Dada una sura nzurii.....

Dada una sura nzurii.....

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,801
Reaction score
43,177
images.jpeg
Kasie Mahaba.

Habari zenyuu,

Ndo naingia home hapa SA hooii,sasa nikiwa migration section pale airport iki nigongewe kuwa nimerudi nchini salama, nikamkabidhi passport yangu (aliyekuwa ananihudumia ni mdada).

Baada ya kuniuliza maswali kadhaa akaniambia niangalie camera, weka finger prints akagonga muhuri kwenye passport halafu akafungua ukurasa wenye taarifa zangu kuangalia mwaka wangu wa kuzaliwa na nilivyo..

Akanitazamaaa huku akiwa ameshikilia passport yangu kwa sekunde kadhaa. Aka tabasamu huku akisema.. Dada una sura nzuri. Sikutegemea usemi ule hasa kutoka kwa mdada. Nikajikuta natabasamu kuanzia pale nia nzima hadi home. Nikamwambia asante kisha nikachukua passport yangu huyo nikakamata Gautren hadi Sandton kisha nikachukua uber hadi home.

Njiani nikawa najiuliza..... kwani huyu dada kaniambia nina sura nzuri.....

Update:

Mara nyingi watu husema wadada ni ngumu sana kusifiana yaani huwa tunaoneana wivu. Lakini huyu dada kwa tabasamu alilotoa niliona alimaanisha kunisifia aidha kwa kulinganisha umri na sura akaona sura bado ina ahueni japo umri umeenda.

Najua wako ambao wanasifia kwa unafiki ile mtu anakwambia Umependeza wakati uko kama kituo. Kama kawaida yangu nilikuwa kawaida tuu sikuwa na makeup yoyote usoni zaidi ya lipstick na wanja. Huyu dada sifa yake haikuwa ya kinafiki tabasamu lake lilisema yote.

Kingine nikaona kuwa kweli wadada tunalewa sifa, wallah angekuwa mkaka ndo kanisifia ningempa namba yangu ya simu hehehehe.

Sio siri wadada tunasikia raha sana tukisifiwa hasa sifa ikiwa ya ukweli.... yaani hadi sasa kila nikiwaza natabasamu.

Kasie Kiuso hehehehehe.

Heeey, sijaweka huu uzi kujisifia bali nimeelezea kilichotokea. This pic below is real Kasie ..... nimeipiga lini jibu kwenye mabano hehehehhe

images.jpeg


Kasie Mahaba.
 
Kwani sio kweli?? Nimekalia seat ya mbele tu ngoja waje.
 
Kuna mada iliwahi kuletwa humu na mwanamke akidai amekitana na mwanamke mwenzie pahala fulani hawafahamiani wala nini lakini alimtamani ile mbaya ikafikia hatua ya kutamani angekuwa na uwezo wa kujiotesha ubor amdinye nao. Huenda nae huyo kakutamani Kasie matata toto la konyamwezi hahahaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom