CUF yaendelea kumeguka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF yaendelea kumeguka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Mar 1, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  Jinamizi linaloendelea kukitesa Chama cha Wananchi (CUF) limeendelea kukigubika chama hicho, kufuatia Uongozi wake Manispaa ya Mtwara-Mikindani kujiuzulu.

  Tukio hilo lilitokea jana baada ya kundi la watu wnaodaiwa kuwa ni wanachama kuvamia ofisi za chama hicho na kushinikiza kujiuzulu kwa uongozi wote wa manispaa. Katika kutii amri hiyo, Mwenyekiti wa chama hicho, Salum Mchimbuli, alitangaza kuvunjwa kwa kurugenzi zote kisha na yeye kujiuzulu.

  Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa uongozi wa chama hicho ulikuwa katika kikao cha ndani ambapo pamoja na mambo mengine, kilikuwa kinajadili taarifa ya aliyekuwa mgombea ubunge wa chama hicho, Uledi Abdallah, kujivua uanachama.

  “Walikuwa katika kikao cha ndani,ghafla kundi la watu waliojitambulisha kuwa ni wananchama walivamia ofisi na kutaka kufanya vurugu…Mwenyekiti aliwasihi wasifanye vurugu huku akiwauliza shida yao, kundi hlo la vijana likasema kuwa wanataka uongozi wote ujiuzulu,” alisema mmoja wa wajumbe.

  “Abdallah alitangaza nia ya kujiondoa katika chama hicho kwa madai kuwa chama hicho kimekaribia kufa hivyo hana budi kuachana nacho,” alisema.

  Aliyekuwa Katibu wa CUF, Said Kulaga, alithibitisha kurungezi zote kujiuzulu pamoja na mwenyekiti. “Ni kweli tukio hilo limetokea na Mwenyekiti alitumia busara ili kuepusha madhara, lakini ni kinyume na katiba ya chama,” alisema Kulaga.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,893
  Likes Received: 5,346
  Trophy Points: 280
  hakuna chama kinachoitwa cuf...kuna ccm B
   
 3. tembeleh2

  tembeleh2 JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 768
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Na bado, Dhambi ya unabii utaendele kukitafuna chama hicho.
   
 4. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,660
  Likes Received: 17,666
  Trophy Points: 280
  prof.safari aliliona mapeeema, yupo huku nyumbani jikoni kabisa tunapopika chakula cha watz 2015
   
 5. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hivi bado hiki chama kipo? cuf si imebakia pemba kwa **** na maalim
   
 6. Rock City

  Rock City JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,270
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Yaani CUF inakufa kifo kibaya kabisa, ngome zake zote ndipo inpoporomokea. Bado Lindi na Tabora hatujasikia
   
 7. z

  zamlock JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  yan cuf inakufa jaman nawaonea huruma sana
   
 8. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #8
  Mar 1, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,507
  Likes Received: 1,683
  Trophy Points: 280
  Mtwara hakuna mwanachama wa KAFU ambaye ni mkristo?
   
 9. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #9
  Mar 1, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,507
  Likes Received: 1,683
  Trophy Points: 280
  Tena ife haraka. Wasije wakatuletea boko haram nchini kwetu. Hao sio wa kuwaonea huruma hata kidogo
   
 10. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #10
  Mar 1, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Safari imewadia leo Musoma wanavunja kambi......dhambi hii cjui itawatafuna hadi lini?
   
 11. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #11
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,046
  Likes Received: 13,259
  Trophy Points: 280
  Kadi za uanachama zinapatikana misikitini kwa Maimamu. na ndio maana Uzini ni jimbo gumu kwao kwa sababu lina Wakristo na Wabara wengi.
   
 12. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #12
  Mar 1, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sio mbaya chama chao kitabaki hukohuko visiwani.....hasa Pemba na si unguja kwani hawajawahi kuwa na power hiyo unguja, unguja ni ngome ya ccm na kwakuwa walishindwa kuivunja kipindi wako ngangari basisasahv wako rojorojo nina hakika wataishia stori. Ni sawa na mtu uende marekani then urudi na picha tu baaasi,utaishia kusimulia tu marekani hivi vile zaidi huna.
   
 13. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #13
  Mar 1, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  UDINI utakuteketeza wewe kijana! Bila shaka wewe una ugonjwa mbaya sana wa Islamaphobia!!
   
Loading...