Hii sheria itakosa mashiko..so itakosa uhalali wa kisheria wa kuwatuhumu na kuwatia hatiani washtakiwa
Nilishapata kusema humu ndani siku moja kuwa ili kosa lidhihirike kuwa ni kosa ni lazima basi pawepo na uhusiano kati ya "Mens rea" na "Actus reus"...hayo ni maneno ya kilatini...
Mens rea ni akili, mawazo, fikra zinazokushawishi kutenda kosa.. guilty mind...criminal mind...criminal desire. ..criminal feelings...
Actus reus..physical action to criminal acts...ambapo ili kosa lidhihirike kuwa ni kosa ni lazima basi ithibitike kuwa..kuna uhusiano kati ya mens rea. Na actus reus. ..
Sasa ktk sheria hii ya mitandao kuna ibara inasema kuwa..mtu yoyote atakaefungua ujumbe ambao sheria imeufanya kuwa ni jinai....basi..mfungua ujumbe atakuwa ametenda kosa..
Kwa mfano mimi nimepost ujumbe humu ndani ya group ambao sheria imeufanya kuwa ni jinai...na wewe..ukaufungua....hakutakua na kosa...simply because hukujua nilichopost...so kukakosekana mens rea. ..