CVT gear box problem

new generation

JF-Expert Member
Mar 14, 2012
814
1,629
Wadau nahitaji kupata msaada wa fundi mzuri wa CVT gear box..nipo dsm, kigamboni, namba yangu (0719058458) nina vitz new modal yenye injini 2SZ-FE, yenye CVT gear box, ( gear selector ina P, R, N, D, B) sasa hii gari nimepatwa na tabu kwenye transmission system, na limeanza baada ya kubadili transmission fluid.

Gari inatumia transmission fluid aina ya CVT-TC, wakat wa kufanya service nilikuta fundi kaisha fanya kazi kamaliza nkaja kulichukua na kuondoka, nimetembea km 1600 nkaanza kuona gafla gari inakua inishiwa nguvu, unashangaa injini inaunguluma kwa nguvu ila mwendo mdogo na gia zinashndwa kupanda kwenda 3, mpaka 4, au inaishia gia numba 1, ila ukiweka reverse gari inarudi nyuma poa, ila mbele majanga.

Katika kutafuta tatizo, nkagundua fundi aliweka ATF transmission fluid badala ya CVT-TC, ndo nkabidi ni flush oil yote ya gia box.. Fungua sampl, toa filter pamoja na chesi, vyote vikasafishwa. Ila baada ya kuflush nkaweka fluid original ya gari (cvt-tc) but maajabu bado gari imeendelea na ugonjwa uleule wa kushindwa kushift gear smoothly and with power. Wadau kuna anaweza nipa way foward?

Nitafutahi kupata solution.
 
Mkuu new generation, nafikiri tatizo lako sio kubwa. CVT gear (actually ni pulley) settings zinafanywa na your on-board computer. Nafikiri kati ya fundi wa mwanzo na ulipobadilisha wewe transmission fluid hizi settings zilijifuta.

Computer settings zikifutika gari linaingia kwenye safe-mode, au saa nyingine huitwa limp-mode. Gari likiwa kwenye hii safe-mode basi gear za kwenda mbele zinabakia kwenye low gears tu.

Unachopaswa kufanya ni kuzirudisha hizi settings to factory levels. Nenda kwenye mannual yako au mtandaoni uangalie wanasemaje kuhusu "CVT Transmission Settings" kwa gari lako.

Good luck.
 
Mkuu new generation, nafikiri tatizo lako sio kubwa. CVT gear (actually ni pulley) settings zinafanywa na your on-board computer. Nafikiri kati ya fundi wa mwanzo na ulipobadilisha wewe transmission fluid hizi settings zilijifuta...
Naomba kujua, gari ikiwa kwenye safe mode kuna warning light yoyote huonekana kwenye dashboard?? Maana hapa gari haina warning light yoyote, na nimeipeleka kwenye mashine sikuona fault code yoyote.. Nkatoa waya wa betri kureset still changamoto ipo palepale mkuu..
 
Actually, inategemea na aina ya gari kama kutakuwa na warning light au hapana. Magari mengi yenye electronic transmission control, ukiondoa power, kama ku-disconnect betri kwa muda mrefu, basi hizo control codes zinajifuta kwenye compyuta ya gari na inabidi uziset tena.

Mimi nina Audi ya miaka ya karibuni ilioniletea tatizo kama lako kwa ajili ya kutoa betri kwa muda mrefu. Rafiki wa karibu ndie alienitonya na nikaweza kuziseti transmission settings upya mwenyewe.

Unaweza ukataka kumtumia fundi mwenye uzoefu, kama anavyojaribu kukutafutia mkuu Mshana Jr.
 
Siku hizi nahoji kila kitu ambacho fundi anasema, baada ya kupata shida kama yako. Na service haifanyiki bila ya mimi kuwepo.

Gari yangu pia ni CVT. Baada ya fundi kuona rangi ya gear box oil ni nyeupe, akadai inatakiwa iwe na rangi nyekundu na sio nyeupe. Akashauri tumwage transmission fluid iliyopo na tuweke nyekundu. Hili lilikuwa kosa kubwa.

Baada ya kama wiki mbili, nikamhoji fundi mwingine kuhusu kilichofanyika, na ndipo akanieleza lazima tuflush transmission oil iliyowekwa na kuweka ya CVT, otherwise muda si mrefu gear box itafeli.

Nilienda mbele zaidi na kumtafuta fundi wa dealer wa hayo magari hapa nchini. Nilinunua kopo kama nne za CVT. Baada ya kuflush mara ya kwanza na ya pili, nilibadili transmission oil tena kila baada ya mwezi kwa miezi miwili.

