CUF: Tutasimamisha mgombea urais

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,266
33,039
headline_bullet.jpg
Yatangaza ratiba ya kura ya maoni

Lipumba1%289%29.jpg

Profesa Ibrahim Lipumba

Chama cha Wananchi (CUF), kimetangaza kwamba kitasimamisha mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Naibu Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa chama hicho, Shaweji Mketo, katika mkutano na waandishi wa habari ambao aliutumia kutangaza kuanza rasmi mchakato wa kushiriki Uchaguzi Mkuu.

Katika kujipanga kuelekea uchaguzi huo, CUF imetoa ratiba ya kura za maoni ya kuwapata wagombea wa udiwani, ubunge wa majimbo, ubunge viti maalum na urais katika uchaguzi huo kwa upande wa Tanzania Bara na kutangaza tarehe ya kuchukua na kurejesha fomu kwa wanachama wanaotaka kugombea urais kuwa ni Mei 1-5, mwaka huu.

Kwa kauli hiyo sasa CUF itakuwa imesimamisha mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano kwa mara ya nne mfululizo; wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995, 2000 na 2005, chama hicho kilimsimamisha Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba kuwania nafasi hiyo.

Hata hivyo, Profesa Lipumba mara zote hizo amekuwa akishindwa na wagombea wanaosimamishwa na CCM, kuanzia Rais Mstaafu Benjamin Mkapa mwaka 1995 na 2000, kisha Rais Jakaya Kikwete mwaka 2005.

Katika mkutano huo uliofanyika makao makuu, Buguruni, jijini Dar es Salaam, Mketo pia alisema wamefikia uamuzi huo ili kukata kiu ya wananchi wengi waliokuwa wakitaka kujua iwapo CUF itasimamisha mgombea urais katika uchaguzi huo.

“Jambo la muhimu, ambalo tungependa wananchi wajue ni kwamba, CUF imedhamiria kushinda uchaguzi huu na kwamba wengi wamekuwa wakihoji iwapo tutaweka mgombea urais au la.

Kwa kinywa kipana kabisa CUF itaweka mgombea wa urais na ndiye atakayekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2010-2015,” alisema Shaweji na kuongeza:

“Haiwezekani katika kipindi ambacho nchi imekumbwa na ombwe la uongozi, hali ya maisha ya Watanzania imezidi kuwa mbaya, uchumi wa taifa umezidi kudidimia, migawanyiko katika jamii inaongezeka kwa kasi ya kutisha ambayo inatokana na serikali kushindwa kuwajibika, kutoweka kwa maadili ya taifa na hata kufutika kwa utu wa watu, jamii iendelee kukikumbatia Chama Cha Mapinduzi.”

Aliwataka wanachama wa CUF wenye sifa za kugombea wajitokeze kwa wingi kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya chama kuwania uongozi katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu.

Pia, aliwaomba Watanzania kujiandaa kuchagua viongozi makini watakaotetea maslahi ya taifa.
Kwa mujibu wa ratiba ya kura za maoni, wanachama wanaotaka kugombea urais wametakiwa kuchukua na kurejesha fomu hizo kwa makatibu wa wilaya, ambapo Mei 6 -10 fomu za wagombea urais zitafikishwa kwa Katibu Mkuu.

Shaweji alisema fomu za kugombea udiwani na ubunge (ikiwamo viti maalum) zilizoanza kuchukuliwa Februari 23, zimetakiwa ziwe zimerejeshwa kwa makatibu wa tawi ifikapo Aprili 13, mwaka huu.

Alisema Aprili 14 - 20, itakuwa ni kipindi cha kurejesha fomu za wagombea udiwani na ubunge (ikiwamo viti maalum) kwa makatibu wilaya, wakati Aprili 27 - Mei 6 itakuwa ni kipindi cha mikutano ya wilaya ya kura za maoni kwa wagombea udiwani na viti maalum.

Mei 13 - 20 matokeo ya kura za maoni kwa wagombea ubunge na viti maalum kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu, wakati Mei 29 - 30 Baraza Kuu la Uongozi la Taifa litafanya uteuzi wa mwisho kwa wagombea ubunge.

Alisema Juni 2, Mkutano Mkuu wa Taifa wa kura za maoni kwa wagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na urais Zanzibar na Juni 3 maandalizi ya kampeni.

CHANZO: NIPASHE
 
Mikakati gani wameweka CUF ya kushinda ushaguzi au ni kuw washiriki wa Uchaguzi.....!!!
 
Mikakati gani wameweka CUF ya kushinda ushaguzi au ni kuw washiriki wa Uchaguzi.....!!!

Mikakati gani waweke?

Tumekuwa tukijipa moyo tuna vyama vya siasa nchini, pamoja na makombora yote ya miaka mitano, lakini bado hakuna uhakika wa upinzani kuchukua urais hata miaka ijayo!

wengine tumekuwa tukipiga kelele kam wendawazimu kuwa jamani msipeane moyo na kuoneana aibu kuhusu wapizani na jinsi wanavyoongoza vyama vyao na wanavyouza sera na kujitoa kwa wananchi.

Inapofikia muda na kuwa tuna hakika wa asilimia 99% kuwa JK ndiye rais ajaye, still tunatoana damu kwa kupeana moyo kuwa tuna upinzani, nadhani tunastahili adhabu kali sana,

wanakimbilia ubunge, na still watu huko wanasema ndio strategy nzuri kwa kuanzia , kana kwamba upinzani nchi hii umeanza mwaka jana! au kana kwamba wakiwa wabunge basi mambo shwari, spika mwana CCM! yaani wapinzani wamefikia muda na kuona eti wakiwa na spika kama Sita vile basi kila kitu shwari! we IN OTHER WORDS our hope is still in some CCM members?!

If they dont change, if we will not change na ku blind followers, then we may be wasting our time. Kuna vyama tukavipa majina kama vyama mbadala!

CUF they too fall into this category, however, CUF wamekuwa wakifanya vizuri kwenye kupata kura (siyo kwenye kusema sana) kuliko vyama vingine vya upinzani kwenye chaguzi nyingi. But still nguvu zao za kuinyima usingizi CCM ni ndogo

CUF zanzibar ndiyo mfano halisi wa wapinzani wanatakiwa wawe vipi!

maoni yangu tu,
 
bora umemalizia kwa kukiri haya ni maoni yako na ni mtazamo wako tu..very good vinginevyo nilikuwa nianze kufyatuka maana mimi CUF kindakindaki
 
Huu uchaguzi wa 2010 wengi tulitegemea kwamba ungeleta mabadiliko mkubwa ya kisiasa nchini hasa ukitili maanani utendaji finyu wa Kikwete, mpasuko ndani ya CCM, Kikwete kushindwa kuwashughulikia mafisadi na kushindwa kutimiza ahadi hata moja kati ya ahadi zake alizozitoa 2005. Ni usanii tu ambao utaishia kumpa Kikwete ushindi wa kishindo pamoja na kuwa hastahili na pia kuwapa Wapinzani viti vya Bunge ambavyo havitafikia hata 20.

Nilikuwa naipinga sana kauli ya CCM kutawala Tanzania milele, lakini kwa huu upinzani uliopo ambao umejaa ubinafsi wa hali ya juu basi ni kweli hata CCM iboronge vipi, hata Rais aboronge vipi asilimia kubwa ya Wapiga kura watapewa tonge chache za pilau, soda, magwanda ya kijani na njano na kuimbiwa nyimbo za kifisadi na Komba kwamba CCM ni nambari one basi kuwahakikishia tena CCM ushindi wa kishindo

Inasikitisha sana lakini ndiyo ukweli wa mambo. Kama upinzani hautabadilika haraka sana na kuachana na ubinafsi wa hali ya juu na kupokea rushwa toka CCM, basi kweli CCM itatawala Tanzania milele.
 
Asante kaka kwa kuweka wazi kila kitu, tumekuwa na tabia ya kujipa moyo na mpaka makamanda wetu tukawapa majina ya chama mbadala, I adore Chadema, lakini how? nipende tu hata sehemu ninayojua sitapata changes zozote? maana kwa Tanzania bara , tukisema chama haraka tunakumbuka chadema, hao wengine wanapumulia mashine. Kama chama mbadala hakitaweza kusimamisha mtu, naam, hata kikisimamisha tunaona dhahiri kwa macho mawili hakuna dalili ya ushindi tumekosea wapi? tusipoweza kutafuta ukweli wa matatizo ya hivi vyama na sisi raia, basi tujue tutawasindikiza hawa jamaa mpaka kizazi cha tatu na cha nne cha Ridhiwan Kikwete!

Nilimejaribu kuuliza na mpaka kutuma personal e-mail kwa baadhi ya wanachadema kuhusu sera ya nyumba tano tano, sera hii ilikuwa superb na hakuna anayenijibu! maana kuindoa CCM ni strategy, sera ya nyumba tano tano ilikuwa kama vile unawasha moto wa chini chini, siku ukitaka ulipuke, ni kumwagia mafuta kidogo tu!

wananchi wamekosa nguvu, utaona hata turn up ya watu kupiga kura itakuwa ndogosana na watakojitokeza wana CCM walioshiba pilau, wakipiga kura wanampa JK, percentage ikiwekwa JK ataonekana ana asilimia 95%!

Ikifikia state katika uchaguzi wowote kuwa haileweki rais atatoka CCM au Chadema au CuF watu hujitokeza sana kupiga kura!

BAK, kazi tunayo, naona kabisa kama vile RA na EL wananizomea! hilooo, hilooo!
 
bora umemalizia kwa kukiri haya ni maoni yako na ni mtazamo wako tu..very good vinginevyo nilikuwa nianze kufyatuka maana mimi CUF kindakindaki

Kigogo hata kama wewe ni CUF ki-ndakindaki au ngangali...tunachotaka kujua wana JF ni mikakati gani mnayo kuweza shinda uchaguzi...!!! kama after 15yrs ya kuruhusiwa Vyama vingi, bado baadhi ya maeneo mnakosa watu wa kugombea, maana yake bado real upinzani haujajengwa...!!!! Mfano mzuri tulikuwa wa Senegal, namna Mzee Wade alivyoweza shinda after more than 20yrs ya kushiriki uchaguzi..!! lkn Hatujaamua kwenda kujifunza kwake!!!

