CUF yaiachia CHADEMA kata zote uchaguzi mdogo

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,251
2,000
CHAMA cha Wananchi CUF kimesema hakijasimamisha mgombea yoyote katika chaguzi za marudio zinazotarajiwa kufanyika Januari 22 mwakani katika kata 20.

Akizungumza na MwanaHALISI Online leo jioni Shaweji Mketo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CUF amesema hatua hiyo inatokana na mgogoro unaondelea ndani ya chama hicho.

Mgogoro unaoendelea ndani ya CUF ni juu ya Prof. Lipumba aliyejiuzulu uenyekiti wa chama hicho Agosti 2015 lakini Juni 2016 akatangaza kutengua uamuzi wake na kuirejea nafasi hiyo huku uongozi wa CUF chini ya Maalim Seif ukipinga na hatimaye kumvua uanachama lakini ameendelea kutambulika na Msajili wa Vyama vya Siasa.

Mketo amesema hapo awali CUF ilikutana na vyama washirika katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) – Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), NCCR – Mageuzi na National League For Democracy (NLD) ili kujadili namna vyama hivyo vitavyoshiriki katika uchaguzi ikiwemo kuachina kata.

“Sisi CUF tulikutana na vyama washirika wa ukawa katika kamati ndogo ya ufundi ya Ukawa ambapo tulikubaliana mambo kadhaa kuhusu kuachiana kata.

Wakati tukijiandaa kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu ushiriki wa Ukawa katika uchaguzi wa marudio, ghafla akajitokeza Magdalena Sakaya (Mbunge wa Kaliua – CUF ambaye ni mfuasi wa Prof. Lipumba) na kutangaza kuwa CUF itasimamisha wagombea katika kata zote,” amesema Mketo.

Ameongeza kuwa, “Ieleweke kuwa hatujasimamisha wagombea sehemu yoyote na Sakaya na wenzake kutangaza kusimamisha wagombea katika kata zote ni utekelezaji wa kazi zao za kukisaidia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupata ushindi.”
 
Mshangai

JF-Expert Member
Feb 16, 2008
452
1,000
CUF inayotambuliwa ni ya mwenyekiti Lipumba hiyo ya akinqa MKETO nA Seif ni CUF koko.Hitambuliwi.WAtasemaje hawajasimamisha wagombea watu ambao hawatambuliwi na msajili.Mketo alitakiwa aseme hatujasimamisha sababu ni wanaharamu hatutambuliwi.
Ulimsikia mkurugenzi wa NEC alivyosema? Kutokana na mgogoro huo kila mgombea lazima aidhinishwe na pande zote mbili hivyo hao watakao pendekezwa na kundi la Lipumba watapata wapi sahihi ya upande wa pili? Hapo tayari wamechemsha.
Namwonea huruma sana Sakaya kwa kuharibu future yake kisiasa baada ya kumfuata Lipumba anayefahamika wazi kuwa anatumika na ccm ambayo nayo inafutika
 
sweettablet

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
5,875

Masahihisho Mkuu. Kwa nafasi ya Mbunge ndio mgombea wao anatakiwa aidhinishwe na pande mbili. Kwa wagombea udiwani wataidhinishwa na viongozi wa ngazi husika huko chini.
 
DUBULIHASA

JF-Expert Member
Nov 26, 2016
1,856
2,000
Ila hii dunia ni ya ajabu sana na pia mara nyingine matukio mengi ukiyatafakari sana utashangaa mno, hebu jiulize swali dogo hivi kwa nini wafuasi wengine wa Cuf wanampenda Lipumba aendelee kuwa Mwenyekiti wa chama wakat haonyesh jipya lolote miaka nenda miaka rudi. Nimeamin kwel chama cha Cuf kina vilaza wengi na ndio maana kina mashabiki weng kutoka maeneo ya mikoa ya pwani.
 
ITEGAMATWI

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
4,760

Mkuu umetumia vigezo gani kusema wafuasi wengi wa CUF wanamuunga mkono Lipumba?
 
Mthuya

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
1,415
1,225
CUF inayotambuliwa ni ya mwenyekiti Lipumba hiyo ya akinqa MKETO nA Seif ni CUF koko.Hitambuliwi.WAtasemaje hawajasimamisha wagombea watu ambao hawatambuliwi na msajili.Mketo alitakiwa aseme hatujasimamisha sababu ni wanaharamu hatutambuliwi.
Lumumba tulieni haya hayawausu
 
Mthuya

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
1,415
1,225
Ila hii dunia ni ya ajabu sana na pia mara nyingine matukio mengi ukiyatafakari sana utashangaa mno, hebu jiulize swali dogo hivi kwa nini wafuasi wengine wa Cuf wanampenda Lipumba aendelee kuwa Mwenyekiti wa chama wakat haonyesh jipya lolote miaka nenda miaka rudi. Nimeamin kwel chama cha Cuf kina vilaza wengi na ndio maana kina mashabiki weng kutoka maeneo ya mikoa ya pwani.
Lipumba hana mfuasi anaempenda bali yupo na mamluki
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom