CUF kuwachukulia hatua wanaochoma kadi na bendera zao

NyotaMalaika

Senior Member
Aug 6, 2012
167
77
Chama cha Wananchi (CUF), Wilaya ya Tanga, kimefungua kesi mahakamani kwa ajili ya kuwachukulia hatua za kisheria waliokuwa wanachama wa chama hicho waliohamia Chama cha ACT- Wazalendo kwa madai ya kuchoma bendera na kadi za chama hicho.

Hayo yalibainishwa jana kwenye kikao maalumu kilichoshirikisha wanachama na madiwani wa chama hicho ambao walikuwa na ajenda ya kujadili mustakabali wao baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad, kuhamia ACT Wazalendo mapema wiki hii.

Akizungumza baada ya kikao hicho, Naibu Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CUF Taifa, Masoud Mhina, alisema dhumuni la kikao hicho ni kujitathmini na kuchukua hatua kwa wale waliochoma bendera na kadi kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.

Mhina alisema kikao hicho cha kamati tendaji pia kimetoa tamko la kumtaka aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Mkoa wa Tanga, Rashidi Jumbe, kuhakikisha mali zote za CUF alizokuwa anazishikilia anazirudisha kabla hatua kali hazijachukuliwa dhidi yake.

Alisema miongoni mwa mali za chama hicho zinazoshikiliwa na Jumbe ni pamoja na pikipiki tatu, spika, samani za ofisi na mafaili.

“Tunaheshimu maamuzi yao ya kujiunga na chama mbadala, lakini kuhama kwao hakuhalalishi kuondoka na mali za chama chetu, mali zote za CUF zirejeshwe kwa mustakabali wa chama hicho,” alisema.
 
Sasa Mali wamekimbia nazo wahuni, kiongozi atajuaje Sasa apo
Maendeleo hayana chama
Hahahahahha hahaha hahaha hahaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waanze kwanza kuwachukulia hatua washirika wao CCM ambao ni kawaida kuzichoma moto kadi za wapinzani wanaojiunga na chama Chao

Au ndiyo kusema ule msemo unaosema "mkuki mchungu kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu" ndiyo unao-apply hapa??
 
Tatizo hizo wanazo ziita mali za chama hati za makabidhiano zimepotea zote, hivyo hakuna uthibitisho utakao wafanya watuhumiwa kukutwa na hatia
 
Chama cha Wananchi (CUF), Wilaya ya Tanga, kimefungua kesi mahakamani kwa ajili ya kuwachukulia hatua za kisheria waliokuwa wanachama wa chama hicho waliohamia Chama cha ACT- Wazalendo kwa madai ya kuchoma bendera na kadi za chama hicho.

Hayo yalibainishwa jana kwenye kikao maalumu kilichoshirikisha wanachama na madiwani wa chama hicho ambao walikuwa na ajenda ya kujadili mustakabali wao baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad, kuhamia ACT Wazalendo mapema wiki hii.

Akizungumza baada ya kikao hicho, Naibu Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CUF Taifa, Masoud Mhina, alisema dhumuni la kikao hicho ni kujitathmini na kuchukua hatua kwa wale waliochoma bendera na kadi kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.

Mhina alisema kikao hicho cha kamati tendaji pia kimetoa tamko la kumtaka aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Mkoa wa Tanga, Rashidi Jumbe, kuhakikisha mali zote za CUF alizokuwa anazishikilia anazirudisha kabla hatua kali hazijachukuliwa dhidi yake.

Alisema miongoni mwa mali za chama hicho zinazoshikiliwa na Jumbe ni pamoja na pikipiki tatu, spika, samani za ofisi na mafaili.

“Tunaheshimu maamuzi yao ya kujiunga na chama mbadala, lakini kuhama kwao hakuhalalishi kuondoka na mali za chama chetu, mali zote za CUF zirejeshwe kwa mustakabali wa chama hicho,” alisema.
Kafungueni tu hizo kesi mumalizie pesa ya ruzuku ilobakia
 
Hahaha waongo hao CUF, walikuwa wanauza madela, kofia,,skufu, hadi bendera. Sasa waliovinunua wamevipiga moto wanalalamika wauzaji.
Wavaaji wanachoma mali zao CUF inadai vipi? Au iwarudishie pesa zao ndio idai hivyo vitu visichomwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom