CV ya Naibu Waziri wa Elimu Philip Mulugo: Je inatosheleza kusimamia majukumu aliyopewa?

Status
Not open for further replies.
Jamani hebu nisaidieni.Huyu Mheshimiwa nasikia mara nyingi akijiita au akiitwa mwalimu, kwa usomi upi wa elimu ya ualimu? KaCV kake hakaoneshi alisomea elimu ya ualimu wapi au ni muendelezo wa "slip of the pen/hand" kwenye kaCV haka kama ilivyokuwa kwenye "slip of the tongue" kule kwa Mzee Madiba juzi? Kwa stahili hii unategemea kipya huko Wizarani au/na kwenye mfumo wa elimu yetu kweli?
 
Wadau naomba tuiangalie CV ya huyu Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi tuone kama ina kidhi majukumu mazito :

First Name: Philipo
Middle Name: Augustino
Last Name: Mulugo
Member Type: Constituency Member
Constituent: Songwe


EDUCATION

Open University of Tanzania BA (Economics Education ) 2002 2008 GRADUATE
CERTIFICATIONS

Degree miaka 6

Ya medicine hiyo
 
Hapa mie sijaona tatizo. Mi nilijua labda ana certificate kama ya Makamba. Elimu yake ni nzuri na inatosha. Pia CV yake nzuri tofauti na Masele ambaye hana uzoefu wowote wa uongozi lakini mkuu kampa unaibu waziri wa madini
Tanzania is formed in one nineteen sixty four. Du kweli kihiyo hata kutaja tarakimu hajui hao wanafunzi alikua anawafundisha nini sasa?
 
ngalau ya darasa la saba -sic
Elimu ya kumfanya ajiamini kuweza kutuwakilisha
Elimu ya kutambua Zimbabwe siyo kisiwa
Elimu ya kutosha kujua kuwa Bahari ya Hindi siyo nchi ( Kumbukeni alisema TZ imepakana na nchi 8 ikiwemo bahari ya hindi)

Elimu ya kumwezesha kuomba radhi kwa kufanya makosa na siyo kuongeza kosa kwa kujitetea kitoto.



Pia kwa waziri ambaye anatueleza kua amekua ni mwalimu (ingawa ualimu wake hauonekani kwenye CV ktk maana ya chuo cha ualimu alichosoma baada ya form 6, inaonekana wakati anafundisha ndo wakati alipokua anasoma OUT) alitakiwa kuwa na elimu ya kumwezesha kujua Zanzibar ni (Unguja + Pemba), lakini ukimsikiliza hata kwenye utetezi wake akiwa Clouds Fm anaonekana hajui kitu hicho.

Hakupaswa kuzungumza muungano TZ kwamba ni Zanzibar (Zimbabwe) + ''Pemba'' + Tanganyika kwa sababu kama kweli ni mwalimu wa Geography na History tena kiongozi wa serikali, alitakiwa kujua Pemba is already inside Zanzibar.

Muungano huo unatakiwa kua ni Zanzibar + Tanganyika. Na kama nia yake ilikua ni kuichambua Zanzibar, basi tungepata Unguja + Pemba, lakini kwake Mh. inaonekana Unguja kwake ndio Zanzibar. Wanafunzi waliofundishwa naye lazima watakua mashahidi wa kiwango chake cha uelewa.

Kifupi presentation yake ktk level ya kimataifa ilitia aibu kwa taifa, hata akijitetea vipi. Tunafahamu asingekaa kimya bila utetezi (mfa maji haachi kutapatapa) lakini angejitetea huku akijua kuna watu wenye uelewa kuliko yeye.

Watanzania wote hawawezi kua wanasiasa au mawaziri, hivyo yeye kua naibu waziri siyo kwamba ni exceptional. Kama ukimsikiliza alivyoongea Clouds Fm anasema ''SISI wanasiasa'' tunapoongea .......... as if they know more than others.
 
Anatosheleza kitu gani? Kwanza waliosoma naye wanasema alipokuwa Songea boys alitowekatoweka tu na kuibukia kwenye shule hiyo alikopewa nafasi kama adm Officer. Shule hiyo ilikuwa inaendeshwa na Wazungu na walipoondoka nchini dada zake Mulugo ambao ni masista waliachiwa kuiongoza ndipo walipomuita kaka yao. Baada ya hapo kaibukia kwenye siasa.

Swali la msingi hapa kusoma si tija ila je alifaulu vizuri? kuongoza Wizara nyeti kama ya elimu inahitaji weredi wa kutosha, je anatosha? maana alipokuwa akifundisha ktk shule hiyo aliwahi kutimuliwa na wakaguzi (kama anavyofanya yeye kwa wenzie sasa hivi)kwa kukosa sifa na vigezo.

Hivi hata kama mtu amekuandikia speech unaisoma kama ilivyo bila kuipitia na kuona ipo sawa? huenda aliipitia na kwa kuwa uwezo wake mdogo hakugundua makosa. kwa kuwa uwaziri is a political post kila mtu anaweza kuongoza? tuondolee utumbo hapa! ndio maana elimu imshuka hivi TZ kwa mizaha ya kipumbavu kama hiyo! kuna wasomi wangapi tz wanaoweza kuongoza wizara hiyo>? kila kitu siasa...siasa....siasa.....****!

ndo'huyu huyu aliyekuja na wazo la mtihani wa hesabu darasa la saba uwe multplechoice...!
 
Vyeti vya kufoji, assignments za degree zote unafanyiwa, bingwa la kuiba mitihani ya form four kwa ajili ya shule yake,....... What more trash is there about this guy?

Ndo maana hata hajui maana ya supplementary (exam), yeye alijua ni moja ya masomo yanayofundishwa chuo cha ualimu Mpwapwa.

Loh, asante mkuu wa kaya.
 
.......Akili ndogo haiwezi ongoza kwa ufasaha akili kubwa.....anafaa kuwa mbunge,lakini sio majukumu ya kitaifa kama aliyopewa hasa kwa kuzingatia ulimwenge wa sasa wenye changamoto nyingi.Walio na misingi inayoeleweka ndio wanafaa kusimama mbele ya mataifa na kutuwakilisha watanzania.Afadhali angekuwa naibu wa wizara ambazo sio core kwa maendeleo ya taifa na sio kuchezea elemu yetu.
 
Wadau naomba tuiangalie CV ya huyu Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi tuone kama ina kidhi majukumu mazito :

First Name: Philipo
Middle Name: Augustino
Last Name: Mulugo
Member Type: Constituency Member
Constituent: Songwe


EDUCATION
Rukwa Primary School, Chunga Primary Education 1982 1989 PRIMARY
Mbeya Secondary School O-Level Education 1990 1993 SECONDARY
Songea Boys' High School A-Level Education 1994 1996 HIGH SCHOOL
Open University of Tanzania BA (Economics Education ) 2002 2008 GRADUATE
CERTIFICATIONS

EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From Date To Date
The Parliament of Tanzania Member - Songwe Constituency 2010 2015
Southern Highland Secondary School School Managing Director 2008 2010
Southern Highland Secondary School Administrative & Personnel Officer 2005 2010
Southern Highland Secondary School Teacher 2000 2004
POLITICAL
Chama Cha Mapinduzi, CCM Member - National Executive Committee 2008
Chama Cha Mapinduzi, CCM Secretary General - Mbeya Region (Parents) 2008
Chama Cha Mapinduzi, CCM Member - Chunya District Political Committee 2007

............. Pamoja na yote Mheshimiwa huyu anazifahamu mbinu nyingi zinazofanywa na shule za sekondari ikiwemo uzembe na ujanja ujanja kwa maana hiyo amejitahidi kupambana nazo kwa kuwa alikuwa huko..............
 
