Kiranja wa Kijiweni
JF-Expert Member
- Mar 9, 2023
- 588
- 1,053
Mh. Lema aliposema bodaboda siyo kazi watu walimdhihaki sana. Lakini kiukweli hii siyo kazi. Kwanza inatakiwa ibuniwe Kodi kubwa ambayo itazifanya bodaboda ziadimike barabarani. Nenda kwenye mahospitali yote makubwa na madogo idadi ya waathirika ni kubwa na wafanyakazi wa sekta ya afya ni wachache kuwahudumia waathirika.
Pia serikali yetu tukufu haioni jinsi uchumi wa nchi unavyoathirika na hizi ajali...
Hii inaogopesha aiseeWataisha sana wazee wa Nduthi
Hii picha niliiona toka jana kwenye baadhi ya Group,hakika nilidhani ni Editing tu,ila mmnh pikipiki inasimamaje hivyo kwenye Mbunga kama hiyo?Unaweza jiuliza kwenye 'lane' hiyo alifata nini ila unaweza kosa majibu ya haraka.
View attachment 2959875
Uko sahihi kabisaHii picha ni kama ime-setiwa kinamna, yaani ni kama tukio la kuigiza. Sijui lakini, pengine nimekosea.
Kwani gari za Rwanda huwa zinafuta mafuta wapi? Hapo ni TZ nadhani, angalia namba za pikipiki
Namba za pikipiki ni za kibiasharaKwahiyo hitimishi huyo ni bodaboda, hawezi kuwa mwendesha pikipiki wa kawaida? Mbona hapo chini kuna kabegi, labda alikuwa ni mwanachuo, au kijana mjasiriamali anakimbizana na muda!
Pikipiki ukisajili aina ya boxer, wanaichukulia ni ya biashara nadhaniNamba za pikipiki ni za kibiashara
Ni aibu nchi yenye hekari za mamilioni ya ardhi inayofaa kwa kilimo kuiacha na kusema bodaboda ni ajira. Bodaboda imefanya vijana waingie kwenye unywaji wa pombe kali na mihadarati mingine. Serikali ya mama Samia itafanya jambo jema kama ikitangaza kuwa bodaboda ni janga la kitaifa. Lakini sababu wananufaika kisiasa sidhani kama hilo litakaa lifikiwe. Bodaboda siyo kazi. Nasema na mimi ili mninangeSahihi mkuu, Serikali iwezeshe Vijana. Nguvu kazi kubwa la Taifa hili ni Vijana, Sasa vijana wakiwa tegemezi kwa wazee hiyo ni changamoto kubwa sana, vijana wanahitaji kuwa na Familia Bora, na kukiendeleza kizazi chao
Serikali yetu pendwa wekeni mazingira wezeshi ya Vijana kupata kazi Rasmi, na kuweka mazingira Rafiki pale kijana anapojiajiri haswa suala la Kodi kubwa za TRA.
Vijana wanapata msongo wa mawazo sababu ya Maisha Magumu. Vijana na sisi tuache Makundi, Starehe haswa pombe, wanawake. Ukiendekeza pombe, madawa ya kulevya na wanawake kutoboa ni ngumu sana.
Maisha yanahitaji nidhamu ya hali ya Juu, Eid imeisha, tuendelee kuijenga nchi yetu.
Kwa hizi akili za bangibangi lazima watu waishe.Wataisha sana wazee wa Nduthi
Hata mimi naona hivoHii picha ni kama ime-setiwa kinamna, yaani ni kama tukio la kuigiza. Sijui lakini, pengine nimekosea.
Ukiwa ni mtu wa barabarani huwezi sema haya maneno.Mhh hii picha ya mchongo ukiangalia vizuri. Kwanza hakuna hata damu wala nyama nyama zimetapakaa, pili hakuna hata mashuhuda pembeni wakishangaa, tatu mtu kanasaje hapo maana analingana na gari unene.
Pkpk ina namba za tanzania.Left hand hiyo ya Rwanda. Daaah Pole sana, Maisha haya Jamani.
Sahihi mkuu, hilo Lori la Mount Meru lina Plate No. Ya Rwanda, ambapo magari yao ni Left Hand.Pkpk ina namba za tanzania.
Hiyo picha ni ya kweli na huyo sio boda bali ni mwalimu mmoja wa shule ya msingi huko Tabora. Amezikwa last week huko Same KilimanjaroMhh hii picha ya mchongo ukiangalia vizuri. Kwanza hakuna hata damu wala nyama nyama zimetapakaa, pili hakuna hata mashuhuda pembeni wakishangaa, tatu mtu kanasaje hapo maana analingana na gari unene.