CUF waridhia uamuzi wa JK; Wampongeza kusaini muswada mabadiliko ya katiba na kumuunga mkono | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF waridhia uamuzi wa JK; Wampongeza kusaini muswada mabadiliko ya katiba na kumuunga mkono

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Dec 5, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Dec 5, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2]05 DECEMBER 2011[/h][h=3][/h]

  *Wampongeza kusaini muswada mabadiliko ya katiba
  *Wasema uamuzi huo umezingatia kilio cha Watanzania
  *Sasa waahidi kumuunga mkono hatua zote za utekelezaji


  [​IMG]

  Na Peter Mwenda

  CHAMA cha Wananchi (CUF), kimeridhia na kupongeza hatua ya Rais Jakaya Kikwete kusaini muswada wa kuratibu maoni ya kutekeleza Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya 2011. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Bwana
  Julius Mtatiro, alisema ujumbe wa chama hicho ulikwenda Ikulu kuonana na Rais Kikwete sambamba na kupongeza hatua ya Serikali kukubali madai ya muda mrefu ya Watanzania kutaka Katiba Mpya.

  Alisema katika Ilani ya Uchaguzi wa CUF mwaka 1995, 2000, 2005 na 2010 ilikuwa na madai ya kutaka Katiba Mpya pamoja na Tume Huru na Uchaguzi ambapo madai hayo ndio yalichangia kufanyika maandamano ya amani yaliyoitishwa na chama hicho Januari 27,2001.

  “Tunapofikia hatua ya Rais Kikwete kukubaliana na madai ya wananchi, hatua budi kumpongeza na kumuunga mkono katika hatua zote za utekelezaji wa suala hili muhimu katika historia ya nchi yetu,” alisema Bw. Mtatiro.

  Alisema mapendekezo waliyowasilisha kwa Rais Kikwete, wameomba uteuzi wa Makamishna wa Tume ya Katiba na sekretarieti yake, wateuliwe na Rais Kikwete kwa kushauriana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein.

  Alisema Makamishna na sekretarieti hiyo wawe watu waadilifu, wanaoheshimika mbele ya jamii na wenye ujuzi na uzoefu wa kutosha katika masuala ya katiba wakiwa na uelewa mpana wa mambo ya sheria, siasa, uchumi na maendeleo.

  Bw. Mtatiro alisema pia CUF inapendekeza wajumbe wa Sekreterieti ya Tume ambao kwa mujibu wa Sheria watateuliwa na Waziri wa Katiba na Sheria wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi. Celina Kombani na Waziri wa Katiba Zanzibar, wawe watu wenye sifa na vigezo sawa na Makamishna wa tume.

  Alisema CUF imemwomba Rais Kikwete baada ya kupokea hadidu za rejea za maoni ya wananchi, yasipelekwe moja kwa moja kwa rais badala yake tume itoe hadharani na kuzichapisha moja kwa moja katika vyombo vya habari.

  Aliongeza kuwa, pia kuwepo upana usio na vikwazo kwa wananchi kutoa maoni yao kwa sababu wao ndiyo watakaoihodhi na kuimiliki katiba, ila wafanye hivyo kwa njia ya amani na utulivu na kuondoa dhana potofu kuwa lengo la serikali ni kubana uhuru wa wananchi katika kutoa mapendekezo.

  Bw. Mtatiro alisema CUF imependekeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), zinanyiwe marekebisho kuwa Tume Huru kabla ya 2014, ili zisiweze kutiliwa shaka katika matokeo ya kura.

  “Vyama vya siasa haturidhiki wala hatukubaliani na mfumo wa sasa wa NEC kuwatumia Wakurugenzi wa Halmashauri na wasaidizi wao kuwa ndiyo wasimamizi wa uchaguzi katika wilaya na majimbo.

  Aliongeza kuwa sheria ya uchaguzi zifanyiwe marekebisho ili kuweka muundo mpya wa Tume ya Uchaguzi na sekreterieti yake ambapo tume ikiendelea kukusanya maoni, mchakato wa kufanya marekebisho ya katiba sasa na sheria za uchaguzi uanze kwa kushirikisha serikali, wadau wa vyama vya siasa na kiraia.

