CUF wataka serikali ya umoja wa kitaifa Tanzania Bara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF wataka serikali ya umoja wa kitaifa Tanzania Bara

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Nov 7, 2011.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1][/h]Written by Hassan10 // 07/11/2011 // Habari // 1 Comment


  [​IMG]Makamu Mwenyekiti wa Cuf taifa, Machano Khamis Ali

  Saturday, 05 November 2011 20:42Claud Mshana
  CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema matatizo ya kiuchumi yanayoikabili Serikali yatamalizwa kwa kuundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. CUF imesema Serikali ya Rais Jakaya Kikwete imeelemewa na majukumu ya kuongoza na hivyo kuhitaji msaada kwa kuundwa serikali hiyo kama ilivyo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, visiwani.
  Tamko la Baraza Kuu la Uongozi Taifa la chama hicho lililotolewa jana na Makamu Mwenyekiti wa Cuf taifa, Machano Khamis Ali lilisema Serikali ya CCM kushindwa kutatua matatizo makubwa yanayolikabili taifa ni dalili za kuwepo kwa ombwe la uongozi.
  Ali alitaja matatizo hayo kuwa ni kuyumba kwa uchumi, kushuka kwa kiwango cha mapato ya serikali, kuporomoka kwa shilingi na mfumuko wa bei na matatizo ya ajira. “Baraza Kuu linaona njia pekee ya kulitoa taifa hapa tulipofikishwa ni kwa rais Jakaya Kikwete na CCM kukubali kusaidiwa dhamana ya kuongoza nchi kwa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Ali.
  Aliongeza kuwa hatua hiyo pia itaisaidia nchi kuvuka salama katika mchakato wa kuandika katiba mpya ambayo itasaidia kuyapatia ufumbuzi matatizo hayo. Ali alisema serikali ya CCM imeshindwa kutatua tatizo la upatikanaji wa nishati ya umeme na kuongeza kuwa tatizo la nishati hiyo linachangiwa na kuingizwa siasa na si utaalamu au rasilimali fedha.
  “Miaka 50 baada ya kupata uhuru, hatuna sababu ya kutokuwa na umeme wa uhakika, serikali imeshindwa kutatua tatizo hili na kusababisha nchi kupata hasara kubwa kwa kudhoofisha uchumi wa nchi,” alisema. “Baraza Kuu linaitaka serikali ya CCM kufanya maamuzi mazito ya kuwashughulikia wahusika wote wa uzembe huu kwa kuwachukulia hatua zinazofaa,” aliongeza Ali.
  Alifafanua kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar imefanikiwa katika kipindi cha mwaka mmoja kwa kusimamia uendeshaji wa shughuli za serikali katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupanda kwa bei ya zao la karafuu.
  Katiba mpya Kuhusu mchakato wa kuandikwa kwa Katiba Mpya, chama hicho kilisema rasimu mpya ya muswada huo bado inakasoro kwani bado umeweka madaraka na mamlaka makubwa kwa rais katika kudhibiti na kuamua mchakato wa kuandika katiba mpya.
  “Hili linavunja msingi mmoja wa madai ya katiba mpya ambayo ni kupunguza madaraka makubwa ya rais,” alisema na kuwataka wabunge wa Cuf kuhakikisha wanasimamia marekebisho yake ndani ya Bunge linalotarajiwa kuanza keshokutwa.
  Mwananchi news papes
   
 2. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,499
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280
  Wazo zuri kama wataanzisha na CCM B (CUF), CHADEMA hawawezi kukubali upuuzi huo!! Kwa hiyo ina maana CCM B wameshakubali kuwa serikali imeshindwa kazi siyo?? Sasa ngoja tusubiri Magamba, nafikiri nayo si siku nyingi yatakubali hadharani kuwa nchi imewashinda!!
   
 3. M

  Mgongo wa paka JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 486
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  chaga development. Kweli hawawezi kwani hawapo kwa ajili ya taifa, nawapo kwa manufaa yao so ukiwaweka kwenye umoja hawatapata maslahi ndio maana hata umoja wa upinzani hawataki tuna vyojuwa wachaga
   
 4. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Sawa mkuu.
  Sasa kakojoe ukalale.
   
 5. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #5
  Nov 7, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Wewe wasemeseme Wachagga tu hujui kuwa nusu ya kwenu Kiwangwa wameshaichukua..
   
 6. f

  firehim Member

  #6
  Nov 7, 2011
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Siku ile wakati kikwete akiapa kwa mara ya 2, CUF kupitia mwenyekiti wao Prof. Ibrahim Lipumba walikabidhi ilani ya chama chao kwa Kikwete ili isaidie kuongoza nchi. Ina maana Serikali hii legelege tayari inaendeshwa kwa ilani ya vyama viwili yani CCM-A na CCM-B (CUF). Hivyo hamna haja ya kuanza kulalama. Bara tunahitaji mapinduzi sio Umoja wa kitaifa.
   
 7. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #7
  Nov 7, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,689
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  Afrika Kusini mbona huwa wanafanya hivyo? Mgombea urais kuna idadi ya kura akipata anapewa Uwaziri ktk serikali itakayoongoza.Nalog off
   
 8. M

  Marytina JF-Expert Member

  #8
  Nov 7, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  CUF wanatafuta wali wa Lipumba kwa bara
   
Loading...