Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,329
- 33,138
Mikakati gani wameweka CUF ya kushinda ushaguzi au ni kuw washiriki wa Uchaguzi.....!!!
Mikakati gani waweke?
Tumekuwa tukijipa moyo tuna vyama vya siasa nchini, pamoja na makombora yote ya miaka mitano, lakini bado hakuna uhakika wa upinzani kuchukua urais hata miaka ijayo!
wengine tumekuwa tukipiga kelele kam wendawazimu kuwa jamani msipeane moyo na kuoneana aibu kuhusu wapizani na jinsi wanavyoongoza vyama vyao na wanavyouza sera na kujitoa kwa wananchi.
Inapofikia muda na kuwa tuna hakika wa asilimia 99% kuwa JK ndiye rais ajaye, still tunatoana damu kwa kupeana moyo kuwa tuna upinzani, nadhani tunastahili adhabu kali sana,
wanakimbilia ubunge, na still watu huko wanasema ndio strategy nzuri kwa kuanzia , kana kwamba upinzani nchi hii umeanza mwaka jana! au kana kwamba wakiwa wabunge basi mambo shwari, spika mwana CCM! yaani wapinzani wamefikia muda na kuona eti wakiwa na spika kama Sita vile basi kila kitu shwari! we IN OTHER WORDS our hope is still in some CCM members?!
If they dont change, if we will not change na ku blind followers, then we may be wasting our time. Kuna vyama tukavipa majina kama vyama mbadala!
CUF they too fall into this category, however, CUF wamekuwa wakifanya vizuri kwenye kupata kura (siyo kwenye kusema sana) kuliko vyama vingine vya upinzani kwenye chaguzi nyingi. But still nguvu zao za kuinyima usingizi CCM ni ndogo
CUF zanzibar ndiyo mfano halisi wa wapinzani wanatakiwa wawe vipi!
maoni yangu tu,
Huu uchaguzi wa 2010 wengi tulitegemea kwamba ungeleta mabadiliko mkubwa ya kisiasa nchini hasa ukitili maanani utendaji finyu wa Kikwete, mpasuko ndani ya CCM, Kikwete kushindwa kuwashughulikia mafisadi na kushindwa kutimiza ahadi hata moja kati ya ahadi zake alizozitoa 2005. Ni usanii tu ambao utaishia kumpa Kikwete ushindi wa kishindo pamoja na kuwa hastahili na pia kuwapa Wapinzani viti vya Bunge ambavyo havitafikia hata 20.
Nilikuwa naipinga sana kauli ya CCM kutawala Tanzania milele, lakini kwa huu upinzani uliopo ambao umejaa ubinafsi wa hali ya juu basi ni kweli hata CCM iboronge vipi, hata Rais aboronge vipi asilimia kubwa ya Wapiga kura watapewa tonge chache za pilau, soda, magwanda ya kijani na njano na kuimbiwa nyimbo za kifisadi na Komba kwamba CCM ni nambari one basi kuwahakikishia tena CCM ushindi wa kishindo
Inasikitisha sana lakini ndiyo ukweli wa mambo. Kama upinzani hautabadilika haraka sana na kuachana na ubinafsi wa hali ya juu na kupokea rushwa toka CCM, basi kweli CCM itatawala Tanzania milele.
bora umemalizia kwa kukiri haya ni maoni yako na ni mtazamo wako tu..very good vinginevyo nilikuwa nianze kufyatuka maana mimi CUF kindakindaki
Katika mkutano huo uliofanyika makao makuu, Buguruni, jijini Dar es Salaam, Mketo pia alisema wamefikia uamuzi huo ili kukata kiu ya wananchi wengi waliokuwa wakitaka kujua iwapo CUF itasimamisha mgombea urais katika uchaguzi huo.
Jambo la muhimu, ambalo tungependa wananchi wajue ni kwamba, CUF imedhamiria kushinda uchaguzi huu na kwamba wengi wamekuwa wakihoji iwapo tutaweka mgombea urais au la.
Kwa kinywa kipana kabisa CUF itaweka mgombea wa urais na ndiye atakayekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2010-2015, alisema Shaweji na kuongeza:
CHANZO: NIPASHE