Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,280
- 25,858
CUF na vyama vingine vidogo vya kisiasa visiwani Zanzibar vimejitokeza hadharani na kutangaza kususia uchaguzi wa marudio wa Machi 20. Vipo vyama vilivyotangaza kuwa vimeandika barua za kujitoa.
Jana, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Jecha Salum Jecha ametangaza ya kwamba hadi sasa hakuna chama wala mgombea aliyejitoa kwenye uchaguzi wa marudio. Jecha amezungumzia matakwa ya kisheria ya kujitoa uchaguzini na kwamba hakuna aliyeyakidhi.
CUF na wengineo mmemsikia Jecha? Kama kweli hamtaki kushiriki uchaguzi wa marudio,fanyeni hima kukidhi matakwa ya kisheria ya kujitoa. Mfanye haraka kabla karatasi za kupigia kura kuwasili mwanzoni mwa Machi.
Msipojiondoa kisheria,mtapigiwa kura na washindi kutangazwa. Uchaguzi huongozwa na sheria. Masharti yatakiwayo lazima yatimizwe.