CUF kumkamata Maalim Seif iwapo atafika katika Jimbo la Liwale kumnadi mgombea bila kufuata utaratibu kutoka kwa Mwenyekiti

w0rM

Member
May 3, 2011
68
164
Mbunge wa jimbo la Kaliua kupitia tiketi ya CUF, Magdalena Sakaya amesema kuwa endapo Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamadi atajaribu kufika katika jimbo la Liwale kwa nia ya kumnadi mgombea bila kufuata utaratibu kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama hicho anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya siasa nchini kiongozi huyo atakamatwa na Jeshi la Polisi.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku chache tangu Maalim Seif atangaze mpango wa kwenda kumnadi Mgombea wa jimbo la Liwale, Mohamed Mtesa ambaye alipitishwa na upande wa Profesa Lipumba. Ambapo licha ya pande hizo zote kuwa na migogoro zimenonesha kumuunga mkono mgombea huyo.

Sakaya amesema “Maalim Seif itakuwa ngumu kuingia Liwale, kwa sababu baada ya kukihujumu chama kwa muda mrefu tulitoa taarifa kwamba popote atakapofika akamatwe kwa sababu atahujumu tena, Makamanda wa mikoa na vituo vyote vya polisi Tanzania bara wanataarifa, akilazimisha kupanda jukwaa la kampeni atakumbana na nguvu ya Dola ".

“Sisi tulishawajua wao ni wahujumu siku zote, wamekuja kutuunga mkono kwa sababu CHADEMA wamejitoa kwenye uchaguzi, kwa hiyo tulikuwa tumeshawaandaa askari wetu ili wakionesha njama ya kutuhujumu wakamatwe, akitaka kuja kufunga kampeni lazima afuate taratibu, afike ofisini ili apangiwe na Mwenyekiti.” Ameongeza Sakaya

Kupitia Naibu Mkurugenzi wa Habari wa CUF upande wa Maalim Seif, Mbarara Maharagande hivi karibuni alisema,

“Sisi upande wetu hatuna tatizo, kwa sababu yule ni Mwenyekiti wetu wa Halmashauri na viongozi wetu wameshaelekea huko kumuunga mkono, Maalim Seif wiki hii anatarajia kwenda kufunga kampeni, Sisi ndio tulimwambia akachukue fomu na apitishe kwa upande wa Lipumba kwa sababu ndie anayetambuliwa na dola ".
 
Magdalena Sakaya ana mamlaka gani ndini ya nchi hii adi kutoa 'amri' ya kukamatwa kwa katibu mkuu wa chama chake?
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Maalim keshafikia mpaka kusema, "Mimi ndie raisi niliyechaguliwa na Wazanzibar" na hajakamatwa, aje kukamatwa kwa kufanya mkutano?

Jambo la pili kama mgombea ni wenu, naamimi nyie ndio wenye mamlaka ya kuwataarifu polisi na kuomba eneo la.kufanyia mkutano kwa sehemu husika, sasa itakuwaje Maalim aje kufanya mkutano wakati wewe ndiye unajiitia Kaimu Katibu Mkuu. Maalim atafanya mkutano kama nani wakati wewe unakaimu nafasi yake.

La tatu ni kuwa wewe siku zote unapiga kelele kwamba Maalim arudi mujenge chama pamoja na ulipiga kelele sana ulipisikia tetesi za uwezekano ya Maalim kujiunga Chadema. Cha kushangaza leo unataka akamatwe badala ya wewe kushangiria ujaji wake.

My take: Ikiwa haya yanayosemwa yana mashiko kuwa Maalim anamuunga mkono huyu mgombea, basi itakuwa huyu mgombea ni pandikizo la Maalim na Lipumba and Co. wamepigwa bao na wameshtukizia watu wako wanatoa mpira wavuni.
 
Wanaelekea kufanikiwa sasa, Maalim Seif amekwama kifupi njaa imemshika na umaarufu unashuka. Walioplan hili wanaelekea kufanikiwa kwa Maalim kuwa upande wa Lipumba na Cuf kuendelea kukinzana na CDM bara kura zinagawanywa kwa Cuf kumsimamisha Mgombea Urais atakayetoka CCM kujiunga Cuf kwa kazi maalumu na kule Zanzibar kama kawa Maalim kashazungukwa
 
Wanaelekea kufanikiwa sasa, Maalim Seif amekwama kifupi njaa imemshika na umaarufu unashuka. Walioplan hili wanaelekea kufanikiwa kwa Maalim kuwa upande wa Lipumba na Cuf kuendelea kukinzana na CDM bara kura zinagawanywa kwa Cuf kumsimamisha Mgombea Urais atakayetoka CCM kujiunga Cuf kwa kazi maalumu na kule Zanzibar kama kawa Maalim kashazungukwa
Mtasubiri sana ndege bandarini
 
Magdalena Sakaya ana mamlaka gani ndini ya nchi hii adi kutoa 'amri' ya kukamatwa kwa katibu mkuu wa chama chake?
Wasaliti utawajua tu kwa maneno yao ......... kama anaweza kutoa maneno kama hayo, basi anahua hiyo nguvu/mamlaka yanatoka wapi!!
 
Back
Top Bottom