CUF, NCCR wajipakaza uozo wa CCM

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
CUF, NCCR wajipakaza uoza wa CCM

Na Mwandishi wetu

KAMA viongozi wa NCCR-Mageuzi, Chama cha Wananchi (CUF), Tanzania Labour Party (TLP) na United Democratic Party (UDP) wangekaa chini na kupima sababu za kuporomoka kisiasa kwa Mchungaji Christopher Mtikila wa DP, wasingekubali mwaliko wa ikulu kunywa sifongo.

Prof. Ibrahim Lipumba (CUF), James Mbatia (NCCR-Mageuzi), Augustine Mrema (TLP), na John Cheyo (UDP) wametia saini kujimaliza kisiasa wao na vyama vyao ili kunusuru hadhi ya Rais Jakaya Kikwete pamoja na chama chake – Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Taratibu wameamua kufuata nyayo za Mtikila kuporomoka wao na vyama vyao.

Katika miaka ya mwanzoni mwa 1990, mara baada ya mfumo wa vyama vingi kuruhusiwa, Mtikila alikuwa miongoni mwa wanasiasa waliotikisa nchi na kuvutia wananchi.

Mwaka 1993 alitinga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na kuwasha moto wa mageuzi nchini. Alipotaka kuanza kuhutubia kwa Kiswahili wanafunzi wakamwambia "English please."

Mtikila alitii agizo hilo na alipomaliza "kumwaga sumu" akajikuta mamia ya wanachuo wamemzunguka kwenye gari lake na kuanza kulisukuma. Walikuwa wanamfurahia.

Siku nyingine akiwa katika viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam, Mtikila alitoa hotuba iliyohamasisha mamia ya watu kwenda kuvunja vioo vya magari ya watu aliowaita ‘ma*********' yaani matajiri wa Kiasia.

Kila mahali alipokwenda kuhutubia alifuatwa na maelfu ya watu kumsikiliza na kujiunga na chama chake. Mtikila wa leo si wa miaka ya 1990; amebaki yeye na wanachama wake kiduchu sana.

Mambo kadhaa makubwa yalichangia kuporomoka na kumaliza umaarufu wake.

Kwanza ni nguvu ya upepo wa mageuzi aliyoingia nayo Mrema kutoka CCM na kuibukia NCCR.

Mrema aliyejitoa CCM kupinga hatua ya serikali kuratibu wizi wa mamilioni ya shilingi yaliyotengwa kwa ajili ya uendelezaji mashamba ya mkonge; alikuwa kivutio kikubwa.

Alizunguka nchi nzima kuishtaki serikali ya CCM kwa wananchi, kwamba imeshindwa kuwaletea watu maisha bora.

Pili, ili kurejesha mvuto wake, katika kipindi ambacho NCCR ilikuwa madhubuti na kutishia mustakbali wa CCM kuunda tena serikali, Mtikila akajiingiza katika mradi mchafu wa kuisaidia CCM kumponda Mrema na NCCR yake.

Mtikila alikerwa na umaarufu wa Mrema kuliko ufisadi wa serikali iliyopo.

Mtikila ameendelea na mradi huo hadi katika miaka ya hivi karibuni. Mfano katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimboni Tarime, alijitokeza kuwaponda wapinzani wenzake hadi akapigwa jiwe.

Tatu, Mtikila amejitokeza kuwa mtu aliyepoteza dira. Anachokipinga hadharani ndicho anakifanya kwa siri. Mathalani amekuwa akiwaponda mafisadi mchana, lakini usiku anapokea misaada ya fedha kutoka kwao. Wengi ameridhiana nao na kunyamaza.

Ugonjwa huu uliomkumba Mtikila hadi kupotea katika siasa za mageuzi ndio unawanyemelea kwa kasi Mbatia, Mrema, Cheyo na katika hali ya kushangaza Prof. Lipumba.

