Daah! Noma sana...

Adimu

JF-Expert Member
Aug 22, 2013
655
284
Kuna siku nilikuwa maeneo ya mjini kati Arusha (city center), nikaipenda suruali moja ya Tsh 15,000/= na pesa sikuwa nayo ikabidi niende kutoa kwenye ATM ya Posta. Nimefika pale sikukuta mtu hivyo niliingia moja kwa moja. Nimefika mule ndani nikakuta pesa kibao zimemwagika pale kwenye kitundu cha kutolea pesa, ATM Card ilikuwepo pale imetokezea na pembeni kulikuwa na pochi ya kike iliyoonekana kutuna vilivyo.

Kwa uoga huku nikitetemeka mapigo ya moyo yakiwa yameongezeka nikatizama nyuma yangu sikuona mtu, nikachukua zile pesa haraka haraka, ATM na ile pochi. Ile natoka nje kuna dada mmoja alikuwa anakuja kwa kasi maeneo yale nikapata uoga. Nikamuuliza “Samahani dada, kuna kitu umesahau humu”, yule dada hakunijibu kitu kaingia kwenye chumba cha ATM akachomeka kadi kutoa hela mimi nikaondoka zangu fasta kuelekea home.

Nimefika home nikajifungia ndani na kuzibwaga zile pesa kitandani, nikafungua wallet nikakuta imejaa dollar, iPhone na ki-Nokia kidogo cha tochi, ATM Card 2 za benki tofauti ambazo zilikuwa zimezungushiwa karatasi iliyokuwa na namba za siri za ATM zote, moyo ukanilipuka paaaa!

Nikaona bora nipumzike kwanza kitandani!! Muda si mrefu ile iPhone ikaanza kuita, nilipoangalia halikutokea jina nikaona bora nipokee nimsikilize anasemaje, ilikuwa sauti ya kike iliyoongea kwa huzuni kwa kubembeleza huku akilia & alijitambulisha vizuri kuwa ile mali ni ya kwake.

Huruma ilinijia nikamwelekeza nilipo aje kuchukua. Hakuchukua muda akawa amefika nikamkabidhi vitu vyote akavihakiki na kukuta viko sawa. Dada kanishukuru na kunipa ile millioni 3 ya kibongo mi nikazikataa kwasababu ni mali yake na alizisahau tu.

Alinitoa hofu kwa kunisihi nichukue tu, mi kama binadamu mwenyezi Mungu atanilipa, nikakataa. Mwishowe akaomba namba yangu na kuondoka zake, akawa ameniacha ndani huku njaa. Sasa nikaanza kuisikia njaa vilivyo, nilikuwa na buku mbili nikaenda kula viepe vikavu na soda nikawa powa.

Sasa jana kanipigia simu kuwa anakuja nimsubiri, dakika tano tu akanipigia tena kuwa ameshafika yupo nje yupo ndani ya Prado mpyaa nikaingia tukaondoka. Akaenda kunionyesha kwake kisha tukaelekea kwenye nyumba nyingine iliyokuwa ndo imekamilika kujengwa akaniambia hii itakuwa yako akanikabidhi baadhi ya nyaraka na funguo zote sikuamini!!

Akanisindikiza kwangu, kufika home ananiambia hiyo gari (Prado) nayo ananiachia ni kwa mema tu niliyomfanyia, ndani ya ile gari kulikuwa na brief case iliyokuwa na pesa akaniambia pia hii pesa itakuwa yako ya kuanzia maisha, na kumbe yule dada alikuwa kanipenda akanikumbatia.

Kimoyomoyo nikasema umasikini baibai. Akiwa kanikumbatia akihema kwa kasi juu ya kifua changu. Mara nikahisi kubanwa na haja ndogo, nikakimbia fasta chooni na kuanza kukojoa, nasikia raaaha mkojo hauishi mara nikahisi mtu akinishika begani na kuniita kwa sauti.

“Anko, anko, anko; we ankoo amka unakojoa kitandaniii!!! Alikuwa mtoto wa sister ananiamsha. Kumbe ilikuwa ni ndoto tu mweeeh.

Somo: Hakuna mafanikio yanakuja kirahisi tu, tukomae mpaka kieleweke.
 
Ndoto za hivo unatamani hata ui-rewind ili iwe real....😁😁😁
 
Back
Top Bottom