Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,280
- 25,859
Uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Dimani huko Zanzibar una mafunzo mengi. Moja ya mafunzo yanayotolewa ni kwamba Wazanzanibari bado ni wamoja na wanaendesha mambo yao pamoja na kwa amani.
Kampeni za Ubunge Jimboni Dimani zinaendelea kwa amani na utulivu. Funzo lingine ni kuwa CUF iko imara mikononi mwa Maalim Seif Sharrif Hamad. Kuanzia Dimani Zanzibar hadi kwenye kata zenye uchaguzi mdogo Tanzania Bara, Maalim Seif anarindima.
Jimboni Dimani, ni kipimo tosha ya nguvu ya Maalim Seif dhidi ya 'Mwenyekiti' Lipumba. Maalim na CUF yake wamefanikiwa kupitisha mgombea wao na wanaendelea kumnadi. 'Mwenyekiti' Lipumba na timu yake wameshindwa kusimamisha mchakato wa kumpata mgombea.
Kimsingi, CUF iko chini ya Maalim Seif Sharrif Hamad na timu yake. 'Mwenyekiti' Lipumba hana athari wala nguvu yoyote chamani humo. Ameshiwa na hana chake ndani ya CUF. 'Mwenyekiti' Lipumba anapaswa kujisalimisha kwa Maalim Seif na si vinginevyo.