Mwanaukweli
JF-Expert Member
- May 18, 2007
- 4,789
- 1,732
Muft ameishiwa labda tumuulize yeye kama kiongozi amefanya nn ktk maendeleo ya Waislamu ktk nchi hii. Analolijua ni kuuza viwanja vya Waislamu kiongozi mkubwa kama yeye ameishia kuomba msaada wa kujengewa mskiti mfano hai dodoma{msikiti wa ghadafi} sasa hebu jiulize hivi kabla ya ule msikit waislamu wa dodoma walikuwa hawamuabudu mungu wao. Kama ulicheck EATV alionyesha dhahir kwamba anajitenga na watu wake anaowaongoza pale aliposema waliovamia wizarani sio waislamu bali ni kikund cha wahuni sasa hiyo ni lugha ya kutolewa na Muft au yeye alikuwa anafurahi waislamu kuwekwa rumande kwa kugomea sensa. Mimi siijui CV ya Ponda lakini fikra zake tu anamzidi Muft kielimu
Tumesikia kauli ya mufti nanukuu, (maneno yote hapa ni ya Mufti si yangu):
Nawatahadharisha Waislamu wote nchini kwamba Ponda Issa Ponda si mwanazuoni, si Sheikh, hakusoma elimu ya msingi ya kidunia wala ya kidini, hata Quran hajui kusoma. Anajaribu kuwatumia Waislamu kwa manufaa yake binafsi. Hatujawahi kushuhudia kutoka Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu Tanzania jambo lolote la maendeleo zaidi ya ghasia za maandamano, kupora misikiti na kudandia matukio na kuwachangisha Waislamu fedha, mwishoni mwa maandamano hayo huishia kuwatapeli waumini fedha zao ambazo huishia mifukoni mwa Ponda na wenzake.
"Ni kigenge cha watu wachache wenye kufuata madhehebu ya Mawahabi ambao kwa mujibu wa itikadi yao wanaamini kwamba Muislamu yeyote asiyefuata itikadi yao basi huyo siyo Muislamu na hafai kuwa kiongozi kwa ngazi yoyote ile"
"Vurugu, chokochoko na ghasia za uvamizi hazikuanzia Bakwata, wamekuwa wakifanya hivyo sehemu mbalimbali mikoani kwa kuvamia na kuteka misikiti na kuwaondoa viongozi waliochaguliwa kihalali kwa nguvu na udhalilishaji mkubwa na hatimaye kupora na kuhodhi rasilimali za misikiti hiyo."
"Wamekuwa wakiendesha mafunzo ya karate kwenye misikiti hiyo waliyoiteka na kuikalia kimabavu ili waweze kuendeleza dhuluma yao ya uporaji wa Misikiti na vituo vingine vya Kiislamu."
Ni vitendo vinavyokiuka maadili ya Uislamu. Kwa sababu hiyo nawaonya na kuwatahadharisha Waislamu wa madhehebu yote kuepuka vitendo vya uvunjaji wa sheria unaofanywa na kikundi hiki cha watu wachache.
Source: Mwananchi 21.09.2012
Mimi najaribu kutafuta ukweli katika haya anayosema mufti. Naombeni wanaofahamu vizuri CV ya Ponda watuwekee hapa.
Je ni kweli kuwa Sheikh Ponda ni wa dhehebu la Wahabi?
Wewe Wahabi unawajua ?
Ummati uliohudhuria kwenye maandamano na mkutano wa leo mbele ya sheikh ponda ni jibu kwa huyo anaejiita mufti. Na hilo tamko la mufti ni tamko aliloandikiwa na maaskofu alisome nilimuona alivo akilisoma kwa kunesanesa.
Ummati uliohudhuria kwenye
maandamano na mkutano wa leo mbele ya sheikh ponda ni jibu kwa huyo
anaejiita mufti. Na hilo tamko la mufti ni tamko aliloandikiwa na
maaskofu alisome nilimuona alivo akilisoma kwa kunesanesa.
Niwarudishe kwenye topic: Anayejua CV ya Ponda naomba atuwekee hapa.
Mgalatia bana ! Wewe umemnukuu mufti hapo na amekupa CV ya Ponda, sasa unauliza nini ? Hebu tafuta msalaba uuombe kisha ulale, usisahau kukojoa !
Mbona issue ni ndogo sana: ni CV ya Sheikh Ponda. Huko kwingine mnatoka nje ya mada.
umeinukuu hapo juu !
Sheikh Ponda ni mtu maarufu na ana mvuto mkubwa hapa Tanzania.
Watu maarufu wa namna hii huibua maswali mengi: nini siri ya mafanikio yake? Amesoma wapi? Amefanya nini kabla ya hapa alipo leo.
Kutuwekea hapa CV ya Ponda ni kujaribu kuongeza mvuto wa mtu huyu maarufu.
Kwa hiyo tafadhali mtujulishe huyu mtu alizaliwa wapi? lini?
Alikulia wapi? Alisoma shule gani? Mwaka gani? Amehitimu nini?
Ana uzoefu gani wa kazi? Wapi? Kwa miaka mingapi? ndio CV tunaomba ya Sheikh Issa Ponda.