Customer care wa hii mitandao ya kibongo hovyo sana

Customer care wa hii mitandao ya kibongo hovyo sana

kalou

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2009
Posts
4,992
Reaction score
3,880
kama unataka kuwasiliana nao hawa customer care inabidi uishushe roho yako...kama una hasira ziweke mbali kwa kuwa hawa jamaa ni pasua kichwa.

japokuwa wapo wachache sana ambao ukiongea nao unasikia kuwa wanajua wanachokifanya ila asilimia 80 ya ni kama hawajui wanachokifanya.

kwa kweli ukifikiria kuongea na customer care unaona bora usubiri hata siku mbili uende kwenye ofisi kuliko kuongea na hawa viumbe.

wengi wanaonekana kutokujua wanachokifanya.
wengine wanadharau sana.

kuna wale wanaoongea kama hawajapumzika wiki nzima..yaani wamechoka sanaa,wadai kuwa zile simu huwa zinarekodiwa...kama kweli hebu wahusika jaribuni kusikiliza hao watumishi wenu wanavyoongea na wateja wenu.

kuna siku niliambiwa na customer care eti nikate simu ili nikipiga tena niongee na mwingine kwa kuwa yeye hawezi kunisaidia..
mwingine aliniambia usikate simu mara akakata yeye..huku nikimsikia clear anavyobofya bofya.

CUSTOMER CARE JITAHIDINI KUWASAIDIA WATEJA..
 
pole mkuu kimsingi hakutakiwa kukwambia ukate simu upige kwani kuipata namba zao ya huduma ni kazi sana, alitakiwa achukue namba yako aipeleke kwa leader wake wakupigie na kutatua tatizo lako.
 
Yani ni tatizo sana customer care Si ya tigo wala vodacom zote ni majanga nadhani wengi siyo waelewa wa hizi huduma au hawajarithika na kazi zao sababu ya mishahara isiyotosha kujikimu maisha au kufanya kazi mda mrefu zaidi
 
Voda ndo wanaongoza kwa huo ushenzi, ata ukiwafuata kwenye page zao fb au twitter huko ndo balaa tupu!
 
Voda ndo wanaongoza kwa huo ushenzi, ata ukiwafuata kwenye page zao fb au twitter huko ndo balaa tupu!

sijui tatizo ni nini..yaani kuna siku nilikuwa nairobi nikawa na tatizo la kuongea na customer care ikabidi niwacheck voda kwa twitter ...amini usiamini hawa jamaa walikuwa hawajui kuwa kuna namba ya customer care special kwa watumiaji wa roaming...useless kabisaa..
 
airtel majanga tatizo la kupeana ajira kwa kujuana kwa Tanzania customer care ni tatizo unaweza kuingia badala ya kukuhudumia anaongea na simu we unaonekana kama sanamu fulanii hivi hakuna cha voda,tigo wala airtel wote ni wamoja
 
Ila bora tigo wanajibu japo pumba kwenye page yao fb. Mziki upo Airtel, wale ndo hovyo kuliko mitandao yote.
 
Airtel nadhan ndo wanaongoza kuanzia mda wakusubri ili uongee nao had kweny page zao za fb na twiter
 
mimi nilishawahi wapigia...walipopokea tu,nikaambiwa asante kwa kuchagua airtel na endelea kutumia airtel,halafu wakakata hapohapo..
 
ndio maana company zingine wanaajiri wakenya maana wabongo ni majanga matupu...unaweza kwenda sehemu unamkuta mdada kakazana kuchat na simu yake wakati wewe unamsubirie akuhudumie utakaa hapo nusu saa nzima hadi amalize kuchat....majanga.
 
Hvi airtel huwa wapokea simu kweli?,kiukwel sijawah pokelewa simu na customer wa airtel,.itaiiiita na kusubirishwa siku nzima. Mi nliamua kuhama mtandao angalau voda wanapokea haraka hata kama wanajibu utumbo
 
Nje wanaowekwa customer care hasa hiziza mitandao ni wale wenye knowledge kiasi flani na information technology, swali ukiwauliza wanaweza kufanya reasoning, sasa bongo full kupachikana tu, anapewa introduction kdg anaingia mzigoni, nilipiga nawaulizia service flani akaniambia hata hawajawahi isikia, ikabidi nipige later jibu nlilopewa nlitakani kuhama nchi
 
hebu malizia hilo jibu mkuu
 
Hvi airtel huwa wapokea simu kweli?,kiukwel sijawah pokelewa simu na customer wa airtel,.itaiiiita na kusubirishwa siku nzima. Mi nliamua kuhama mtandao angalau voda wanapokea haraka hata kama wanajibu utumbo

hah Hah hah...
 
Voda ndo wanaongoza kwa huo ushenzi, ata ukiwafuata kwenye page zao fb au twitter huko ndo balaa tupu!

wanakuambia tutumie inbox namba yako..hawa jamaa ni majanga matupu
 
Back
Top Bottom