Viongozi hawa wote wanajua ‘rafu' za CCM; wanajua jinsi serikali ya CCM inavyotumia wapinzani kupunguza au kuzima kasi ya upinzani kwa kuchonganisha vyama, kuvilipa fedha, kutumia polisi kutwanga virungu vyama machachari na kuzushia udini, ukabila, fitina na chuki.

Viongozi hawa wanajua jinsi Mrema alivyoshuka daraja alipofuata nyayo za Mtikila kuponda vyama vingine vya upinzani. Baada ya kukataa kuungana na vyama vingine mwaka 1995, Mrema ‘aliugua ugonjwa' wa kuwaponda wapinzani huku akijitukuza yeye tu. Mrema hakusalimika, katika uchaguzi wa mwaka 2000 akiwa amehamia TLP, akaporomoka.

Vilvile viongozi hawa wanajua polisi, usalama wa taifa walivyotumika kumvuruga Mrema hadi akakimbia NCCR na kuhamia TLP ambako uliibuka mgogoro mwingine usio kichwa wala miguu uliomtoa mwasisi wake, Leo Lekwama aliyejipatia umaarufu kwa kusigina katiba katika viwanja vya Jangwani. Hatimaye Lekwama kwa kuchoshwa na visa vya Mrema, akaamua kurejea CCM.

Naye Cheyo anajua umafia wa CCM ulivyomkosesha kura hata katika kituo alichopigia; akaambulia kura yake, mkewe na ndugu zake wawili.

Prof. Lipumba, msomi aliyekubalika zaidi uchaguzi wa mwaka 2000 na 2005, yeye na chama chake, muda wote wamewaaminisha wananchi kwamba kura zao katika uchaguzi wa 2005 ziliibwa kwa teknolojia ya kisasa.

Kwamba watu wakimpigia kura Profesa Lipumba wino ulikuwa unafutika katika karatasi zile za kura kutoka Afrika Kusini.

Katika kampeni mwaka jana alijibainisha kuwa ni Mlima Kilimanjaro huku mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa akimwita kichuguu.

Baada ya uchaguzi, Profesa akaungana rasmi na kina Mrema, Cheyo na Mbatia kushambulia CHADEMA eti kina mikakati ya kuvunja amani ya nchi.

Hao wote wanaimba wimbo "heri shetani umjuaye CCM kuliko CHADEMA usiyemjua." Kama CCM hawako salama, wamepoteza umaarufu, kitu gani kimewavutia Mrema, Mbatia, Cheyo, Profesa kuingia katika jahazi linalozama?

Viongozi wa vyama hivyo wanaweza kujibu hoja hizi kwa mstari mmoja tu au wakapuuza, lakini ukweli historia itawahukumu.

Maana hawawezi kushirikiana na adui yao CCM na wakabaki wanaaminiwa na wananchi kuwa ni wapinzani makini wenye nia ya kuingia ikulu.

Maana wote; Mrema, Cheyo, Mbatia na Profesa wamenyanyua bango linalosomeka ‘On ne change pas l'equipe qui gangne' yaani Hakuna Kubadili Timu ya Ushindi (CCM).'

Mrema anajua CCM wanavyotapatapa wakibanwa vilivyo na njia wanayotumia ni uzushi. Alidaiwa kuchota mamilioni ya shilingi alipoondoka serikalini; alidaiwa kuendesha siasa za ukabila; baadaye akaambiwa ana udini. Leo ameungana na wazushi CCM wanaotapatapa kuzushia CHADEMA kuwa kinataka kuvunja amani.

Profesa anakumbuka CCM ilivyomtumia Balozi wa Marekani, Charles Stith hadi kuanza kutoa taarifa za tishio la ugaidi katika visiwa vya Unguja na Pemba; haukuonekana.

Mwaka 2001 wakati anaaga Balozi Stiith alifafanua kile alichoita ugaidi akisema siasa kali hazitasaidia Zanzibar kutatua matatizo yake ya kiuchumi. Profesa ndiye alikuwa wa kwanza kumjibu Balozi Stith kwamba ni mzushi.

Lipumba ambaye alifikia kuvunjwa mkono na Polisi wa CCM wakati wa kampeni za uchaguzi, anajua uzushi ule ulivyochangia kuiathiri CUF kwamba ni cha kidini na kimejaa Wapemba. Hoja hizo zilitumiwa tena na Fatma Maghimbi alipojiondoa na kurudi CCM.

Lipumba bado anakumbuka jinsi CCM ilivyomtumia aliyekuwa mkuu wa jeshi la polisi, Omari Mahita kuangamiza chama chake kwa kukizushia kuwa kimeleta majambia wakati haikuwa kweli.

Hivyo basi, kama Mtikila aliporomoka kwa kunanga wapinzani wenzake, Mrema akakanyaga kaa la moto alipojiona bora kuliko wapinzani wengine, Mbatia na Prof. Lipumba hawawezi kupata umaarufu kwa kuwachafua wapinzani wenzao. Hapana shaka wataporomoka tu maana historia ina tabia ya kujirudia.

0658 383 979, 0776 383 979

Chanzo: MwanaHalisi toleo Na. 234
 
Profesa was my hero in 2000 and also 2005 elections. Lakini sasa hivi nashindwa kumuelwa kabisa -- yaani kanichomoka ile mbaya. Halafu ni Profesa -- afadhali hao wengine wenye elimu za mpakazo -- Mbatia et al.

Inasikitisha sana!!!! He's going to pay a very big price in 2015 -- that I can assure him.
 
CUF, NCCR wajipakaza uoza wa CCM

Na Mwandishi wetu

KAMA viongozi wa NCCR-Mageuzi, Chama cha Wananchi (CUF), Tanzania Labour Party (TLP) na United Democratic Party (UDP) wangekaa chini na kupima sababu za kuporomoka kisiasa kwa Mchungaji Christopher Mtikila wa DP, wasingekubali mwaliko wa ikulu kunywa sifongo.

Prof. Ibrahim Lipumba (CUF), James Mbatia (NCCR-Mageuzi), Augustine Mrema (TLP), na John Cheyo (UDP) wametia saini kujimaliza kisiasa wao na vyama vyao ili kunusuru hadhi ya Rais Jakaya Kikwete pamoja na chama chake  Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Taratibu wameamua kufuata nyayo za Mtikila kuporomoka wao na vyama vyao.

Katika miaka ya mwanzoni mwa 1990, mara baada ya mfumo wa vyama vingi kuruhusiwa, Mtikila alikuwa miongoni mwa wanasiasa waliotikisa nchi na kuvutia wananchi.

Mwaka 1993 alitinga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na kuwasha moto wa mageuzi nchini. Alipotaka kuanza kuhutubia kwa Kiswahili wanafunzi wakamwambia English please.

Mtikila alitii agizo hilo na alipomaliza kumwaga sumu akajikuta mamia ya wanachuo wamemzunguka kwenye gari lake na kuanza kulisukuma. Walikuwa wanamfurahia.

Siku nyingine akiwa katika viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam, Mtikila alitoa hotuba iliyohamasisha mamia ya watu kwenda kuvunja vioo vya magari ya watu aliowaita ma********* yaani matajiri wa Kiasia.

Kila mahali alipokwenda kuhutubia alifuatwa na maelfu ya watu kumsikiliza na kujiunga na chama chake. Mtikila wa leo si wa miaka ya 1990; amebaki yeye na wanachama wake kiduchu sana.

Mambo kadhaa makubwa yalichangia kuporomoka na kumaliza umaarufu wake.

Kwanza ni nguvu ya upepo wa mageuzi aliyoingia nayo Mrema kutoka CCM na kuibukia NCCR.

Mrema aliyejitoa CCM kupinga hatua ya serikali kuratibu wizi wa mamilioni ya shilingi yaliyotengwa kwa ajili ya uendelezaji mashamba ya mkonge; alikuwa kivutio kikubwa.

Alizunguka nchi nzima kuishtaki serikali ya CCM kwa wananchi, kwamba imeshindwa kuwaletea watu maisha bora.

Pili, ili kurejesha mvuto wake, katika kipindi ambacho NCCR ilikuwa madhubuti na kutishia mustakbali wa CCM kuunda tena serikali, Mtikila akajiingiza katika mradi mchafu wa kuisaidia CCM kumponda Mrema na NCCR yake.

Mtikila alikerwa na umaarufu wa Mrema kuliko ufisadi wa serikali iliyopo.

Mtikila ameendelea na mradi huo hadi katika miaka ya hivi karibuni. Mfano katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimboni Tarime, alijitokeza kuwaponda wapinzani wenzake hadi akapigwa jiwe.

Tatu, Mtikila amejitokeza kuwa mtu aliyepoteza dira. Anachokipinga hadharani ndicho anakifanya kwa siri. Mathalani amekuwa akiwaponda mafisadi mchana, lakini usiku anapokea misaada ya fedha kutoka kwao. Wengi ameridhiana nao na kunyamaza.

Ugonjwa huu uliomkumba Mtikila hadi kupotea katika siasa za mageuzi ndio unawanyemelea kwa kasi Mbatia, Mrema, Cheyo na katika hali ya kushangaza Prof. Lipumba.

Viongozi hawa wote wanajua rafu za CCM; wanajua jinsi serikali ya CCM inavyotumia wapinzani kupunguza au kuzima kasi ya upinzani kwa kuchonganisha vyama, kuvilipa fedha, kutumia polisi kutwanga virungu vyama machachari na kuzushia udini, ukabila, fitina na chuki.

Viongozi hawa wanajua jinsi Mrema alivyoshuka daraja alipofuata nyayo za Mtikila kuponda vyama vingine vya upinzani. Baada ya kukataa kuungana na vyama vingine mwaka 1995, Mrema aliugua ugonjwa wa kuwaponda wapinzani huku akijitukuza yeye tu. Mrema hakusalimika, katika uchaguzi wa mwaka 2000 akiwa amehamia TLP, akaporomoka.

Vilvile viongozi hawa wanajua polisi, usalama wa taifa walivyotumika kumvuruga Mrema hadi akakimbia NCCR na kuhamia TLP ambako uliibuka mgogoro mwingine usio kichwa wala miguu uliomtoa mwasisi wake, Leo Lekwama aliyejipatia umaarufu kwa kusigina katiba katika viwanja vya Jangwani. Hatimaye Lekwama kwa kuchoshwa na visa vya Mrema, akaamua kurejea CCM.

Naye Cheyo anajua umafia wa CCM ulivyomkosesha kura hata katika kituo alichopigia; akaambulia kura yake, mkewe na ndugu zake wawili.

Prof. Lipumba, msomi aliyekubalika zaidi uchaguzi wa mwaka 2000 na 2005, yeye na chama chake, muda wote wamewaaminisha wananchi kwamba kura zao katika uchaguzi wa 2005 ziliibwa kwa teknolojia ya kisasa.

Kwamba watu wakimpigia kura Profesa Lipumba wino ulikuwa unafutika katika karatasi zile za kura kutoka Afrika Kusini.

Katika kampeni mwaka jana alijibainisha kuwa ni Mlima Kilimanjaro huku mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa akimwita kichuguu.

Baada ya uchaguzi, Profesa akaungana rasmi na kina Mrema, Cheyo na Mbatia kushambulia CHADEMA eti kina mikakati ya kuvunja amani ya nchi.

Hao wote wanaimba wimbo heri shetani umjuaye CCM kuliko CHADEMA usiyemjua. Kama CCM hawako salama, wamepoteza umaarufu, kitu gani kimewavutia Mrema, Mbatia, Cheyo, Profesa kuingia katika jahazi linalozama?

Viongozi wa vyama hivyo wanaweza kujibu hoja hizi kwa mstari mmoja tu au wakapuuza, lakini ukweli historia itawahukumu.

Maana hawawezi kushirikiana na adui yao CCM na wakabaki wanaaminiwa na wananchi kuwa ni wapinzani makini wenye nia ya kuingia ikulu.

Maana wote; Mrema, Cheyo, Mbatia na Profesa wamenyanyua bango linalosomeka On ne change pas lequipe qui gangne yaani Hakuna Kubadili Timu ya Ushindi (CCM).

Mrema anajua CCM wanavyotapatapa wakibanwa vilivyo na njia wanayotumia ni uzushi. Alidaiwa kuchota mamilioni ya shilingi alipoondoka serikalini; alidaiwa kuendesha siasa za ukabila; baadaye akaambiwa ana udini. Leo ameungana na wazushi CCM wanaotapatapa kuzushia CHADEMA kuwa kinataka kuvunja amani.

Profesa anakumbuka CCM ilivyomtumia Balozi wa Marekani, Charles Stith hadi kuanza kutoa taarifa za tishio la ugaidi katika visiwa vya Unguja na Pemba; haukuonekana.

Mwaka 2001 wakati anaaga Balozi Stiith alifafanua kile alichoita ugaidi akisema siasa kali hazitasaidia Zanzibar kutatua matatizo yake ya kiuchumi. Profesa ndiye alikuwa wa kwanza kumjibu Balozi Stith kwamba ni mzushi.

Lipumba ambaye alifikia kuvunjwa mkono na Polisi wa CCM wakati wa kampeni za uchaguzi, anajua uzushi ule ulivyochangia kuiathiri CUF kwamba ni cha kidini na kimejaa Wapemba. Hoja hizo zilitumiwa tena na Fatma Maghimbi alipojiondoa na kurudi CCM.

Lipumba bado anakumbuka jinsi CCM ilivyomtumia aliyekuwa mkuu wa jeshi la polisi, Omari Mahita kuangamiza chama chake kwa kukizushia kuwa kimeleta majambia wakati haikuwa kweli.

Hivyo basi, kama Mtikila aliporomoka kwa kunanga wapinzani wenzake, Mrema akakanyaga kaa la moto alipojiona bora kuliko wapinzani wengine, Mbatia na Prof. Lipumba hawawezi kupata umaarufu kwa kuwachafua wapinzani wenzao. Hapana shaka wataporomoka tu maana historia ina tabia ya kujirudia.

0658 383 979, 0776 383 979

Chanzo: Mwananchi toleo Na. 234
The best article ever!
 
Hivi kuna mwenye fununu hawa jamaa wamenunuliwa kwa bei gani?
Bado nafikiria na kumshangaa huyu profesa.
 
be care IBRAHIM, huu ni utafiti wa siasa za tanzania, ukijali fanyia kazi ukipuuza tupa katika ndoo ya taka.
 
Wanajamvi:

Kunradhini -- chanzo ni gazeti la MwanaHalisi -- siyo Mwananchi. Nimerekebisha.
 
Hivi kuna mwenye fununu hawa jamaa wamenunuliwa kwa bei gani?
Bado nafikiria na kumshangaa huyu profesa.

Ni 100 % wamenunuliwa. Nasema hivi kwa sababu CCM imepoteza mvuto kwa wananchi kwa hivyo sasa wanatumia pesa ambazo wanazipata kwa njia ya kifisadi kuwahonga wa kuwapigia debe.

Juzi niliona katika TV Chpaka wa TADEA na Kyara wa SAU wakiipigia debe serikali ya CCM na kuwaomba nao wapate ruzuku huku wakiwaponda CDM kwa kutaka kuvunja amani ya nchi. Huyo Chipaka alihusika katika njama za kupindua serikali ya Mwalumu Nyerere na akahukumiwa kufungwa. Bila shaka alikuwa tayari mwagi imwagiuke kwa tamaa zake za madaraka.
 