  Alisema CUF inapendekeza marekebisho ya kifungu 6(4) kuondoa sharti linalokataza kiongozi wa chama cha siasa ngazi ya Taifa, Mkoa na Wilaya kuteuliwa kuwa mjumbe wa Tume ya Katiba kwa sababu kazi hiyo inahitaji watu wazoefu katika mambo ya siasa.

  Kifungu 9(2) CUF wamependekeza maeneo yaliyotajwa kuanzia kifungu (a) hadi (I), yasiwekwe vikwazo wakati wananchi wakitoa maoni yao na wawe huru kutoa maoni yote waliyonayo ambayo itakuwa ni jukumu la tume kuyaratibu na kuyakusanya.

  Alisema pia CUF imependekeza kuwa kifungu 32, kiwango cha kura za wananchi kuhalalisha Katiba Mpya, kibadilishwe kutoka zaidi ya asilimia 50 kwa Tanzania Bara na 50 kwa Tanzania Zanzibar hadi theluthi mbili za kura za ndiyo.

  Aliongeza kuwa, walipendekeza kifungu cha 33 kifanyiwe marekebisho ili Tume ya Katiba ivunjwe mara baada ya kukamilisha kazi yake, kukabidhi ripoti na rasimu ya Katiba Mpya kwa Rais.

  “Kama kila mjumbe mmoja analipwa sh. 500,000 kwa siku wakati wamekamilisha kazi yao, huo ni ubadhirifu wa fedha za umma, wakikamilisha kazi tume hiyo ivunjwe,” alisema Bw. Mtatiro.

  Alisema CUF imetoa mapendekezo hayo kwa kuzingatia kuwa, ilishiriki katika muswada huo bungeni na kasoro walizogundua na kuziwasilisha zitafanyiwa marekebisho.

  Bw. Mtatiro alisema kutokana na maafikiano waliyofikia, CUF hawataitisha maandamano ya kulazimisha mapendekezo hayo yakubaliwe.   
 2. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Waifu ni waifu tu hawezi kumgomea mumewe kwa chochote. Na nilijua tu wametumwa na magamba kumaliza makali ya cdm, na hawajaweza kwani haki itasimama kwa vyovyote
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hivi CUF ni wanafiki,wanasumbuliwa na ndoa yao na CCM? Walishiriki kupitisha sheria hiyo bungeni, walikuwa wapi kutoa hoja hizo, badala yake waliishia kuijadiri CHADEMA wakaacha kujadiri mswada uliokuwa mbele yao. Kwa jinsi hii tutafika kweli?
   
 4. mwanapolo

  mwanapolo Senior Member

  #4
  Dec 5, 2011
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 194
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa hizo point za CUF nazikubali, ila ninashangaa mbona hawakuziongelea bungeni? Bungeni walikubali kila kitu.
  Kigeugeu chao ndo maana wanapoteza umaarufu
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Dec 5, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Sielewi CUF Tanzania Bara wanapata wapi ujasiri wa kuongea mbele za watu? Sasa tunaelewa kwa nini hakuna la maana lilifanyika wakati CUF wakiwa ndio chama kikuu cha upinzani! Housegirl!
   
 6. T

  Topical JF-Expert Member

  #6
  Dec 5, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Chama cha CUF kimefanya jambo la maana ili tuendlee tupate katiba mpya..tunakiwa kushirikiana na tume ..kuzira ni dalili kwamba hutaki katiba mpya..
  bravo cuf
   
 7. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #7
  Dec 5, 2011
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,049
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  For all intents and purposes, CUF hawakuwa na haja kwenda ikulu kueleza msimamo wao huu; a press conference would have sufficed - wakati mwingine nashindwa kuelewa kwa nini baadhi ya vyama vya siasa vinapewa ruzuku ambayo kimsingi ni fedha ya walipa kodi ambao, unfortunately, hawana mtetezi...
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Dec 5, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hivi Lipumba yuko wapi? Mbona hasikiki?
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  Dec 5, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  It's all politics.. chuki ya CUF kwa Chadema haina kipimo na sielewi haswa sababu zaidi ya kuwaita wana wivu wa kitoto.
   
 10. T

  Topical JF-Expert Member

  #10
  Dec 5, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hivi wewe huoni chuki chadema kwa CUF??

