Cyrus Vance hakufanya ajizi kama Magufuli

Cyrus Vance hakufanya ajizi kama Magufuli

ebaeban

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Posts
2,205
Reaction score
2,707
CYRUS VANCE HAKUFANYA AJIZI KAMA MAGUFULI

Wana body poleni na shughuri za mchana , uzi huu unazungumzia sakata la Waziri mkuu Mizengo Pinda na waziri wa ujenzi Bwana John Pombe Magufuri walivyotunishiana misuri, sakata hili linafanana na wakati ule miaaka ya 1977 wakati huo Rais wa Marekani alikuwa ni Bwana Jimmy Carter na waziri wake wa mambo ya ichi za inje alikuwa ni Bwana Cyrus Roberts Vance.Ilikuwa hivi kiongozi wa Iran alikuwa ni yule dicteta maarufu SHAH wa Iran,miaka hiyo hiyo ya 1977 huyu jama mambo yalikuwa magumu sana kwake Iran , maandamano yalikuwa kila siku kumpinga akatumia askari ikashindikana ikabidi akimbie inchi kwenda ugeninii ( ndio maana watawala maandamano hawayapendi), inchi ya kwanza ilikoenda ilikuwa ni visiwa vya Balmurda.

Huyu jamaa alikuwa ana fedha nyingi sana kaziweka kwa Mabank ya Marekani yapata dolleri billion 15 enzi hizo. Baada ya kukimbia inchini kwake wakataka zile pesa alizokwiba zirudi unajua walifanyaje waliwateka balozi wa Marekani inchni Iran na maafisa wake wote wapatao hamsini , waliwakamata mateka wakadai hawatawaachia mpaka pesa alizoiba SHAH na kuziweka kwenye Mabank ya Marekani zirejeshwe Iran kupitia bank za Argeria.

Baada ya kadhia hilo Marekani nao wakataka wafanye mission kama ile ya Israel ya kuwaokoa mateka wao walioshikiliwa Entebbe, wakaamua kustage military rescue operation ambayo waliita Operation Eagle CLAW, Rais Jimmy Carter na washauri wake wa kijeshi waliamua kufanya hii Operation ya kijeshi lakini waziri wake wa mambo ya inchi za inje Bwana Cyrus VANCE hakukubali kabisa kwa sababu hakuona uwezekano wowote wa kufanikiwa ni kama walimkubalia vile lakini wakamzunguka wakaendelea na zoezi, siku ya siku zoezi halikufanikiwa walifeli kabisa totally na kwa aibu na helikopta zao zingine ziligongana hewani, basi ikawa aibu kweli kwa utawala wa Jimmy Carter, kwa kuwa waziri wa mambo ya inchi za inje alizungukwa na yeye ikawa ni sehemu ya ile aibu basi waziri huyo alijihudhuru haraka sana, Rais akamteuwa jamaa mmoja aitwae Edmund Muskie kumaliza ngwe iliyobaki na mbaya kuliko zote walirudisha pesa za SHAH ikawa aibu ingine tena.

Sasa baada ya Magufuri kuwa amri yake ya tozo ya 5% ya uzito kuzidi malori na baada ya kuwa kakazia amri kwa msisititizo mkubwa sana wa kutoa povu mdomoni na kisha Waziri mkuu wake kuitengua amri hiyo kirahisi sana ilifaa kabisa kujihudhuru kulinda heshima yake kama alivyofanya Cyrus VANCE, Magufuri anangoja nini kujihudhuru maana wenye malori wakina Zakaria ni wazi watamzarau yaani Ph.D holder mzima anajua mambo ya integrity yako kuwa questioned maana yake nini, ya nini kuendelea na kazi, hebu mlioko karibu nae mmueleze ni aibu hata waseme uroho wa madaraka this is too much.

Ebaeban
Tel.Aviv.
 
Umeshawahi kumsikia kwenye hotuba zake anavyojipendekeza kwa raisi? Hawezi kujiuzulu hela za makarandasi wa kichina tamu hela ya kugombea ubunge atapata wapi. Kugombea ubunge ni gharama sana. Tisheti, kofia, kanga, mabango, makarasi yenye picha, posho kwa wapambe, vipesa vya kuhonga, etc etc. Hivyo vyote ni gharama ambazo wabunge waliobahatisha kupata uwaziri wanazipiga kwenye wizara walizopewa kuziongoza.
 
neno "KUJIUZULU" halipo kwenye kamusi au hata dictionary ya mwanasiasa yeyote wa tanzania anayetoka hicho chama cha kina PINDA NA MAGUFULI NA JK NA LOWASA.
 
Ushauri kwamba Magufuli ajiuzulu ni mzuri lakini kwa hali ya kawaida sio utamaduni wa Kitanzania kujiuzulu.Iwavyo iwe bado Magufuli ataendelea kujipendekeza hata kwa huyo aliyemwonyesha namna serikali inavyoendeshwa.Magufuli kama wapenda sifa wengine Serikalini ni tatizo.Badala ya kuleta suluhisho la matatizo wao huyakuza!Sijawahi kusifu utendaji wake kwani hata JMK alishawahi kumwonya aache ubabe lakini si mtu mwelewa huyu.
 
neno "KUJIUZULU" halipo kwenye kamusi au hata dictionary ya mwanasiasa yeyote wa tanzania anayetoka hicho chama cha kina PINDA NA MAGUFULI NA JK NA LOWASA.

Nani CDM aliwaikujiuzuru-Lowasa mbona kajiuzuru,kujiuzuru sio lazima uwe na madaraka makubwa,hata nafasi ndogo Uwajibikaji unatakiwa
 
nani cdm aliwaikujiuzuru-lowasa mbona kajiuzuru,kujiuzuru sio lazima uwe na madaraka makubwa,hata nafasi ndogo uwajibikaji unatakiwa

lowasa kajiuzuru "kuogopa" kufukuzwa kama paka mwizi...angekomaa aone nini kingetokea...cdm nani ajiuzulu na kwa kipi cha ajabu au cha kudhalilishwa kama alivyodhalilishwa makufuli.....acha ubishi na ushabiki wako wa ma-ccm.
 
Back
Top Bottom