CUF wajipanga kuibana serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF wajipanga kuibana serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Josh Michael, Oct 4, 2009.

 1. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema wanawasiliana na wanasheria wao ili kuona hatua za kuchukua baada ya kungundua kasoro nyingi katika mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa.

  Akizungumza na Mwananchi Jumapili kwa njia ya simu jana, Lipumba alisema kuwa ushauri watakaopewa watauchukua na kwamba kwa sasa hawajaamua kwenda mahakamni kuzuia uchaguzi huo.

  Alisema chama chake kimengundua kasoro nyingi katika uchaguzi huo ambazo hazitoi haki sawa kwa wagombea wao.

  Hata hivyo wakati Lipumba akisema hayo, Naibu Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa chama hicho, Shaweji Mketo amesema kesho CUF itafungua kesi mahakamani kupinga uchaguzi huo kwa madai kuwa serikali imekiuka katiba.

  Pia anadai kukiukwa kwa baadhi ya makubaliano yaliyofikiwa katika kikao baina ya Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na vyama vya siasa mwezi Februari mwaka huu mkoani Morogoro kuhusu uchaguzi huo.

  Akizungumza na waandishi jana Dar es Salaam katika makao makuu ya chama hicho, alisema pia mchezo mbaya ‘rafu’pamoja na vizuwizi vimekwisha jitokeza katika utoaji wa fomu kwa baadhi ya wagombea wa chama hicho.


  “Kwanza umekiuka maelekezo ya katiba kuhusu taratibu za uchaguzi zinazotakiwa kufuatwa, pili umekwenda kinyume na baadhi ya makubaliano tuliyokubaliana katika kikao cha Februari 19 mwaka huu kuhusu taratibu na sheria zitakazotumika kwenye uchaguzi huu.
  “Tayari mizengwe ya kujimwa fomu kwa baadhi ya wagombea wetu huko mikoani imeanza tofauti na vyama vingine ambao wanapata bila kipingamizi chochote,” alisema Mketo.

  Aidha akizungumzia suala la baadhi ya wagombea wa CUF kufanyiwa mizengwe katika uchukuaji wa fomu alisema hali hiyo imejitokeza Mbeya mjini, Singinda Vijini, Bukoba Mjini, na katika wilaya ya Bahi.
  Katika mkoa wa Mbeya alisema hadi juzi wagombea wengi walilazimika kushinda katika ofisi za maafisa watendaji bila mafanikio ya kupata fomu huku vyama vingine vikiwa vimepatiwa fomu hizo na kuonekana wakitafuta wagombea.
   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Jamani mechi ya nyani tumbili atakuwaje mwamuzi, principle za haki ya asili haziruhusu hata kidogo,( mtu kuwa mwamuzi katika kesi yake mwenyewe). Kama CCM wanashiriki kwenye uchaguzi huo hakuna jinsi uchaguzi huo unaweza kuwa fair, kwani wasimamizi, wanaotunga taratibu za uchaguzi etc ni wao wenyewe, tunategemea kitu gani hapo.
   
 3. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mimi hapa naona ni vurugu tupu hakuna cha uchaguzi but ni watu kupeana madaraka tu
   
 4. D

  Davie Member

  #4
  Oct 4, 2009
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Huo ndo ukomavu wa democracia...
   
Loading...