  Nani aliyeanza kufanya vitendo vya kijinga kwa mwenzake kama siyo chadema..
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Dec 5, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Vitendo gani nikumbushe!
   
 12. T

  Topical JF-Expert Member

  #12
  Dec 5, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Chadema walishirikishwa kwenye upinzani rasmi bungeni wakati ambapo CUF ilikuwa na majority ya upinzani wao walipopata waliwatosa nje ya kambi

  Hawakuishia hapa viongozi wa chadema waliwashutumu waziwazi CUF kwamba ni CCM-B majukwaani e.g. kampeni igunga etc..

  Chadema ni agent wa kugawanya wapinzani
   
 13. M

  Molemo JF-Expert Member

  #13
  Dec 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Taleban at work
   
 14. M

  Molemo JF-Expert Member

  #14
  Dec 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  chadema hawana haja ya kushirikisha wapemba ambao kwa ujumla wa majimbo yao ni sawa na jimbo la Ubungo.
   
 15. M

  Molemo JF-Expert Member

  #15
  Dec 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  chuki ya hamad rashid na mnyaa kwa watu wa Tanzania bara haina kipimo!
   
 16. M

  Molemo JF-Expert Member

  #16
  Dec 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mkandara umesema vema.Hawa watu wana chuki mbaya sana.Katika uchunguzi wangu nimegundua hawaichukii tu chadema,bali kwa mfano chuki ya hamad rashid na mnyaa kwa watu wa Tanzania bara haina kipimo!
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Dec 5, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Alaa mkuu wangu wewe vipi? Yaani Chadema waliokuwa na CUF toka mwaka 1995 dhidi ya CCM, ghafla CUF wamejitoa na wamekuja unda urafiki na CCM, ulitaka Chadema wakae upande gani?..Maalim Seif alikuwa na kila dalili za Ushindi Zanzibar mkaungana na CCM kugawana vyeo, wewe unataka Chadema washangilie hilo. Na mlipokwenda fanya Muafaka kwa nini msiwajuze Chadema ambao ni wabia wenu..

  Mkuu wangu CUF imejiweka sehemu mbaya wenyewe kwa kudanganywa na CCM. Na niliyasema haya hapa hapa JF kabla hata muafaka haujamalizika ya kwamba CCM watahakikisha wanashika sehemu zote muhimu na wamefanya hivyo. Na kisiasa chama cha Upinzani hujenga kambi na vyama vinavyopingana na chama tawala na sio vile vilivyoshindwa viunde umoja. CUF, NCCR,TLP na vyama vingine vyote vilivyochukua nafasi chini ya pili wana takiwa kuchagua upande wanaoona unashabihiana na malengo yao.

  Hivyo, huwezi kuunda kambi moja na CUF chama kinachoshabikia sera za CCM, na hata kutumika ktk aendeleo ya Zanzibar waliko na Ubia.. Hivi tulivyo leo ndivyo inavyotakiwa kuwa. CCM na CUF kisha unakuta Chadema na NCCR picha zinakwenda na ndivyo ilivyotakiwa. Mimi naweza kusema tu NCCR walitakiwa kupewa nafasi ktk kuunda kambi ya Upinzani lakini sio CUF wala TLP kwa sababu hivi vyama vinaunga mkono sera za CCM..And that is Politics mkuu wangu.
   
 18. Mtoto Wa Mbale

  Mtoto Wa Mbale JF-Expert Member

  #18
  Dec 5, 2011
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Unajua mwaka 2005 kuwa CuF hawakufikisha 12.5% ya wabunge ili kukidhi matakwa ya kanuni za bunge juu ya kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni? Kanuni iliwalazimu kuungana na chadema ili kuunda kambi rasmi ya upinzani.

  Kabla hujatoa maoni, lawama au shutuma tafakari vizuri. Asante.
   
 19. M

  Molemo JF-Expert Member

  #19
  Dec 5, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mkuu Jasusi,Lipumba hana sauti yoyote CUF,pale yuko kama picha tu.Maamuzi yote ya CUF yanaamuliwa kule Pemba.
   
 20. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #20
  Dec 5, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Wife mwenyewe kumbe alikuwa house girl!
   
Loading...