CUF kuishtaki serikali kwa wananchi (nao ni wachochezi?) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF kuishtaki serikali kwa wananchi (nao ni wachochezi?)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Quinine, Mar 17, 2011.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,845
  Likes Received: 11,964
  Trophy Points: 280
  Chama cha Wananchi (CUF), kitafanya ziara ya awali ya siku 15, kuanzia keshokutwa, katika mikoa sita ya Tanzania Bara na Zanzibar, kwa lengo la kuwashukuru wapiga kura na kuishtaki serikali kwa wananchi kwa kushindwa kuboresha maisha yao.

  Ziara hiyo itaongozwa na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, itafanyika katika mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Pwani na kisiwani Unguja, itaanza keshokutwa. Itahitimishwa Aprili 2, mwaka huu.

  Katibu wa Mwenyekiti wa Chama hicho, Thomas Mongi, alisema ziara hiyo imelenga mambo makuu matatu:
  Jambo la kwanza; alisema ni kuwashukuru wapigakura kwa kuipigia kura CUF katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka jana. La pili; kuishtaki Serikali kwa wananchi kwa kushindwa kuboresha maisha yao na kusababisha kupanda kwa gharama za maisha.

  Tatu; kuitaka serikali kuhakikisha mchakato wa kupata tume huru ya uchaguzi unafanyika mapema.

  Nategemea kuanza kuwaona tena Wassira na Simba kwenye vyombo vya habari wakipinga uchochezi huu.
   
 2. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Wasanii kwenye hili game la politics wapo wengi sana..
   
 3. J

  Jonas justin Member

  #3
  Mar 17, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani mbona moshi hawaja taja..
   
 4. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,845
  Likes Received: 11,964
  Trophy Points: 280
  Unategemea CUF wafike huko?
   
 5. M

  MASOKO Senior Member

  #5
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 118
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  mbeya je nyie CUF mbona mnatubagua
   
 6. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hawa wana afadhali maana hawatawaambia Wananchi waige yaliyotokea Libya au Tunisia au Misri!!!! kisiasa wamekomaa!!!
   
 7. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwani CUF si mlisema ni chama cha Waislamu? sasa mnataka waje Moshi na CHADEMA waende wapi?
   
 8. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mkuu, hii ni kweli??? Huko Unguja watishtaki serikali gani vile kwa wananchi??? Na wakishashtaki wananchi wafanye nini sasa? Maajabu hayaishi duniani!
   
 9. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,845
  Likes Received: 11,964
  Trophy Points: 280
  Wataambia wavumilie ndiyo Mungu alivyopanga wawe hadi mauti yao.
   
 10. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,634
  Likes Received: 1,398
  Trophy Points: 280
  wametumia vigezo gani kuchagua hayo maeneo?
   
 11. czar

  czar JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 340
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CUF wako biased na vitu fulani so kuna mikoa fulani hawatafika kama Kilimanjaro n.k. Na ikitokea wakaja ni zuga tu. Wana sehemu zao hao ee.
   
 12. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #12
  Mar 17, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nasikia kichefuchefu
   
 13. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu nasikia ulikuwa kifungoni baada ya kumuita Kiongozi mmoja wa juu katika serikali ya JK sokwe... Vipi Max Shimba,Bigirita,Marytina na Rev Masanilo wanaendeleaje?
   
 14. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Watawaambia wananchi wajifunge mabomu halafu waingie nayo kwenye mawizara, ikulu ile wajilipue si na wao wanaunda serikali.
   
 15. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #15
  Mar 17, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,845
  Likes Received: 11,964
  Trophy Points: 280
  Ndiyo mkuu nimetoka huko jana, ila mazingira ya ban yana utata kidogo Heading ya thread ilikuwa inataja Sokwe kila mtu anakumbuka nilichofanya mimi ni ku post kwa kusema nimechoka kumuona huyo Sokwe nikapigwa ban nakuiacha thread na mtoa thread akiendelea, ni kama kuangukiwa na tai waliokuwa wanasubiri kwa siku nyingi mkono udondoke but Mungu si Abdalah. Huko nilikutana na Rev. yuko fit anawasalimu sana anaendeleza neno la uzima ndani ya gereza kapata waumini wengi nimemuahidi kuendeleza mapambano hadi kieleweke.
   
 16. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #16
  Mar 17, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,163
  Likes Received: 1,122
  Trophy Points: 280
  ....inapendeza japo napata mashaka kidoooooogo!! isije ikawa ni Season 3 ya vijembe kwa CDM!!! Maalim Seif hazunguki? Muda anao sana maana cheo alichopewa ni Ceremonial zaidi so napendekea nae a-join kujisema (maana ni sehemu ya watawala wa kutuletea maisha bora)
   
 17. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #17
  Mar 17, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,265
  Trophy Points: 280
  Kwani si ukweli mtupu kwamba yule bwana anafanana na sokwe? hiyo ban ulipewa kwa misingi ipi?
   
 18. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #18
  Mar 18, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  Sio Cuf tu mbona hata Cdm hawajaenda Znz? na vyama vingine vyote vya siasa mwendo ndio huo,siasa ni mchezo mchafu
   
 19. n

  nndondo JF-Expert Member

  #19
  Mar 18, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 534
  Trophy Points: 280
  Hivi kwa unafiki huu CUF wamegundua wanachekesha? mimi ni mfuasi wa CUF na kwa kipindi chote hichi cha chaguzi 3 nimekua karibu sana nao kwa sababu ya Pro mtu niliyekua namuona makini na msomi. Leo hii nimeshangaa kusoma habari za kwao kuwashitaki CCM kwa wananchi wakati hata wiki haijapita akitangaza kumshambulia Slaa na chadema kwa kuwashitaki CCM kwa wananchi. Je ni kweli prof kapata wazima kwa kukosa madaraka? kumbuka ni mara ya 4 sasa amegombea na kushindwa je kachanganyikiwa? hebu prof na wana cuf tutoleeni upuuuzi huu mbele ya macho yetu kama mnaugonjwa wa kusahau na kutokuona hawa nunueni camcorder muwe mnarekodi mambo mnayoyaseama. Leo mimi mmemnipoteza kama mwanachama na mshabiki wenu kwa kuwa sasa nimehakikisha kweli nyie na CCM B. Kwa ushauri tu, 2015 sio mbali angalieni msije mkapoteza watu wengi zaidi maana wengi wakweli ndani ya CUF wanauona usanii huu maana wao pia walikua wanawachukulia serious, wengine wame invest maisha yao, wamepoteza ndugu zao katika mchakato huu, lakini hawakujua kwamba mlishawasaliti siku nyingi, oneni sasa leo kwa kukubali kuficha ukweli wa ushindi wenu visiwani dhidi ya CCM ili mpewe ulaji, mtu na heshima zake kama Seif leo hii kapewa portfolio ya public health, ukimwi, madawa ya kulevya na homosequality plus bendera na benzi kuna siku atapigwa mawe na hao hao wanachama wake, tahadhari mti na macho sisi sio wajinga lakini hata hao wapemba mnaowatumia kama mtaji, kuna siku watafumbuka macho maana hali ngumu ya maisha nao pia inawakumba. Sasa jana chadema wanaharibu amani kwa maandamano, leo ziara haitaharibu amani? Hypocrits
   
Loading...