Dada huyu anaomba ushauri wenu tafadhali

si ukaolewe na baba wa huyo mtoto?

Naamni yeye ni mrefu ndo maana ulimkubalia na hadi kuamua kuzaa nae.........au naye pia alikuwa mfupi ndo maana mkamwagana nin.........

Ni hayo Tu!!...

The Magnificient
 
Urefu na ufupi kaumba MUNGU unene na wembamba jitihada zako na mume mwema hutoka kwa Mungu
 
N PM nije tuonane mi mrefu 6.1m tall. Ila hilo la mtoto kama unaye kweli plz don't PM.
 
wewe kweli mzabzab...lol...
mwambie ukweli tuu kuwa hapa umegonga mwamba....kwanza hao wafupi wakorofi balaaa.
another thing miezi miwili michache sana huyo atakuwa na lake jambo. mpotezee kabisa
 
mbona umejiita kiburudisho mpenzi?la pili ndoa ni zaidi ya urefu na ufupi mara nyingi watu tunapotaka kuolewa ama kuoa huwa tunaangalia mambo ya muda mfupi sana au vitu vya nje ukishaingia na kujifunza zaidi unagundua maisha ni zaidi ya uzuri wa nje ambao unaisha na kupotea baada ya muda.
snowhite love this!
 
Last edited by a moderator:
Nina umri wa miaka 28,mwaka huu mwezi wa nane nimehitimu diploma ya uuguzi ktk chuo fulani hapa nchini.Kitu kilichopelekea kuja hapa kuwaombeni ushauri ni juu ya ni mwanaume gani atakayenifaa juu ya suala zima la ndoa kwa maana imefika muda sasa ninahitaji kuwa ndani ya ndoa.Tatizo linakuja hivi mimi kiumbo ni mrefu hivyo moja ya sifa ambayo nilijiwekea ya mwanaume wa sifa zipi nitapendezwa nae atakayenioa ni awe mrefu kama mimi na sii mfupi hata tukitoka naona kama haitakuwa inapendezea.Sasa hivi karibuni kama mwezi mmoja uliopita nimekuwa nikiwasiliana kwa simu na mwanaume nisiyemfahamu hadi hapo alipojitambulisha kuwa aliniona kwenye mahafali yangu ya kuhitimu kwangu mwaka huu mwezi wa nane na aliyempa namba yangu ni mwanafunzi mwenzangu.Moja ya kitu alichonieleza ni kuwa alivutiwa/alipendezwa sana na mimi,na anahitaji sana kuwa kwa maana ya kuianzisha familia.Nilimjulisha kuwa kwa upande wangu nina mtoto mmoja wa miaka minne,aliniambia yeye ananipenda na anampenda pia mwanangu na kila anapopiga simu huniomba nimpe mtoto wasalimiane nae.Toka anapewa namba yangu hadi tunafanya mawasiliano sikuwa namfahamu au kuonana ana kwa ana yeye aliniambia yuko Songea hivyo aliniomba aje kunitembelea nilimkubalia,alikuja akafikia kwangu ila moja ya sifa ninazozihitaji hakuwa nazo yeye ni mfupi tukisimama naye ananifikia kwenye kifua.Sikutaka kuonyesha kuwa amekuwa kinyume na matarajio yangu nilimpa makaribisho vizuri ila hakulala kwangu alifikia hoteli.Kwa upande wake anasema anahitaji sana kuwa na mimi ndani ya ndoa ki umri yeye ana miaka 36.Kiukweli bado sijamwambia kuwa napenda kuolewa na mwanaume mrefu tunayelingana.Changamoto iliyo juu yangu nifanyeje ni ndani ya miezi miwili toka tumefahamiana ila yeye anahitaji kama ikiwezekana tuharakishe jambo hili ili niolewe naye.Naombeni mawazo yenu kwa kina ili nitakapofanya maamuzi yawe ya kweli na sahihi.

Simama hapo hapo subiri atakuja mrefu kama mnazi soon.........huyo aliyekupa mimba alikuwa mrefu au mfupi ?
 
ndio maana saa nyengine mapenzi ya kuanziana kwenye simu,huwa yana kasoro zake.unaweza ukapenda sauti na maneno yake.ila ukionana na mtu face to face unaweza kuwa disappoint.lakini kwa upande mwengine,ukipenda haijalishi kama mtu mfupi au mrefu.na mambo ya ndoa hayataki haraka.kwa nini na yeye aharakie hivyo.jaribu kwanza kuendelea kuzoeana nae.isije ikawa ana kasoro zake anaficha
 
Mh acha usubiri warefu waje, kama hujaja mtafuta miaka 4 ijayo na ukamkuta akiwa na mke by that time...wengi wametokewa na bahat kama zko na kudeka na kuzitafuta bdae kwa udi, tena ushazaa na jamaa kafumbia macho we bado unaomba ushauri hapa, endelea kuomba na kwingne

Hili nalo neno
 
mwambie ukweli tuu kuwa hapa umegonga mwamba....kwanza hao wafupi wakorofi balaaa.
another thing miezi miwili michache sana huyo atakuwa na lake jambo. mpotezee kabisa
Hapo umenikuna!
 
