CUF: Tunasikitishwa na muendelezo wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nchini, hususan Uhuru wa kujieleza, Uhuru wa kupata na kutoa habari

CUF Habari

JF-Expert Member
Dec 12, 2019
239
234
IMG_20200702_154300_496.jpg

"Baraza Kuu kwa Mara nyingine limesikitishwa na muendelezo wa ukiukwaji mkubwa wa Haki za Binadamu nchini, hususan Uhuru wa kujieleza, Uhuru wa kukusanyika, kupata na kutoa habari.

Hivyo Basi linaitaka Serikali kuheshimu katiba ya nchi. Chama Cha CUF kikipata ridhaa ya watanzania kuongoza nchini Oktoba 2020 kitaziondoa Sheria zote kandamizi au vifungu kandamizi katika Sheria mbalimbali, mfano sheria ya makosa ya kimtandao (Cyber Crime Act),Sheria ya vyombo vya habari (Media Law)Pamoja na Sheria ya Vyama vya Siasa (Political Parties Act) pamoja na Sheria ya vyama vya Siasa (Political Parties Act) ya 2019.

#MkutanoNaWanahabariLeo.
 
Huyu mzee bana ni hatari kwa kupiga mizinga kijanja - anajua kula na vipofu aisee!

Bbaada ya leo kutamka hivi, hapo tu kesho utamsikia kaenda Magogoni kuonana na mfadhili wake na kuibuka na statement "mtukufu amenihakikishia kuwa kutakuwa na uhuru wa kujieleza, haki ya kukusanyika na kuondolewa kwa sheria kandamizi".

Njaa ni mbaya usipime!
 
Acheni maigizo, nyie mmetumika muda wote kujipendekeza kwa hao wanaokandamiza demokrasia, saa hii wanawatumia ili muonekane wapinzani. Kibaya zaidi huko Zanzibar mmepoteza mvuto, ccm wamelijua hilo mpaka wamehamishia hongo kwa NCCR.
 
Umeelweka vizuri hasa sheria ya vyama vya siasa, uviondoe kama ulivyoiondoa CUF.
 
Acheni kujikomba kwetu nyinyi wachumia tumbo mliofika bei kwani ukandamizaji ulianzia leo..?
 
Back
Top Bottom