CUF Wajipanga kufanya uchochezi Mtwara kesho

CUF Wajipanga kufanya uchochezi Mtwara kesho

Chama cha wananchi cuf kinapanga kufanya mikutano ya hadhara kesho Mtwara kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kutoa elimu kuhusu gesi. Haya yamesema na Naibu Katibu Mkuu Bara Julius Mtatiro kwenye account yake ya facebook. Mimi naona cuf wako nyuma ya mgogoro huu wakijitafutia umaarufu baada ya kupotea kwenye siasa za Tanzania kwa muda mrefu. Cuf wamewagawa wazanzibar na watanganyika kwa kutumia uamsho sasa wanatugawa watanganyika kwa gesi asilia. Vyombo vya ulinzi vinapaswa macho.

Hayo maneno ya mwisho sijakuelewa
 
Msichoke kueneza propaganda,gesi haitoki Mtwara,gesi kwanza vyama baadae
 
Suala la gesi siyo suala la kisiasa ni suala la kitaalam zaidi. Je ni kweli kuwa wataalam wa gesi wako CUF, je ni lazima kufanya mkutano au maandamano ili kuota eleimu? hatuna njia nyingine bora ya kutoa elimu? nawashauri wana mtwara kuwa makini na wanasiasa maslahi hawa, ninaamini wanamtwara wanaelewa fika wanachokitaka na bora wakasimamia hilo kuliko propaganda za wanasiasa njaa wanaotafuta namna ya kula. Chochonde wanamtwara, ikibidi watimuweni hawa wanasiasa hawana cha maana zaidi ya vurugu tu. Walikuwa wapi siku zote kutoa elimu. Waandae warsha, au vipindi kwenye TV na radia kutoa elimu kwa umma juu ya gesi na siyo elimu kwa wanamtwara tena kwa njia ya maadamano.
 
kadiri inavozid kupotoshwa ndivo inavozid kueleweka.

Haitosaidia,ukweli utabaki kuwa ukweli tuh.
 
Kibwagizo cha uamsho huko zenj.....Zanzibar kwanza vyama baadaye


Gesi kwanza Vyama Baadae,Mtwara kwanza majungu na :blah::blah: Baadae! jitahidi sana kueneza propaganda watu tuna move on! karibu mkutano kesho uwanja wa mashujaa!
 
Kauli ya TPDC iliyotolewa na Kalaghane ni nzuri ambayo ndiyo ilitakiwa kusemwa mapema na Prof Mhongo, lakini kinyume chake yeye akatoa kauli za dharau, kejeli na kukemea. Matokeo yake ndiyo haya yanayoendelea. Hata hivyo watu wa Mtwara kauli hiyo tu bila vitendo haitawaamanisha kwa sababu ya uongo waliokwisha onyeshwa na watawala.
 
Inasikitisha sana, kusikia CUF wanajiandaa kufanya uchochezi Mtwara. NCCR Mageuzi ilikuwaje hadi mwenyekiti wake akapigwa mawe? CHADEMA hawakukubalika kwenye zoezi la kuvua gamba na kuvaa Gwanda. Inaonesha CUF inakubalika kusini. Pia naamini CUF imewaunganisha Wazanzibari ndio maana leo wanaishi kama ndugu. Msitake tuamini kuwa watu fulani ndio wanaweza na ndio wanakubalika TANZANIA nzima. Wengine wakiandamana ni haki yao, wakikatazwa wananyimwa haki yao. Naamini hata CUF wanatimiza haki yao. Naamini mtoa mada alikuwa miongozi mwa watu wale wa mwaka 1995 - 2005 kuwa CUF ni chama cha kidini. Sasa mnazimika kama mshumaa mnaanza tena kusema wachochezi. Sibirini mwaka 2015 muone mtakavyo Potea
 
Chama cha wananchi cuf kinapanga kufanya mikutano ya hadhara kesho Mtwara kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kutoa elimu kuhusu gesi. Haya yamesema na Naibu Katibu Mkuu Bara Julius Mtatiro kwenye account yake ya facebook. Mimi naona cuf wako nyuma ya mgogoro huu wakijitafutia umaarufu baada ya kupotea kwenye siasa za Tanzania kwa muda mrefu. Cuf wamewagawa wazanzibar na watanganyika kwa kutumia uamsho sasa wanatugawa watanganyika kwa gesi asilia. Vyombo vya ulinzi vinapaswa kuwa macho.

Unaweweseka, ebu kunywa maji barid tafuta sehem yenye kivuli na upepo utulie kwa dakika 30 kwanza.
 
Daah we kweli Ground Zero yani elimu unataka hiitwe uchochezi!

Nawaunga mkono cuf wakatoe elimu ya kutosha kwa wana mtwara!

Maccm bwana kila kitu wana toa lawama kwa wapinzani!
 
Last edited by a moderator:
hivi watu wa ruvuma mapoyoyo au?mbona wako kimya wakati uranium washauziwa wamarekani!!!na uranium inaacha madhara makubwa kwa wakazi jirani kuliko gesi..
Ruvuma, Mbeya, Lindi na Mtwara zijitenge kama South Sudan.
 
Huo ugonjwa wako umechanganyika na laana za wazazi siwezi kuutibu.
Nani kakwambia laana haitibiki? ukishindwa basi either wewe ni laana au umelaaniwa na unatakiwa umtembelee mzee wa upako mara moja binti. waambie wenzio waache uchochezi
 
Back
Top Bottom