Nina umri wa miaka 28,mwaka huu mwezi wa nane nimehitimu diploma ya uuguzi ktk chuo fulani hapa nchini.Kitu kilichopelekea kuja hapa kuwaombeni ushauri ni juu ya ni mwanaume gani atakayenifaa juu ya suala zima la ndoa kwa maana imefika muda sasa ninahitaji kuwa ndani ya ndoa.Tatizo linakuja hivi mimi kiumbo ni mrefu hivyo moja ya sifa ambayo nilijiwekea ya mwanaume wa sifa zipi nitapendezwa nae atakayenioa ni awe mrefu kama mimi na sii mfupi hata tukitoka naona kama haitakuwa inapendezea.Sasa hivi karibuni kama mwezi mmoja uliopita nimekuwa nikiwasiliana kwa simu na mwanaume nisiyemfahamu hadi hapo alipojitambulisha kuwa aliniona kwenye mahafali yangu ya kuhitimu kwangu mwaka huu mwezi wa nane na aliyempa namba yangu ni mwanafunzi mwenzangu.Moja ya kitu alichonieleza ni kuwa alivutiwa/alipendezwa sana na mimi,na anahitaji sana kuwa kwa maana ya kuianzisha familia.Nilimjulisha kuwa kwa upande wangu nina mtoto mmoja wa miaka minne,aliniambia yeye ananipenda na anampenda pia mwanangu na kila anapopiga simu huniomba nimpe mtoto wasalimiane nae.Toka anapewa namba yangu hadi tunafanya mawasiliano sikuwa namfahamu au kuonana ana kwa ana yeye aliniambia yuko Songea hivyo aliniomba aje kunitembelea nilimkubalia,alikuja akafikia kwangu ila moja ya sifa ninazozihitaji hakuwa nazo yeye ni mfupi tukisimama naye ananifikia kwenye kifua.Sikutaka kuonyesha kuwa amekuwa kinyume na matarajio yangu nilimpa makaribisho vizuri ila hakulala kwangu alifikia hoteli.Kwa upande wake anasema anahitaji sana kuwa na mimi ndani ya ndoa ki umri yeye ana miaka 36.Kiukweli bado sijamwambia kuwa napenda kuolewa na mwanaume mrefu tunayelingana.Changamoto iliyo juu yangu nifanyeje ni ndani ya miezi miwili toka tumefahamiana ila yeye anahitaji kama ikiwezekana tuharakishe jambo hili ili niolewe naye.Naombeni mawazo yenu kwa kina ili nitakapofanya maamuzi yawe ya kweli na sahihi.

Ningependa kupata majibu kwa maswali yangu kabla sija toa maushauri yangu, moja, Je ulivyo muona ulipendezwa, ulivutiwa na kuhamisika nae japo kwa kipengele cha urefu? pili, je wewe mwanaume yeyote mrefu ni ewala kwako hakuna vigezo vyako vingine supplementary?
 
Maumbile syo chanzo cha kutompenda mwenzako mkubalie .

Miaka 28 ni umri tosha wa kuweza kupambanua ni maisha gani ya ndoa unahitaji ingawa nashangaa sana kwa thred ulioleta hapa jamvini kwani nahisi ndoa unaiangalia kwa upande mmoja tu. Kwanza huwezi kuchagua mume eti kwa kuhangalia mnapotoka nje watu wanawatazama namna gani mnapokuwa mnatembea n.k huo ni UPUUZI MKUBWA. Pia wewe ni mbinafsi kwani kwenye ndoa kila mmoja huwa ana vigezo vyake na mara nyingi ni ngumu sana kutimiza vigezo vyote kwa kila mmoja cha msingi hapa ni kuangalia vigezo vya muhimu hasa vile vinaweza kusaidia kujenga familia bora na hivi vya maumbile hasa ya nje mara nyingi mnatakiwa kucompromise. Unajiangalia kujiridhisha wewe binafsi huo ni UBINAFSI MKUBWA na nina wasiwasi na uwezo na utashi wako kwenye kujenga familia iliyo bora. Umesema una mtoto wa miaka minne na mwenzako amesema yupo tayari kumlea wewe unadhani yeye kwake hilo si tatizo? Naye hiyo uliyonayo ni dosari kwake tayari sema kwa kuwa si mbinafsi kama wewe na haangalii sababu ndogo kama hizo ndio maana ameamua kutaka mfunge ndoa pamoja na dosari yako. Cha mwisho nakushauri kwa tabia yako ya kuchagua wanaume kwa vigezo vya OVYO OVYO uangalie usije pewa mimba ya pili nayo ukaachwa kama ya kwanza.
 
Mambo ya kuolewa inabidi umwombe sana Mungu wewe dada. VIGEZO VYAKO HAVINA MAANA KABISA. Binafsi nimejionea ndugu zangu waliojifanya wazee wakuangalia sura wakati wa kuoa. Wote walikumbana na wanawake wenyemapepo. YAN HAPA NYUMBANI KUMEGEUKA NYUMBA YA IBADA SASA HIVI, NIMEJUA HADI KUKEMEA NA MM 7BU YA HAO WANAOCHAGU MAPEPO KUYAOA. mwishowe utasema awe mrefu na O kwenye kidevu. Urefu na ufupi sio kigezo.
 
Mawazo yako ndo sahihi wengine tutakuwa ni kuchagiza tu, so pima upepo mwenyewe bidada

  • :juggle:
 
kama urefu unaoa, kaa chini uungojee. . . 28 kwa mwanamke bado kidogo inafika jioni, usije ukasikilizia ndoa kwenye bomba. . .
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom