Kama mjuavyo wanaJF, CUF ilisusia uchaguzi wa marudio Zanzibar uliofanyika machi 20.
Sasa nataka tuangalie hatima ya kususia uchaguzi huo. CUF itafaidika ama ndiyo imejiondoa yenyewe ktk medani za siasa za visiwani Zanzibar?
Haina jukwaa la aina yoyote:- udiwani, uwakilishi na umakamu wa rais vyote wamevizika. Watapaza sauti zao kupitia wapi? Sheria zitapindishwa bungeni (Baraza la Wawakilishi) ili kujenga mazingira ya upinzani kutofanya shughuli zao visiwani humo. Nani wa kupinga ili hali bunge (BLW) ni la chama kimoja?
Kingine ni kwamba hata fedha ya ruzuku iliyokuwa msaada mkubwa ktk uendeshaji wa chama haipo tena. Ofisi za cuf zitakosa hata wino.
Binafsi naona madhara ni makubwa kwa cuf kuliko hata faida za kususa walizofikiria zitapatikana.
Muda si mrefu tutaanza kushuhudia malumbano na lawama miongoni mwa viongozi wa cuf kuhusu maamuzi ya kususa. Chanzo kikubwa cha mtifuano huu kitakuwa njaa, na ukata ndani ya chama.
Mwenye faida naomba aziorodheshe hapa.
Naomba kuwasilisha.