Dada na mdogo wake,wagombania mwanaume

Dada na mdogo wake,wagombania mwanaume

Mkuu,mbavu sina,umenikumbusha mbali sana Mkuu wangu...Unakumbuka hadithi ya Nondo Mla watu,,,,Lindu amwokoa Kapilima.....,,,,Chilunda apambana na Chui?.....????

Dah! aisee hizi hadith zimenikumbusha mbali sana hadi nimejikuta natoka nje ya mada.Thanks mkuu,you made my day.
 
imekaa vibaya...siku ya siku mmoja kati ya hao wadada atachoka kushea ndo picha halisi litakapoanza
 
Hadithi inayokuja, ni ya Sungura sikia

Hadithi inayokuja, ni ya Sungura sikia,
Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia,
Njaa aliposikia, Sungura nakuambia

Siku ile akaenda, Porini kutembelea,
Akayaona matunda, mtini yameenea,
Sungura akayapenda, mtini akasogea,
Mtini akasogea, Sungura nakuambia.

Sungura karukaruka, lakini hakufikia,
Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,
Hakika alisumbuka, nguvuze zikapungua,
Nguvuze zikapungua Sungura nakuambia.

Mtazame hapo juu Sungura amelegea,
Mtazame na miguu, matunda anarukia,
Atafanya sikukuu, matunda akifikia,
Matunda akifikia, Sungura nakuambia.

Karuka tena karuka, matunda akarukia,
Mwisho wake akachoka, kachoka hata mkia,
Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
Pembeni akasogea, Sungura nakuambia.

“Sizitaki mbichi hizi” Sungura akagumia,
“Naona nafanya kazi, bila faida kujua”,
Yakamtoka machozi matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura nakuambia.

Sio kama hakutaka, sasa nakupasulia,
Matunda aliyataka, ndiyo kisa akalia
Tunajua hakufika, alichoka kurukia,
Alichoka kurukia, Sungura nakuambia.

Hadithi nimemaliza, nimekwisha simulia,
Jambo moja sikiliza, rafiki yangu sikta,
Usikose kujikaza, mazuri kukazania,
Utamshinda Sungura, utapata mbivu hizi

Darasa la 4 enzi hizo! Jamani umenikumbusha mbaaaali mno! Weka na picha yake basi
 
Back
Top Bottom