CUF yapinga bara kupewa ardhi Z’bar

CUF yapinga bara kupewa ardhi Z’bar

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Chama Cha Wananchi(CUF) kimepinga wazo na rai ya kupunguza masharti ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ili kulegeza nguvu zake kisheria na kuwapa fursa Watanzania Bara kumiliki ardhi Visiwani Zanzibar.

Msimamo huo umetolewa na Mkurugenzi wa Habari na Mwasiliano ya Umma wa CUF Salum Bimani katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana visiwani humo, siku chache baada ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais(Muungano) Samia Suluhu Hassan, kushauri Katiba ya Zanzibar kuangaliwa upya na kuwapa nafasi Watanzania Bara kumiliki ardhi Zanzibar.

Bimani alisema kuwa suala la ardhi siyo la Muungano tangu mkataba wa awali wenye orodha ya mambo ya Muungano na siyo sahihi kufanyika marekebisho ili kuwapa nafasi Watanzania Bara kumiliki ardhi Zanzibar kwani ni ndogo na ndiyo sababu hata waasisi wa Muumgano waliamua ardhi hiyo imilikiwe na wazanzibari pekee. Chanzo mwananchi
 
kama mwendo wenyewe....ndoo huu cuf 2015....wasipokuwa makini kitapoteza mvuto bara.... kitabaki pemba tuuu
 
Lazima Tuwe wakweli. Hivi wakija Watu millioni 2 tu kutoka Bara wakataka ardhi kweli tunayo ardhi hiyo. WaZanzibari wapo 1.2 million kuna matatizo ya kugombea ardhi
 
unajua huu ni upuuzi viongozi kufikiri.changu tule wote,chako ufiche.muungano gani huu.Mungu ibariki Tanganyika!
 
Lazima Tuwe wakweli. Hivi wakija Watu millioni 2 tu kutoka Bara wakataka ardhi kweli tunayo ardhi hiyo. WaZanzibari wapo 1.2 million kuna matatizo ya kugombea ardhi

waambie waje Bara kuna ardi.kama watu wa bara na zanzibar hawawezi kuwa na mchanganyiko wa kudumu.muungano kuvunjika ni suala la muda tu.Mungu ibariki Tanganyika!
 
ninavyojua mimi ni kwamba wako Watanzania bara wengi tu wenye
kumiliki ardhi huko visiwani pamoja na makanisa ambayo ni ya bara;
au vp? Kiongozi anaemiliki hecta 500 Morogoro, 300 Bagamoyo, 250
Mbeya na bado anatamaa ya hect 400 Zanzibar ili azihodhi tu haiewzekani.
 
yaaani mimi toka nijue cuf...wamekuwa wakipigania......
1.uhuru wa wapemba........
2.sera zao zilijikita katika dini
3.muungano wa uvunjikee.....

Lakini wenzao chadema...muda mwingi wa wanaoutmiaa

1.katika kujenga hoja nzito bungeni......
2.kujenga chama chao....

3.kuunesha nia ya kwenda ikuluuu
 
Hivi watanganyika mna matatizo ya ardhi mpaka mupewe na ardhi ya zanzibar?sie wenyewe haitutoshi kaeni huko kwenu tanganyika mulime,zanzbr kwanza.
 
Lazima Tuwe wakweli. Hivi wakija Watu millioni 2 tu kutoka Bara wakataka ardhi kweli tunayo ardhi hiyo. WaZanzibari wapo 1.2 million kuna matatizo ya kugombea ardhi
kwani lazima wapewe? Cha msingi katiba ya zanzibar imekosea kuendekeza huo ubaguzi wa wazi!
 
ninavyojua mimi ni kwamba wako Watanzania bara wengi tu wenye
kumiliki ardhi huko visiwani pamoja na makanisa ambayo ni ya bara;
au vp? Kiongozi anaemiliki hecta 500 Morogoro, 300 Bagamoyo, 250
Mbeya na bado anatamaa ya hect 400 Zanzibar ili azihodhi tu haiewzekani.

Punguza hasira we mpemba makanisa yametoka wapi kwenye hoja hii na ninani anamiliki ardhi zenji kutoka bara labda ya shea
 
ninavyojua mimi ni kwamba wako Watanzania bara wengi tu wenye
kumiliki ardhi huko visiwani pamoja na makanisa ambayo ni ya bara;
au vp? Kiongozi anaemiliki hecta 500 Morogoro, 300 Bagamoyo, 250
Mbeya na bado anatamaa ya hect 400 Zanzibar ili azihodhi tu haiewzekani.
mkuu huu muungano ni wa kitapeli sana! Wazanzibar waachwe salama..
 
Hivi watanganyika mna matatizo ya ardhi mpaka mupewe na ardhi ya zanzibar?sie wenyewe haitutoshi kaeni huko kwenu tanganyika mulime,zanzbr kwanza.
wapemba wajiandae kuja kumiliki ardhi huko pemba na unguja! Tumechoka na huo unyanyasaji wenu kwa wabara walioko zanzibar!
 
Kwa kuwa suala la ardhi si la muungano basi hata Wazanzibari walioko bara wasiruhusiwe kumiliki ardhi bara. Wapemba waliojazana bara watambue kwamba wao ni wapangaji tu. Wakamiliki ardhi kwao na si bara!

Inategemea kama kuna vipengele hivyo mkuu.
 
Bimani mwenyewe aliyetoa press conference huyo hapo kwenye picha. Mwangalie kwa makini halafu tuambie umegundua nini. Kazi kwako.

salum_bimani.jpg
 
Hizo ndio siasa za vibaraka wa ccm, ukiwa kibaraka ccm inakubidi ujitoe ufahamu kwanza, cuf hawajui kuwa wanaumiza ndugu zao wanaoishi bara.
 
Hapa nilipo kuna jirani yangu ambaye ni mzanzibar pure na anamiliki ardhi ya kutosha. Sasa huu uzi umenifungua macho kuwa kumbe ile ardhi inaweza kuwa yangu muda wowote,ni suala la muda tuuuu. Huyu jirani yangu alishawahi kumkatalia mtoto wangu wa mwanaume alipoenda kuchumbia kwake kwa kigezo cha kwamba suala la kuoleana si la muungano!!!!, kumbe hata ardhi nayo cyo suala la muungano!! Huyu jamaa atanikoma kwenye hili suala la ardhi lazima alikimbie jiji la sivyo akubali kijana wangu amuoe binti yake.
 
duh...mkuu hesabu na reaction zako zinatisha...hiyo decimation unayomfanyia uyo mzenji ingekuwa kwenye battle field ange surrended within few minutes
 
Back
Top Bottom