CUF: Wasiotaka Serikali ya Umoja wafukuzwe

CUF: Wasiotaka Serikali ya Umoja wafukuzwe

rosemarie

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2011
Posts
6,887
Reaction score
3,439
Zanzibar. Chama cha Wananchi (CUF) kimesema wanasiasa wanaojadili suala la kuendelea au kutokuendelea na Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), wanastahili kujiuzulu au kufukuzwa ndani ya vyama vyao.

Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Mnadhimu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW), Salmin Awadh Salmin kusema kuwa Wawakilishi wa CCM wanajiandaa kuwasilisha hoja binafsi kwenye Baraza hilo ili kuwapa nafasi wananchi waulizwe iwapo wanataka kuendelea na Serikali ya Umoja wa Kitaifa au vinginevyo.

Salmin aliyasema hayo juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Kibandamaiti, Unguja kwa kuwa wanaona kwamba lengo la kuundwa kwake halina dalili njema kwa siku za usoni.

Jana, Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Salum Abdallah Bimani alisema: “Kimsingi mpango huo unakwenda kinyume na uamuzi wa vyama vya CCM na CUF ambao ulipitishwa na kuridhiwa na vikao vya juu vya vyama hivyo viongozi wanaopinga jambo hilo wanaonyesha kupingana na uamuzi wa vyama vyao.”

Ajenda ya siri

Mkurugenzi huyo wa CUF alikana chama chake kuwa na ajenda ya siri ya kuvunja Muungano au kuyasambaratisha Mapinduzi ya Zanzibar na kusema kinachopiganiwa ni muungano wenye usawa, haki na heshima kila upande wa washirika.

Kuhusu Ukawa kususia Bunge Maalumu la Katiba, Bimani alisema chama chake kimetoa masharti matatu yanayopaswa kuzingatiwa kabla ya kubadilisha msimamo wake. Alitaja masharti hayo kuwa ni kuijadili Rasimu ya Katiba kama iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba; wajumbe wa CCM kuacha matusi, vijembe na ubaguzi na hilo lithibitishwe kwa maandishi na viongozi wake wa kitaifa.

Jambo la tatu ni kuhakikishiwa kuwa vikao vya Bunge vitumike kujadili rasimu na si sera za vyama vya siasa kwa vile ndiyo mwanzo wa kukaribisha malumbano na kusababisha Bunge kupoteza mwelekeo na kuweka nyufa katika Umoja wa Kitaifa.

Mbatia alaani

Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia amelaani kauli zilizotolewa na viongozi wa CCM katika mikutano yake ya Unguja na Pemba.

Mbatia alisema kuwa hoja ya CCM kutaka kufuta Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar inapaswa kulaaniwa kwani italeta machafuko. “Serikali ya Umoja wa Kitaifa si ya CCM na CUF tu, ni ya wananchi wote, ni makosa makubwa kudhani kuwa Serikali hiyo ni ya vyama hivyo viwili. Ilifanyika hivyo ili kutokuendelea umwagaji damu,” alisema Mbatia.

Mbatia alisema madai ya CCM kuwa Maalim Seif hatalipwa mafao yake hayana msingi wowote kwa sababu anacholipwa ni haki yake. “Kwani hayo mafao ni ya CCM au wanaolipa kodi ni CCM tu? Ukweli ni chanzo cha amani na haki ni msingi wa amani, ukweli utatuweka huru.”
 
Cuf na tamaa za fisi mla watu, mtaka vyote hukosa vyote
 
Hivi mume halisi wa cuf ni ccm au huyu mpya chadema maana....
 
Tatizo ni la CHAMA changu kutowafunga midomo wanachama wake hata pale wanapohatarisha AMANI na mustakabali wa nchi.
 
Ni sawa kabisa lakini kwanza wazanzibari waulizwe Je muungano wanautaka? Halafu ndio lije hilo swali ya umoja wa kitaifa
 
Japo hujaweka source ya hii taarifa lkn maudhui yanaonyesha ni gazeti la Mwananchi!
Mwananchi= UKAWA!
 
Mimi nafikiri MAWAZO YA CCM YA KUTAKA ZNZ IPIGE TENA KURA YA MAONI YA KUAMUA MFUMO WA SERIKALI YAKE wangeyaweka na kuwa kwa TANZANIA NZIMA IPIGE KURA YA MAONI YA KUAMUA AINA YA MUUNGANO WANAOUTAKA ili kuikwamua Bunge la Katiba Mpya ili liweze kuendelea bila kuwa na kikwazo.

Kwani kuwakhusisha wananchi katika suala la muungano ni kitu muhimu na sahihi.

Tujiulize kwanini maoni ya Tume ya Warioba yasihishimiwe?
 
Ni sawa kabisa lakini kwanza wazanzibari waulizwe Je muungano wanautaka? Halafu ndio lije hilo swali ya umoja wa kitaifa

Na the same question waulizwa wa TGK kwani wote ni wadau wa huo mvungano wenu. najiuliza KWANINI WATGK WASIULIZWE?

 
Back
Top Bottom