Mkuu ukiona hivyo ujue CCM B1,B2,B3,B4 etc wako kikazi zaidi.Usisumbue sana akili yako waache tu pumba na mchele vitakuja julikana mbele ya safari.Kijani original yenyewe unaiona iko taabanii.NJAA ikikuzidi unakubali hata KUTUMIWA.Huna usemi weye.
 
Hivi kuna mwenye fununu hawa jamaa wamenunuliwa kwa bei gani?
Bado nafikiria na kumshangaa huyu profesa.

Atafanyaje Lapumba kama mwenzake zanzibar kaingia kwenye serikali ya ulaji na yeye hana jinsi,ameona ale na yeye kwa kuchafua wenzake huku bara
 
Wadau hapa jamvini mniwie radhi kwa sababu ntaanzia mbali,

Kwanza naheshimu sana maoni ya mwandishi wa habari hii ambaye bila shaka ni kada mzuri wa chadema na kwa hiyo anafanya kazi yake ya kuipaisha chadema.

Pili lazima niseme wazi kuwa gazeti aliloandikia habari hii la mwanahalisi ni gazeti linalomilikiwa na mmoja wa vigogo wa CHADEMA-antony komu na katika hali ya kawaida gazeti hili linafanya kazi sawasawa na kazi anayofanya ngurumo pale tanzania daima.
Tanzania daima nalo linamilikiwa na mhe freeman mbowe ambaye ni mwenyekiti wa chadema taifa.

Kazi kubwa ya magazeti ya Mwanahalisi na tanzania daima ni kuhakikisha kuwa vyama vyenye nguvu vinavyotishia uwepo wa chadema vinapigwa vita na vinatokomea.

Kazi ndogo waliyonayo magazeti haya ni kuwaeleza wananchi ubaya wa ccm ''chama kilichoshindwa kuongoza nchi'' jambo ambalo ni muhimu kwa maslahi ya taifa.
Chadema wanajua kuwa ikiwa ccm itaondoka wao wanaweza kuwa mbadala lakini wanajua pia kuwa watakaa muhula mmoja tu madarakani kwani sera zao hazitekelezeki,na kwa sababu hiyo ili wakae madarakani muda mrefu ni lazima CUF isiwepo kwani kwa wakati huo ndio chama cha pekee kinachoweza kuwa-challenge cdm na kuwatoa madarakani kwa sbb ccm ikifa itakufa totaly like what happened to KANU.

THUS, makala za namna hii za kipropaganda zina lengo kubwa la kuhakikisha kuwa CDM inavimaliza vyama vingine kwa faida ya CDM na siyo faida ya taifa.

Kwa nini nasema hivi japokuwa sijagusa makala yenyewe?
Nasema hivi kwa sababu mwandishi wa makala ya kuviponda TLP,CUF na NCCR anaonekana too biased,anakwepa kuongea ukweli na anajaribu kusema uongo,katika ufuatiliaji wangu wa mambo ya kisiasa mara nyingi sana nimesikia chadema wakivishambulia vyama vingine vya upinzani kila kukicha ktk mikutano yao,

Lakini vyama husika viki-ijibu chadema vinaonekana vimefanya dhambi na hata hapa JF wadau walio wengi wanataka ukipost thread iwe ya kuisifia CDM tu.
Mfano ulio wazi ni hivi karibuni CHADEMA walivyoanza kuishambulia CUF waziwazi kuwa CUF ni CCM B na kwa hiyo wananchi wasiiunge mkono n.k.