Ukiona mtu amesoma OUT, lazima uwe na wasiwasi na uwezo wake kitaaluma. Hii nafasi haiendani na elimu yake, hana sifa ya kuwa ktk sekta ya elimu. He is as poor as dr dhaifu.
 
Tanzania nchi yenye neema kila kitu kinawezekana. Nyie wenye CV nzuri si hamtaki kuomba nafasi za uongozi kwa hiyo hakuan sababu za kulaumu.
 
Hii kweli ni aibu ya taifa.

  1. Tuko mwaka 2012 na sio 1961 halafu mtu mwenye uwezo dhaifu kama huyu anapewa kuongoza wizara muhimu kama ya elimu.
  2. Anashindwa hata kufanya presentation ambayo sio ajabu kasaidiwa kuitengeneza na ndio maana kaichanganya Zanzibar na Zimbabwe.
  3. Hivi Kikwete hii aibu kubwa kwa taifa yeye haioni na hajui kuwa wenzetu wanatucheka?
Raisi kilaza mawaziri ndio usiseme, wamechaguliwa tu kwa kujuana na sio kwa uwezo wao. When will Kikwete leave the presidency? Angalia hii video uone kama hutatokwa na machozi.
http://youtu.be/e3BNegmIUKM
<span style="color: rgb(0, 0, 128); font-size: medium; ">[video=youtube_share;e3BNegmIUKM]http://youtu.be/e3BNegmIUKM[/video]

Jamani, hamna Tanzania mpya nikimbilie?2015 naiona kama vle 2051, jaman muda ufike tuondoe haya magugu maji...
Pole nyingi sana kwa wa-TZ waliokuwemo mule ndani, kwani wao hope waliondoka kwa aibu tena bila kuaga!
 
............. Pamoja na yote Mheshimiwa huyu anazifahamu mbinu nyingi zinazofanywa na shule za sekondari ikiwemo uzembe na ujanja ujanja kwa maana hiyo amejitahidi kupambana nazo kwa kuwa alikuwa huko..............

.....So, tutegemee siku moja 'jambazi' akapewa wizara ya mambo ya ndani coz naye anauzoefu na anajuambinu nyingi za kihalifu??HAPANA
 
Unarusha mawe wakati upo kwenye nyumba ya vioo! Kama ulianza darasa la kwanza 1982 unatakiwa kumaliza darasa la saba mwaka gani?
Kweli wewe ni Babu na akili yako imezeeka:-
Haya, ngoja tukupeleke taratibu:
Mwaka 1982 - Darasa la I
1983 - Darasa la II
1984 - Darasa la III
1985 - Darasa la IV
1986 - Darasa la V
1987 - Darasa la VI
1988 - Darasa la VII
Sasa mwaka 1989 alikuwa anasoma darasa gani, au la VIII? Akili yako na ya M.k.w.e.r.e haina tofauti!
 
............. Pamoja na yote Mheshimiwa huyu anazifahamu mbinu nyingi zinazofanywa na shule za sekondari ikiwemo uzembe na ujanja ujanja kwa maana hiyo amejitahidi kupambana nazo kwa kuwa alikuwa huko..............
Wewe ni Pilau na kwa kweli pilau la Eid limekufanya uvimbiwe. BTW: Ukiona mtu ana maneno mengi sana, kila siku yuko kwenye TV utadhani yeye ndio Waziri wakati Boss wake yeye anatokea mara chache tena kwenye issues za msingi, basi ujue shule yake ni ndogo. Any politician who is provocative is intellectually retarded! Angalia Tambwe Hiza, Anna Kilango, Captain Komba, Lukuvi, Makamba Sr, M.k.w.e.r.e na majuha wengine wengi tuliowakabidhi maisha yetu utaona viwango vyao kielimu vilivyo na utata! Always greatest minds act in silence.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom