Dada huyu anaomba ushauri wenu tafadhali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dada huyu anaomba ushauri wenu tafadhali

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by KIBURUDISHO, Oct 11, 2012.

 1. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2012
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 953
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Nina umri wa miaka 28,mwaka huu mwezi wa nane nimehitimu diploma ya uuguzi ktk chuo fulani hapa nchini.Kitu kilichopelekea kuja hapa kuwaombeni ushauri ni juu ya ni mwanaume gani atakayenifaa juu ya suala zima la ndoa kwa maana imefika muda sasa ninahitaji kuwa ndani ya ndoa.Tatizo linakuja hivi mimi kiumbo ni mrefu hivyo moja ya sifa ambayo nilijiwekea ya mwanaume wa sifa zipi nitapendezwa nae atakayenioa ni awe mrefu kama mimi na sii mfupi hata tukitoka naona kama haitakuwa inapendezea.Sasa hivi karibuni kama mwezi mmoja uliopita nimekuwa nikiwasiliana kwa simu na mwanaume nisiyemfahamu hadi hapo alipojitambulisha kuwa aliniona kwenye mahafali yangu ya kuhitimu kwangu mwaka huu mwezi wa nane na aliyempa namba yangu ni mwanafunzi mwenzangu.Moja ya kitu alichonieleza ni kuwa alivutiwa/alipendezwa sana na mimi,na anahitaji sana kuwa kwa maana ya kuianzisha familia.Nilimjulisha kuwa kwa upande wangu nina mtoto mmoja wa miaka minne,aliniambia yeye ananipenda na anampenda pia mwanangu na kila anapopiga simu huniomba nimpe mtoto wasalimiane nae.Toka anapewa namba yangu hadi tunafanya mawasiliano sikuwa namfahamu au kuonana ana kwa ana yeye aliniambia yuko Songea hivyo aliniomba aje kunitembelea nilimkubalia,alikuja akafikia kwangu ila moja ya sifa ninazozihitaji hakuwa nazo yeye ni mfupi tukisimama naye ananifikia kwenye kifua.Sikutaka kuonyesha kuwa amekuwa kinyume na matarajio yangu nilimpa makaribisho vizuri ila hakulala kwangu alifikia hoteli.Kwa upande wake anasema anahitaji sana kuwa na mimi ndani ya ndoa ki umri yeye ana miaka 36.Kiukweli bado sijamwambia kuwa napenda kuolewa na mwanaume mrefu tunayelingana.Changamoto iliyo juu yangu nifanyeje ni ndani ya miezi miwili toka tumefahamiana ila yeye anahitaji kama ikiwezekana tuharakishe jambo hili ili niolewe naye.Naombeni mawazo yenu kwa kina ili nitakapofanya maamuzi yawe ya kweli na sahihi.
   
 2. kalou

  kalou JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2012
  Joined: Aug 22, 2009
  Messages: 4,357
  Likes Received: 972
  Trophy Points: 280
  Asiwe na haraka,miaka 28 sio mingi kihivyo.
   
 3. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  kama hana sifa unazozihitaji meleze ukweli usimpotezee muda
   
 4. V

  Von Mo JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 1,830
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  hana vigezo vyako, basi tena.....
   
 5. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  mh!MY DEAR
  Urefu na ufupi ni mambo ya nje sana ambayo kiukweli sidhani kama i moja ya vigezo vya kukufanya uwe na ndoa bora!
  ndoa ni kukamilishan wewe ni mrefu mkamilshe mwenzio kwa ufupi wake!
  kwanza huo urefu unauona nje tu akiwa ndani huyo boooonge la tolu!
  pili urefu wa mtu huanzia kiunoni kwenda juu chini wala poa tu!hebu jiachie mwanakwetu unless kama hujmpenda huyo kaka!
  hizo nyingine story lakini la msingi ni hili
  NDOA NI ZAIDI YA MAUMBILE YETU YA NJE!
   
 6. M

  Mtoto wa PWANI Member

  #6
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 10, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dada ndoa ni bahati, sasa chunga sana yawezaikawa hiyo ndio bahati yako kwasasa, unaweza ukapenda alafu we usipendwe!
   
 7. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,981
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  mwambie ukweli tuu kuwa hapa umegonga mwamba....kwanza hao wafupi wakorofi balaaa.
  another thing miezi miwili michache sana huyo atakuwa na lake jambo. mpotezee kabisa
   
 8. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,725
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 180
  "Mchagua nazi huambulia koroma". Pia kuwa makini usije ukaimbiwa ule wimbo....dada anaolewaaa, madunga embe yamebakiaa..
   
 9. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,275
  Likes Received: 22,030
  Trophy Points: 280
  Kama uko tayari kuvumilia kisirani cha watu wafupi, basi olewa naye
   
 10. N

  Nsuri JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 996
  Likes Received: 183
  Trophy Points: 60
  Mbona hata wanaume wafupi wanataka wanawake warefu? sasa itakuwaje kama na wanawake warefu hawataki wanaume wafupi?? Ukimkubalia halaf badae aje mwanaume mrefu itakuwaje?? mimi sidhani kama ni kigezo muhimu sana labda awe mfupi kupitiliza. Sifa za muhimu ni kama uaminifu, upendo na tabia
   
 11. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Naona mwanakwetu unatafuta mtu wa kukuangaulia embe mtini akiwa amesimama chini na siyo mme wa kutengeneza familia. All the best...
   
 12. ENZO

  ENZO JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,057
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  Vipi unahisi alivyo mfupi na nanihii yake itakua fupi??
   
 13. KIBURUDISHO

  KIBURUDISHO JF-Expert Member

  #13
  Oct 11, 2012
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 953
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Hapana ndugu si hivyo.
   
 14. KUN

  KUN JF-Expert Member

  #14
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nenda Rwanda, wapo wanaume warefu sana.
   
 15. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #15
  Oct 11, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  mbona umejiita kiburudisho mpenzi?la pili ndoa ni zaidi ya urefu na ufupi mara nyingi watu tunapotaka kuolewa ama kuoa huwa tunaangalia mambo ya muda mfupi sana au vitu vya nje ukishaingia na kujifunza zaidi unagundua maisha ni zaidi ya uzuri wa nje ambao unaisha na kupotea baada ya muda.
   
 16. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #16
  Oct 11, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  namshauri amchunguze kwa kama 2years huyo mtu asije mwaribia maisha wengine majini ati au katumwa usimwamini kila mtu ndufgu yangu!!!!!!!
   
 17. wiseboy

  wiseboy JF-Expert Member

  #17
  Oct 11, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,703
  Likes Received: 1,885
  Trophy Points: 280
  Mh acha usubiri warefu waje, kama hujaja mtafuta miaka 4 ijayo na ukamkuta akiwa na mke by that time...wengi wametokewa na bahat kama zko na kudeka na kuzitafuta bdae kwa udi, tena ushazaa na jamaa kafumbia macho we bado unaomba ushauri hapa, endelea kuomba na kwingne
   
 18. MASELE

  MASELE JF-Expert Member

  #18
  Oct 11, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 706
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  NDOA HAINA TBS, WENGI TULIKUWA NA TBS ILA TUKA ZI ABANDON, 28 HALAFU UNA MTOTO bado una aply MS (MS=MAN STANDARDS) SUBIRI UTAPATA AMBAYE ANAKUFUKIA KWENYE KIUNO.
   
 19. LEGE

  LEGE JF-Expert Member

  #19
  Oct 11, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 4,914
  Likes Received: 5,351
  Trophy Points: 280
  mhhh bado hujapenda wewe??? Ndio mana unapata nguvu ya kuzungumzia maumbile.
   
 20. Emma.

  Emma. JF-Expert Member

  #20
  Oct 11, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 19,923
  Likes Received: 3,001
  Trophy Points: 280
  Maumbile syo chanzo cha kutompenda mwenzako mkubalie .
   
Loading...