Nancy Tweed tafadhali sana usitusemee watanzania na wana-JF.
Mimi, na nina uhakika wapo watu wengi, wenye kufahamu na kuamini kuwa waisilamu ni watu makini na wenye sifa zote nzuri. Ukiambiwa utoe sababu za kutowa-support nina wsiwasi kama unaweza. Si vema kutoa maneno ya kujuisha watu kwa mfano wahaya wote ni.... wachaga wote ni.... wahehe wote ni... Hayo majumuisho wote tunajua si kweli
Watanzania tumeoana waisilamu na wakristo, tunashirikiana kwenye kwenye raha na shida na juu ya yote tuna matumaini na ndoto moja ya maisha bora na Amani kwa mama TANZANIA.
Tafadhali wapeni watoto na wajukuu wetu nafasi ya kuishi kwa upendo na sio chuki