Chadema imekuwa ikitoa matamko ya kuichafua CUF vyombo kama MWANAHALISI-GAZETI LA CHADEMA,
TZ DAIMA-GAZETI LA CHADEMA,
MWANANCHI-GAZETI LINALOUNGA MKONO CHADEMA,
na RAIA MWEMA-GAZETI LINALOUNGA MKONO CHADEMA vinapigia debe sana kauli chafu za CHADEMA dhidi ya CUF na zinatetewa kwa nguvu zote na wahariri wa magazeti husika na hata wakitoa nafasi kwa makada wa CHADEMA kuandika makala za kutosha kuishambulia CUF na hata katika mikutano yote ya CHADEMA ilofanyika hivi karibuni katika mikoa ya mara,mwanza,kagera na kigoma, kazi kubwa ya viongozi wa juu wa chadema ilikuwa ni kuishambulia NA kuidhoofisha CUF na kisha ndio huishambulia CCM,

Kwa hiyo binafsi katika mazingira ya namna hii sielewi mtu yeyote mwenye akili timamu anawezaje kusema ati CUF na vyama vingine vinaishambulia CHADEMA.

Ukweli utadumu milele hata kama muda huu utapotoshwa , ukweli utabakia kwamba CUF ndiyo inashambuliwa sana na CHADEMA na CCM,

Na kama CUF inataka kufa ijaribu kukaa kimya, katika siasa dawa ya propaganda ni ukweli,propaganda huwa hazidumu,chadema ni chama kinachojiendesha kipropaganda mno, wanapokea mabilioni kila siku kutoka kwa makada wa CCM kina sumaye,mengi,sabodo n.k. Lakini wakienda kwa wananchi wanadanganya kuwa wao ni chama kinachoichukia ccm hasahasa na kuwa vyama kama CUF ni wakala wa CCM,

Kwa mtu mwenye akili timamu na zenye kujituma anapata maswali mengi sana!
Yupi wakala wa ccm kati ya chama kilichounda serikali pamoja na ccm kutekeleza matakwa ya kikatiba yaliyotokana na maamuzi na maoni ya wananchi-zanzibar
au chama kinachopokea mabilioni kila kukicha kutoka kwa mawakala wa CCM(sabodo na wenzao) fedha ambazo sote humu JF hatujui zinatoka wapi.

Tujiulize CUF iliyoingia madarakani kwa nguvu na matakwa ya wananchi zanzibar na CDM itakayoingia madarakani kwa nguvu ya fedha za vigogo wa CCM nani kati ya vyama hivi atakwenda kulipa fadhila na kuwasaliti wananchi? Ni aliyeingizwa madarakani kwa fedha za vigogo au aliyeingizwa madarakani kwa maamuzi ya wananchi(kura ya maoni na mabadiliko ya katiba ya zanzibar)?

Watu wanakalia humu ndani ushabiki, kama nilivyowahi kusema na kusisitiza hapo awali, i strongly recommend that CUF shud not keep quite, go to citzens and tell people the truth,
The advantage of speak out truth is the assurance of meeting the most success and here is where you CUF shud stick on,msiwe na sera za papara za kuwaahidi watu katiba mpya ndani ya siku 90, treni ya umeme mwanza to dar,mfuko wa cement TZS 5000,n.k. Ili kuingia madarakani haraka kama wanavyofanya wenzenu CHADEMA,
It is costing much mkiiga mkondo wa siasa za chadema,siyo siasa za kudumu ni za muda tu,
CUF you ar the only party which had/the best and easy to implement manifesto in 2010 of all the parties, stick on your goals,go and speak to people all over the country, speak about CCM failed regime, speak about how your party is alternative, talk to people deeply about how CHADEMA propaganda eats your party and talk to them about CHADEMA'S aims,
Msimwogope mtu yeyote CUF msiwe kama ccm,kama kina mtatiro mnaingia humu just copy this thread and paste it to your computer.

Msitishwe na magazeti yanayofanya kazi za kuitafutia chadema njia ya ikulu, jibuni kila hoja wanayotoa ili wawaangamize,jibuni kila propaganda kwa mifano halisi,
If not today you will serve people of this country tomorrow.

Chama chenu kina wafuasi wa uhakika,watu masikini wa chini watumieni,waacheni chadema waendelee na propaganda zao, kazi yenu ni kuzijibu na kueleza ukweli then let us wait and see if propaganda has ever lived.
Najua wengi mtakasirikia maoni haya lakini the truth always prevails.
Dawa ya moto ni moto tu.
 
Naona umemaliza kila kitu kaka..na kimya hiki cha dakika 45 ambapo jamaa zetu wanaolipwa na CDM kwa ajili ya kujibu na kuanzisha hoja za CDM wamekaa kimya...kama ni mwaka 1985 kule Kizota, Mchonga angeuliza......''kuna Maswali !!!?'' jibu akajipa menye we ''hakuna'' tunaendeleza. Yaanu ukisikia kumkoma mtu giladi ndio huku.

Nice artcicle,
Shkh Yahya,
Magomeni.
 
Thadhari...
Usituletee Majini yako hapa ndani
 
Na hata kama wakirudi hawatakuwa na hoja za kujibu tuhumu hizi nzito ulizozishusha dhidi ya CDM
Shkh Yahya,

Magomeni.
 
Marmoboy, Umejieleza sana lakini kwa sababu nakufamu wewe ni Mh. Fulani na kinara mkubwa wa ndoa hii kati ya CCM na CUF na pia ndio hasa uliyehamasisha hamasa za wananchi kuelewa ndoa iliyokuwepo kati ya vyama viwili uliposhinikiza kushirikishwa kwenye kambi ya upinzani bungeni, na sasa umepewa jukumu la kulizungumzia hili kama ulivyofanya TANGA kwenye mkutano wa hadhara. Watanzania sio watoto wadogo, muandishi wa makala hii ameatoa onyo au angalizo, sasa ni wajibu wa Pr. Lipumba ama akubaliane nae au akatae, mimi naona wewe unamaslihahi binafsi na huutakii CUF mema na hasa upande wa Tanzania Bara. Historia itakusuta baadae kwani asemayo mwandishi ni hisia halisi za watanzania wengi hasa wa bara.

Kalaga baho...
 
Kinachoshangaza ni jinsi profesa huyu anavyoweza kuiponda CCM kwa hoja na maneno yale yale yanayotamkwa na viongozi wa CDM na hapo hapo kugeuka tena na kuiponda CDM kwa maneno na hoja zilezile zinazotolewa na CCM!

Ni maajabu ya dunia! Maprofesa ndiyo wafundishwa hivyo -- au ni yeye tu?
 
Nilikimbilia kununua Mwanahalisi leo lakini hiyo makala haimo. Kumbe ni gazeti la toleo lililopita. Ni makala moja nzuri kwelikweli kuonyesha usaliti wa viongozi wakuu wa CUF -- kwamba wanaweza bila wasiwasi kutumika na chama tawala.
 
Kinachoshangaza ni jinsi profesa huyu anavyoweza kuiponda CCM kwa hoja na maneno yale yale yanayotamkwa na viongozi wa CDM na hapo hapo kugeuka tena na kuiponda CDM kwa maneno na hoja zilezile zinazotolewa na CCM!

Ni maajabu ya dunia! Maprofesa ndiyo wafundishwa hivyo -- au ni yeye tu?

Duh! Hii kali -- jinsi ulivyoiweka! hakika ni kazi kubwa kufanya anavyofanya Lipumba lakini kwa nguvu ya pesa anakubali kuifanya bila wasiwasi! Kweli tuna wanasiasa!
 
Duh! Hii kali -- jinsi ulivyoiweka! hakika ni kazi kubwa kufanya anavyofanya Lipumba lakini kwa nguvu ya pesa anakubali kuifanya bila wasiwasi! Kweli tuna wanasiasa!

Pesa ni balaa -- inaweza kuifanya maajabu kabisa kama vile kuuondoa utu ktoka kwa mtu.
 
Back
Top Bottom