CWT kwawaka Moto Arusha yatoa tamko

CWT kwawaka Moto Arusha yatoa tamko

Waziri2025

Senior Member
Joined
Sep 2, 2019
Posts
149
Reaction score
380
Kufuatia kusambaa mitandaoni kwa taarifa juu ya ubadhilifu wa mamilioni ya fedha za Chama Cha walimu Tanzania CWT zilizotolewa na aliyekuwa mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Dodoma , Mwl.Clement Mahemba ,chama hicho mkoa wa Arusha kimetoa tamko la kulaani taarifa hizo kikidai ni upotoshwaji.

Akiongea baada ya waandishi wa habari kufika ofisini kwake,mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Arusha ,Lotta Laizer alisema kuwa hatua ya aliyekuwa mwenyekiti wa CWT mkoa wa Dodoma ,kujirekodi na kusambaza taarifa zinazokichafua chama na viongozi wake ni ukiukwaji wa katiba ya chama hicho na utovu wa nidhamu.

Alisema kuwa Mahemba alifukuzwa nafasi yake ndani ya chama hicho Mkoa wa Dodoma,June ,2021lakini amekuwa akiendesha propaganda za kupotosha na kuleta taharuki ndani ya chama.

Mwenyekiti huyo alimshauri Mahemba kutumia busara kwa kufuata kanuni na katiba ya chama hicho kwa kukata rufaa ngazi husika iwapo hakuridhika na maamuzi ya kuenguliwa nafasi yake yaliyotolewa na Baraza la CWT Mkoa wa Dodoma.

Lotta alisema kuwa video aliyojirekodi Mahemba inawahusisha viongozi wawili wa ngazi za juu wa CWT Taifa ambao ni Katibu mkuu,Deus Seilf na Mweka hazina , Abubakar Alawi ambao Hata hivyo tayari wamefikishwa mahakamani kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka suala ambalo Mahemba hakupaswa kuingilia jambo lililopo mahakamani .

"Ikiwa Mahemba ataona ameonewa asitengeneze taharuki nchi nzima au kujificha kwenye kivuli cha dini,lakini afuate kanuni na katiba ya chama cha walimu kwa kukata rufaa kwenye chombo husika ,hatua ya kuchafua chama na viongozi ni utovu wa nidhamu najua amepata mkwamo baada ya kuvuliwa nafasi yake na Baraza la CWT Mkoa pia nawasihi ndugu na jamaa zake waone namna ya kumsaidia matibabu ya kisaikolojia kutokana na mkwamo alioupata "alisema Lotta.

Katika clip ya Mahemba anaeleza jinsi alivyoenguliwa wadhifa wake kimizengwe na Baraza la CWT Mkoa wa Dodoma akidai Baraza hilo halina mamlaka kwa mujibu wa katiba yao, kwani chombo pekee chenye uwezo wa kumwondoa madarakani kiongozi wa ngazi yoyoye ni Mkutano mkuu wa CWT.

Mahemba ameitaka Serikali kuingilia Kati suala la Katibu wa CWT ,Seif Deus na Mweka hazina Abubakar Alawi kuendelea kubakia madarakani wakati wamefikishwa mahakamani kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka na usababisha upotevu wa mamilioni ya fedha mali ya chama hicho Jambo ambalo wanaweza kuharibu ushahidi.

Mahemba anadai kwamba mara baada ya viongozi hao kufikishwa Mahakamani Mei 3 Mwaka huu na kusomewa mashitaka, walipata dhamana na kurejea katika majukumu yao lakini wamekuwa wakisaka mchawi aliyepeleka taarifa za ubadhilifu Takukuru .

"Kwa mujibu wa sheria za utumishi mtumishi wa umma ukishashtakiwa mahakamani unasimama kazi ,Sasa huyu Self Deus anaendeleankung'ang'ania ofisi anatumia Rushwa kuhonga ili abakie madarakani aliwahi kufungia ofisini wafanyakazi wote na kukagua laptop zao akitaka kujua nani amepeleka taarifa Takukuru"ilisema taarifa ya Mahemba

Akiongea kwa njia ya simu Mahemba alisema kimsingi hana ugomvi binafsi na viongozi hao ila anacholalamikia ni hatua yao kuendesha mtandao ndani ya chama hicho na kuwavua madarakani baadhi ya viongozi akiwemo yeye baada ya kuwahisi ndio waliopeleka taarifa Takukuru.

Alisema kuwa amejipanga kufungua kesi mahakamani kulalamikia ukiukwaji aliodai umefanywa na Baraza hilo la chama cha walimu Dodoma, kumvua madaraka wakati linajua halina Mamlaka ya kufanya hivyo.

Ends..

IMG-20210721-WA0002.jpg
 
Nimekuja mbio nikajua wanataka kulianzisha waongezwe Mishahara kumbe ni ujinga, haya ndo wanayo weza, waambie wapiganie masilahi ya walimu hutawaona
 
CWT wanapiga dili wakati hali za walimu wengine ni mbaya, jamaa hawana huruma kabisa.
 
CWT NI UOZO MTUPU USITETEE UJINGA CHAMA CHA WEZI TU HICHO KILA MTU ANAJUA HUYO MWALIM MLIEMHUJUMU NDIO ANASEMA KWELI SIJUI HATA WEWE HUU UJASIRI WA KUTETEA UPUMBAVU UMEUTOA WAPI TENA UNATOKEA MKOA WA WATU WENYE AKILI TIMAMU TOKA HUKO UNATUDHALILISHA TU.
 
Walimu Walimu Tuna Hali Ngumu Sana 😏🙄🙄😶
Wagosi Wa Kaya Wana Song Lao
 
YANI HUYU BWEGE ANAEWATETEA WEZI NDIO TAKUKURU WANATAKIWA WAANZE NAE YANI WALIMU WANA HALI MBAYA NA WACHACHE WANAFAIDIKA HALAFU ANAJITOKEZA MOUMBAVU MMOJA ANAETUMIWA NA WEZI KUTETEA UJINGA. HIVI WALIMU WA MKOA WA MNA AKILI KWELI KUONGOZWA NA HUYO MPUMBAVU. KWANZA WALIMU MMEMTUMA AWASEMEE?
 
Kwanza rudisheni asilimia za matawi mmezikalia kwa kudai mutatoa mafunzo kwa wawakilishi lakini hamna kitu wezi nyinyi
 
Hawa waalimu na chama chao cha CWT ni 'kama' sehemu ya Jumuiya ya chama cha Mapinduzi CCM kama UVCCM, WAZAZI , UWT kwa matendo yao ya kushirikiana na chama tawala kwa karibu sana, hivyo watamalizana wenyewe kama Jumuiya ya CCM.
 
Back
Top Bottom