Wapinzani wameshindwa kuungana, najua wanapenda kuungana lkn kuna external forces ambazo zimewafanya wasiungane. Inawezekana wanazijua na inawezekana hawazijui....Wangeweze kukubaliana kutofautiana ktk yale ambayo hawakubaliani, na yale wanayokubaliana, basi wakaekeana terms za kukubaliana.

Kila Team ina potentialities zake...na kila team ina weakness zake, Wangeweza kukusanya potentialities za kila mmoja, ambazo zinge-overcome weakness zao...!!!
We wish you all the best!!!
 
Kuna wa-TZ wengi tu hawatopiga kura, chukulia wa-tz waliopo NJE ya nchi ambao kwa nature za kazi hawatoweza kuja kushiriki kupiga kura.

Wenzetu IRAQ pamoja na un-stability ya nchi, bado wameweza kuandaa mazingira ya waliopo nje ya nchi yao kushiriki. Najua nchi zilizoendelea nazo zinafanya hivyo,Even India, Je CUF ambao wana-taraji kusimamisha Mgombea imeandaa mazingira gani ya wana-nchi waliopo Nje ya TZ kushiriki uchaguzi. CCM may wanaogopa hilo, pamoja na kuwa matawi UK na US, kwakuwa wa-tz hawapo happy kuona step ya maendeleo nchi yao ilipofikia...!!!

CUF mmefanya mikutano mingapi Vyuoni(Vyuo Vikuu) ambapo wasomi wetu ni sehem u ya chachu ya mageuzi...Hii ni ktk Potentialities za Zitto, kwani amekuwa akipita vyuoni akinadi Chadema au kuzungumzia national Issues...!!!

Ikiwa CCM wanawapa Kadi au wanawahubiria SIASA wanafunzi wa Sekondari, CUF kama mmejiandaa kushinda uchaguzi, ni wapi mmefanya alau kuwakusanya wanafunzi wa Namna Hio kuwa Ujumbe, ambao wanaweza kuwafikishia Wazazi wao, au wengine in next 5yrs wanaweza kuwa wapiga kura wa maana....!!!

Ktk Kundi muhim ktk Nchi hii ni WAALIM wa primary na Sekondar ambao kama mngewatumia vyema wangeweza kuleta mageuzi ya kweli. kwa Kero wanazofanyiwa na Serikali, nyinyi kama mmejiandaa na Urais...mmeshawahi kukutana na Chama cha waalim na Kuzungumza nao?..Ok Mnaweza msikutane nao, lkn hata kuwa karibisha na kula nao Lunch au Dinner just kuwaambia sisi tunajua matatizo yenu...na alau kuwa Mipango kuwa Mkipewa Madaraka, nini mtawafanyia na Kuboresha Mazingira ya Elimu Nchini?

Vyama vya Wafanyakazi... CUF kama mmejiandaa ni lini au mnamkakati gani wa kukutana alau na Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi. Najua wapo wengine ni CCM, lkn still kukaa nao na Kuzungumza nao Issues. Ikumbukwe kuwa Vyama vya wafanyakazi ndivyo vilivyokuwa chachu ya Mageuzi au Vuguvugu la Kumuondoa MKOLONI Tanzania na kwingineko.
 
Katika mkutano huo uliofanyika makao makuu, Buguruni, jijini Dar es Salaam, Mketo pia alisema wamefikia uamuzi huo ili kukata kiu ya wananchi wengi waliokuwa wakitaka kujua iwapo CUF itasimamisha mgombea urais katika uchaguzi huo.
“Jambo la muhimu, ambalo tungependa wananchi wajue ni kwamba, CUF imedhamiria kushinda uchaguzi huu na kwamba wengi wamekuwa wakihoji iwapo tutaweka mgombea urais au la.
Kwa kinywa kipana kabisa CUF itaweka mgombea wa urais na ndiye atakayekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2010-2015,” alisema Shaweji na kuongeza:
CHANZO: NIPASHE

"Kuwa na akili ni pamoja na kufahamu jambo unaloliweza na lile usiloliweza" Mwl JK Nyerere
 
CUF wana akili ndio maana wameamua kuweka mgombea urais kwa kuwa wanaamini kwamba wanaweza kuongoza nchi na hasa kwa kuzingatia changamoto nyingi ambazo rais Kikwete ameshindwa kuzishughurikia Ufisadi, ukosefu wa ajira {ondoa za kuokota chupa}kupanda kwa gharama za maisha kwa kutaja machache.anaeitetea CCM na serikari yake kuna masrahi binafsi.HONGERA CUF wananchi wako nyuma yenu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom