KIBURUDISHO
JF-Expert Member
- Mar 28, 2011
- 1,002
- 278
Nina umri wa miaka 28,mwaka huu mwezi wa nane nimehitimu diploma ya uuguzi ktk chuo fulani hapa nchini.Kitu kilichopelekea kuja hapa kuwaombeni ushauri ni juu ya ni mwanaume gani atakayenifaa juu ya suala zima la ndoa kwa maana imefika muda sasa ninahitaji kuwa ndani ya ndoa.Tatizo linakuja hivi mimi kiumbo ni mrefu hivyo moja ya sifa ambayo nilijiwekea ya mwanaume wa sifa zipi nitapendezwa nae atakayenioa ni awe mrefu kama mimi na sii mfupi hata tukitoka naona kama haitakuwa inapendezea.Sasa hivi karibuni kama mwezi mmoja uliopita nimekuwa nikiwasiliana kwa simu na mwanaume nisiyemfahamu hadi hapo alipojitambulisha kuwa aliniona kwenye mahafali yangu ya kuhitimu kwangu mwaka huu mwezi wa nane na aliyempa namba yangu ni mwanafunzi mwenzangu.Moja ya kitu alichonieleza ni kuwa alivutiwa/alipendezwa sana na mimi,na anahitaji sana kuwa kwa maana ya kuianzisha familia.Nilimjulisha kuwa kwa upande wangu nina mtoto mmoja wa miaka minne,aliniambia yeye ananipenda na anampenda pia mwanangu na kila anapopiga simu huniomba nimpe mtoto wasalimiane nae.Toka anapewa namba yangu hadi tunafanya mawasiliano sikuwa namfahamu au kuonana ana kwa ana yeye aliniambia yuko Songea hivyo aliniomba aje kunitembelea nilimkubalia,alikuja akafikia kwangu ila moja ya sifa ninazozihitaji hakuwa nazo yeye ni mfupi tukisimama naye ananifikia kwenye kifua.Sikutaka kuonyesha kuwa amekuwa kinyume na matarajio yangu nilimpa makaribisho vizuri ila hakulala kwangu alifikia hoteli.Kwa upande wake anasema anahitaji sana kuwa na mimi ndani ya ndoa ki umri yeye ana miaka 36.Kiukweli bado sijamwambia kuwa napenda kuolewa na mwanaume mrefu tunayelingana.Changamoto iliyo juu yangu nifanyeje ni ndani ya miezi miwili toka tumefahamiana ila yeye anahitaji kama ikiwezekana tuharakishe jambo hili ili niolewe naye.Naombeni mawazo yenu kwa kina ili nitakapofanya maamuzi yawe ya kweli na sahihi.