GE2025 CWT yakanusha uzushi wa walimu kutoshiriki uchaguzi

GE2025 CWT yakanusha uzushi wa walimu kutoshiriki uchaguzi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) kimekanusha vikali taarifa zinazosambazwa kwenye baadhi ya mitandao nchini na baadhi ya vyombo vya habari zikihamasisha waalimu kutoshiriki kwenye uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 kwa maelekezo kuwa ni msimamo wa chama hicho Taifa

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa CWT Mwalimu Joseph Misalaba leo Jumapili Oktoba 26, 2025 kwenda kwa Makatibu wa Mikoa imetoa rai pia kwa waalimu na wanachama wa CWT kupuuza taarifa hizo kwani hazina ukweli wowote na zinalenga kuzua taharuki, uzushi na uchonganishi ambao unapaswa kupingwa ili kuendelea kulinda umoja, amani na utulivu ambao ni tunu ya Tanzania

“CWT pia inawahakikishia waalimu, serikali na wananchi wote kuwa tutaendelea kushirikiana na mamlaka husika kuhakikisha kuwa tabia hii ya utoaji taarifa potofu inakomeshwa ili kulinda misingi na madhumuni ya uwepo wa vyama vya wafanyakazi kwa mujibu wa sheria.” Amesema Mwalimu Misalaba katika taarifa yake kwa umma.

CWT pia imewataka waalimu wote nchini kuendelea na msimamo wao wa kujitokeza kwa wingi Oktoba 29, 2025 kwenda kupiga kura kwani ndiyo msimamo wa Chama hicho ambao ulishatolewa na Msemaji wa CWT ambaye ni Rais wa Chama hicho


 
Toka lini walimu wakawa na akili
Ningeshangaa walimu jamii ya walimu walio wapumbavu wangetoa andika makini kama lile
 
Back
Top Bottom