USHAURI:
Nenda Toyota, ongea na mlinzi pale getini, mwambie unaomba kuonana na fundi mzuri kuliko wote. Ni bora ukaenda muda wa lunch ili baada ya kuelekezwa, uongee naye.

Mafundi wa mle ndani Totota ni wazuri ila bei zao huwa ni kubwa na mara nyingi wanafanya kazi za nje weekend.
 
Pole kw janga,
Ulivosema kw maelezo yako pale mwanzo, tatizo lilisababishwa na mafuta yasiofaa, ATF kabla ya CVTF! ILA, mlipo kua mkibadilisha kuweka yaliofaa, mlisahau kua kuna mafuta mengi yaliobaki mle ndani kwa torque converter na pia cooler pale kwa radiator. Haya ndio yanayosumbua sasa, the best way woulda been to flush through- yaani kujaza mafuta na kungurumisha engine na kuyamwaga mafuta kutoka kwa return pipe!!!
 
Nilipodadisi sana kwenye internet, nikakuta huu ushauri wako.

Lakini nilivyomweleza fundi kuhusu kuflush kwa njia hiyo, alikataa. Akasema tutauwa transmission.

Ikabidi tufanye manual. Very costly.
 
Nilipodadisi sana kwenye internet, nikakuta huu ushauri wako.

Lakini nilivyomweleza fundi kuhusu kuflush kwa njia hiyo, alikataa. Akasema tutauwa transmission.

Ikabidi tufanye manual. Very costly.
Bro, asante kw kuunga mkono. Nimekua nikikabiliana na watu wa mawazo hayo hayo ya huyo 'fundi', wawe wateja na ushauri waliopewa(potoshwa) au pia mafundi wenzangu wasiojiongeza au kuelewa issue kabla ya kuishtumu.

Niliweza kuijaribu hiyo mbinu kw Nissan Note, pia CVT ikawekwa ATF, na gari likawa safi kabisa. Kwa magari ya Mercedes yasiokua na drain cork kw T/C, hii ndiyo mbinu tunayotumia katika Drain-Flush-Fill procedure. VERY EFFECTIVE!!
 
Cvt fluid inashauliwa kubadilishwa baada ya mda gan au km ngap
Kwa uhakika itategemea na transmission yenyewe, mazingira ya matumizi na uendeshaji. Ila kwa matumizi ya kawaida - mwendo taratibu, umbali wastani na dereva makini, km 50000 ni makadirio mazuri.
KWA UHAKIKA TIZAMA OWNERS MANUAL YA GARI!
 
Ni ist new model
 
Mkuu naomba uni pm namba yako nahitaji kuongea nawe kwa guidance zaid, maana gari mara ina engage gia zote mara hazibadiliki... Gari inakwenda kwa gia namba 1&2 pamoja na reverse.. Ingawa nazo hazina nguvu kama inavotakiwa... Na uki-shift ear lever kwenda D kuto N gari inashtuka kama mara mbili (ths is unusual). Sijajua kama inaweza tengenezeka na garama yake kuitegeneza, na baada ya kuitengeneza inaweza kua reliable? Maana gia box wanauza bei juu (700, 000-800, 000) sasa kwa usawa huu dah..
 
Cvt fluid inashauliwa kubadilishwa baada ya mda gan au km ngap
Na fluid yenyewe ni CVT-TC
IMG-20171019-WA0009.jpeg
 
Hili tatizo lilinifanya nikatumia hela nyingi sana bila mafanikio,hatimae nikanunua gearbox nyingine,
Unapo engage gear inakuwa kama inataka kuruka,inashtuka kumbe ndani clutch zote zilikuwa zimeungua kasoro rivasi tu,niliingia hasara za kununua cvt oil mara 3 ili kuisafisha bila mafanikio, hapo na fundi lazima akununulishe pump mpaka nikajilaumu kwa nini nisingefanya uamuzi wa kununua gearbox nyingine,
Hivyo basi kwa ushauri wangu ni bora ununue gearbox kupunguza hasara mkuu
 
Wadau, sikupata solution ya kutengeneza gia box hyo, so Nilibidi kununua nyingine nkaweka and the problem was solved. It run properly by this time ingawa fundi alie nitia hasara hii nimemuweka lock-up kidogo akili ikamkae sawa.
IMG_20171104_152157.jpeg
 
Back
Top Bottom