CUF ya Lipumba na CHADEMA 2020 tutaishinda kweli CCM kwa mwendo huu

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
CUF ya Lipumba ni mwenyekiti bado Lipumba na Katiba ya CUF mwenyekiti hana kikomo

Chadema ya Mbowe pia mwenyekiti ana kikomo.

CUF ya Lipumba imeshiriki uchaguzi mdogo wa kata 43 na ccm ikashinda kata zote

Chadema imeshiriki kata 43 na CCM imeshinda kata 42 kati ya CCM.

Chadema chini ya mwenyekiti Mbowe madiwani na wabunge wanajiuzulu na kurudi ccm.

CUF chini ya lipumba nayo pia madiwani na wabunge wanajiuzulu na kurudi CCM

CUF chini ya lipumba wanaipinga Chadema na Chadema ya Mbowe wanampinga Lipumba wakati CCM inasonga mbele.

Chadema ya Mbowe wamesusia uchaguzi CCM imeshinda lakini pia CUF imeshiriki uchaguzi ccm imeshinda.

CUF ya lipumba ina mgogoro na katibu mkuu Maalim Seif na chadema ya mbowe ina mgogoro na lowassa umeshanza.

Chadema ya mbowe haimuamini tena CUF ya Lipumba na CU ya lipumba hawaiamini tena chadema mbowe.


Chadema ya mbowe imekuwa ikimponda lipumba ni msaliti

Lakini pia cuf ya lipumba imekuwa ikiwaponda chadema ni mafisadi na wezi wa democrasia.


Je kwa mwendo huu cuf na chadema mtaweza kweli kupambana na ccm 2020.
 
Lipumba kwa muda huu anafanya kazi ya CCM.

Lipumba amerudishwa na CCM baada ya kujiuzulu kwa kuwa CCM walihitaji kutatua mambo mawili yaliyokuwa yanawakera.

La kwanza ni UKAWA. Hakuna kitu CCM wanakihofia kama vyama vikuu vya upinzani kuungana. CCM wanafahamu kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. CCM walimpata mtu ambaye ana uwezo wa kuvuruga umoja huo UKAWA katika nafsi ya Lipumba. Ndio maana tunaona msajili alivyojiingiza kumkingia kifua Lipumba. Ndio maana Lipumba alisindikizwa na Polisi kuingia ofisini, na ndio maana dola inamkingia kifua Lipumba kupata ruzuku.

La pili ni mgogoro wa uchaguzi wa Zanzibar. Zanzibar kuna madai ya CUF kwamba walinyang'anywa ushindi. CCM iliona namna ya kudoofisha madai hayo ni kupandikiza mgogoro ndani ya chama kwa kumrudisha Lipumba madarakani.

Kwa hiyo mleta uzi ufahamu kwamba Lipumba yuko hapo kuwezesha mambo ya CCM yafanikiwe. Wapinzani wanapokuwa na sababu za msingi kususia uchaguzi, Lipumba anashiriki. Lipumba anashiriki si kwa nia ya kushinda, ila kwa nia ya kuupa uhalali uchaguzi licha ya kasoro nyingi za uendeshaji wa uchaguzi kwa tume ya uchaguzi.

Kwa upande wa Mbowe, ujue kuwa nguvu kubwa za dola zinatumika kutisha wabunge na madiwani na hata kuhujumu shuguli zao za kiuchumi ili waone hasara ya kuendelea kuwa ndani ya vyama vya upinzani. Hata rushwa imetumika. Aliyekuwa DC wa Arumeru alichukuliwa video akiwa anashawishi kununua diwani, na TAKUKURU imepuuzia hilo. CHADEMA inahujumiwa kwa kutumia nguvu za dola. Hii ni kosa kisheria. Kosa kama hili lilimfanya Nixon ajiuzulu urais Marekani.
 
Hapo kuna vitu vingi sana vinaisaidia CCM kushinda kwanza Lipumba,tume ya UChaguzi,Police MKUU WA MKOA MKUU WA WILAYA DED TAKAKURU
 
Ingawa umeandika kwa herufi kubwa lakini una hoja kubwa sana.

Kuandika kwa herufi kubwa ktk ulimwengu wa mitandaoni maana yake una shout hayo maneno.
 
Hapo kuna vitu vingi sana vinaisaidia CCM kushinda kwanza Lipumba,tume ya UChaguzi,Police MKUU WA MKOA MKUU WA WILAYA DED TAKAKURU
KAMA TATIZO NI LIPUMBA ILIKUWAJE UCHAGUZI MKUU 2015 TULIANGUKA UCHAGUZI MKUU LIPUMBA HAKUWEPO.

LIPUMBA AMERUDI CUF VIPI KUHUSU 2020 TUKISHIDWA TUMLAUMU LIPUMBA .
 
Hapo kuna vitu vingi sana vinaisaidia CCM kushinda kwanza Lipumba,tume ya UChaguzi,Police MKUU WA MKOA MKUU WA WILAYA DED TAKAKURU
HADI SASA TUNAVYOZUNGUMZA NDANI YA CHADEMA KUNA MADIWANI 21 WAMEJIUZULU.

CHAMA KINAZIDI KUOTEZA MWELEKEO NA HAPA TUMLAUMU KWELI
 
Back
Top Bottom