CWT Mmethubutu kugoma, Mmeshindwa kesi na Hamsongi mbele katika Mgomo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CWT Mmethubutu kugoma, Mmeshindwa kesi na Hamsongi mbele katika Mgomo!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Emashilla, Aug 3, 2012.

 1. Emashilla

  Emashilla Senior Member

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MIGOMO KISHA MAHAKAMA ZIKASEMA NI BATILI BADO KUAHIRISHA HAKI SIO SULUHISHO LA MADAI YA WANYONGE

  Hatuwezi kuwalipa Madaktari iweje tuwalipe hawa wana wa wito kama hawataki tunazowapa wanaweza kufanya wanalotaka au tuwafukuze katika zoezi la sensa. Lakini tunawajali na kuwapenda walimu na madaktari. Hivi walimu wanadai mazingira magumu wana mazingira magumu yapi? tuisheni tayari tumepiga marufuku, Sensa tumewapa wao, uchaguzi mdogo na mkubwa bado huwa wanapewa jamani walimu mnataka posho gani hii ya mazingira magumu? Bima ya afya mnapata ingawa mtachangia kidogp kununua dawa kwa marafiki zenu madokta waliogoma kama ninyi lakini tuliwashinda na sasa huduma zinaendelea vizuri na ninyi walimu tumewashinda kwa kishindo kama sera zetu za kishindo rudini shuleni mkawalipe wanafunzi kwa utoro wenu kwa mgomo batili.
  Kweli mimi ninawashangaa Viongozi wa chama cha walimu Tanzania-CWT! Nilitaka kuwaunga mkono, lakini nimepata wazo jipya. Walimu mnapata shikamoo na Good morning Sir/Madam nyingi sana kuliko mtu yeyote kwa siku. Bado hamridhiki tu? Mikopo katika mabenki kwa riba kubwa inawahusu. Mnadai nyongeza ya mishahara na maposho hivi mnataka nini tena jamani? au niwatume huko wauzaji wa bidhaa ili wawakopeshe; niwakate kwenye hizo fedha zenu za kila mwezi?
  Lakini kwa nini jamani walimu wangu! Vumilieni. Wenzenu huku gharama za maisha ni kubwa mno. Sasa tunataka gari zuri na posho ya shilingi 200,000/= kwa masaa machahe tu kila siku. Sisi tukigoma sijui nani atawatungia sheria za kuzuia migomo? Kumbukeni hata maneno ya Mungu yanasema aliyenacho ndiye ataongezewa, lakini asiyenacho atanyang'anywa hicho kidogo alichonacho. Walimu wangu Malipo yenu ni WITO na KUWAJALI WANAFUNZI. Watu mpendwao ndio mtakaoendelea kulipwa kidogo. Mgomo huu kama vile umefika mwisho! Je! mazoezi haya ya Mgomo yatafuatiwa na ule wa TUCTA au Wahadhiri au wanavyuo kudai mikopo toka bodi ya mikopo ya elimu ya juu?

  Mwalimu Pole! Nilikuona ukilia baada ya hukumu ya mahakama divisheni ya kazi.Machozi yako si bure.

  Mungu yupo Upande wenu Walimu wa Tanzania.
   
 2. G

  Godwishes JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 577
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Viumbe hai,wana sifa ya ukuaji hyo ni concept ya Biolojia.Bt wanaweza kukua kwenda juu yaani Growing up or kukua kwenda chini yaani Growing down. Kwa hoja yako hapo juu Mkuu,gro***dauni.Unauma au Unapuliza?Mind yu,Mwl.ni chanzo cha uanasheria wako,kumbe ana haki ya kuwa na mshahara mkubwa kuliko prof.nyngne.Let us wait and see the outcomes.Tuombe uzima utatoa ushuhuda one day.
   
 3. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Msome tena Emashila utamwelewa, ameuma na hajapuliza popote...
   
 4. Mhadzabe

  Mhadzabe JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 1,657
  Likes Received: 717
  Trophy Points: 280
  Hujamwelewa mwanzisha uzi! Read btn lines you will note something hidden!
   
Loading...