa anakuja kazini Amevaa Nusukanzu,Kobazi na Kibarakashia huku Anafuga Ndevu kama Osama, hadi akawa anatisha waajiri wake ikabidi Sister aitwe haraka sana akaambiwa kuwa Huyu kama ni mwanao basi kaa nae umkanye mara moja kuwa Yale hayakuwa mavazi sahihi kwa mafanyakazi akashauriwa kuwa avae mavazi official ambayo yapo kwenye muongozo kwa mujibu wa kazi

Sister ikabidi amuite Dogo amkanye kuwa Uongozi pale wamemkanya ajirekebishe ile ni Hospitali kubwa na ni lizima afuate miongozo, Dogo akawa mbishi na alipoona anazongwa sana kwa lile swala akaacha kazi kabisa kwa Hasira akaenda mikoani huko akawa anajihusisha na mambo ya kidini

Kuanzia kipindi hicho Dada yangu ni presha za kupanda tu na kushuka, Juzi kati hapa hadi akazimia maana kijana alikengeuka akawa hamuheshimu na hama maisha ya kueleweka tena na ukiangali amechoma zaidi ya milioni 7 kumsomeaha na hadi leo hii hana kiwanja wala nyumba amepanga
Huyo ameshakuwa gaidi, mark my words. Soon atamwona Somalia na alshabab.
 
Ndio madhara ya kusomesha mtoto ukitengemea akianiriwa upate sehemu ya mshahara wake,mm nilidhani mvuta bnghe mwizi mlevi mzizi kumbe kachagua njia nzuli sana ya mitume na manabii ifahamike kusoma sio lazima uajiriwe huyo mama hasimkatie tamaa amuuluze kazi anayo iweze amuwezeshe tu
Andika tukuelewe bhana
 
Maarifa hukaa penye akili zilizotimia, mtu mwenye kasoro kwenye akili umpa maalifa nusu nusu utakuta kaua watu uko, sasa kama anafikia hatua ya kumtelekeza mama ake wakati ndo sehemu yakujipatia pepo hapo kuna tatizo chamsingii tumwombee apate mtu mzuri wakumuelekeza.
Kitendo cha kutomuheshimu mama yake tu kishakosea. Tumeambiwa Tumuamini Mungu na Mtume wake na tuwaheshimu wazazi wawili.

Huyu hajasoma dini bali kakutana na vigenge vya wahuni

Na Allah Amhidi
 
Sijui kwann mababa huwa wanadharaulika. Mzee wa watu alishamuona dogo na uchizi wake akaamua kumpotezea mkamuona fala mzee wa watu mkaenda kukopa kumsomesha dogo. Ukute mkatoa na kashfa kibao kwa mshua. Haya sasa mkakope tena mumtibie dogo afya ya akili
Tunaweza kuwa tunamuonea huruma mother kumbe mtoto alishakuwaga mwehu kitambo tu ndiyo maana mzee akaachana naye.
 
Huyo dada mbona anajitesa mwenyewe? Mwambie kosa analo yeye kwa kutumainia mwanadamu hasa huyo Dr wake, yeye ilipaswa azae katika uwezo wake wa kulea kama jukumu lake na huku akipanga mipango yake ya baadaye, je huyo Dr angekufa mapema yeye akiwa amechukua hiyo mikopo kwani asingeishi?, Yeye alifanya nafasi yake kama mzazi Sasa kama huyo kijana hataki kazi Wala kujenga maisha yake na ameongea naye wakashindwa kuelewana amuache, na mwambie ukifanya wema huku unategemea malipo huwa hao unaowategemea wanaharibika ili upate fundisho.

Mtu kama huyo dada yako yupo tayari hata kuumiza watu wengine ili watoto wake wapate vitu vizuri na waje walimpe vitu vizuri ila angefanya kama wajibu wake huku akiwa rafiki na watoto au huyo mtoto hao watoto ndo wangebaki na hatia kukumbuka wema wa mama Yao, yeye hakupaswa kuweka mategemeo kwao na thamani yake ingeonekana tu.
 
Ndio madhara ya kusomesha mtoto ukitengemea akianiriwa upate sehemu ya mshahara wake,mm nilidhani mvuta bnghe mwizi mlevi mzizi kumbe kachagua njia nzuli sana ya mitume na manabii ifahamike kusoma sio lazima uajiriwe huyo mama hasimkatie tamaa amuuluze kazi anayo iweze amuwezeshe tu
Pepo zipo ktk chini ya nyayo za mama zenu
 
Wazungu walituweza, hasa ulimwengu wa tatu dini imenasa kwenye damu za watu. Unaacha utamadumi wako unafuata wa kizungu!!
Hakuna mzungu atakwambia huo upumbavu wa kumpigania Mungu ukakosana na wazazi na kuacha kazi uteseke mtaani. Dini za wazungu unazijua, dini ijenge shule na hospitali kisha ikusumbue kusoma na ukiajiriwa hospitalini ikushawishi uache?

Huo sio utamaduni wa kizungu haijalishi wana dini au hawana
 
Dini ya uislamu unamfunza muumini wake kumtii mola wake na mtume wake na kuwafanyia wema wazazi wawili (ikiwemo kuwatunza uzeeni kwao).
Dini ya uislamu inasisitiza wauminini wake kufanyakazi kwa bidii na kwa uadilifu.

Hapa nimeona tatizo lililoainishwa ni uvaaji wa kanzu kazini na kufuga ndevu. Huu sio ugaidi kwa mujibu wa uislamu au katiba ya nchi.
Hapa naona uelewa wa kijana kuheshimu mwongozo wa mavazi ya kitabibu ulikua mdogo, na kwa menejimenti ya hospitali huenda reaction yao kwa kijana ilikua kubwa na ya kumhukumu zaidi.
Huenda pia bada ya apo kijana akatengwa naye akaamua kuondoka jumla
na nafasi ya mzazi naye ikiwa laana na maneno makali ((kijana kaamua kupotea kabisa)).

Ni ushauri wangu kulingana mada jinsi ilivyowasilishwa.
 
Back
Top Bottom