CUF: Kikwete hana uwezo akae pembeni 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF: Kikwete hana uwezo akae pembeni 2010

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tumain, Dec 11, 2009.

 1. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kukaa kando ili kumaliza migongano yao ndani ya CCM na kumpisha kiongozi atakayestahili kuwa rais katika uchaguzi mkuu mwakani.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam wakati akitoa maazimio ya kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la chama hicho, Lipumba alisema kutokana na kuwepo kwa makundi ndani ya CCM ndiyo sababu kubwa ya nchi kuwa na ombwe katika uongozi.

  “Rais akiwa kama ni Mwenyekiti wa CCM ambayo ndiyo inaongoza nchi kwa sasa, anatakiwa kukaa kando ili kuweza kumaliza makundi yao ndani ya chama na kuwapisha viongozi wengine wanaofaa, kuweza kushughulikia masuala ya maendeleo na kukuza uchumi nchini,” alisema Profesa Lipumba.

  Alisema wanachama wa CCM ambao wengi wao ni viongozi wa ngazi za juu, wamekuwa wakijihusisha na makundi, ugomvi na hata kurushiana maneno badala ya kukaa na kujadili njaa inayowakabili Watanzania wengi kwa sasa.

  “Baraza Kuu limesikitishwa na kitendo cha CCM kuacha kuwatumikia wananchi iliyowaahidi kuwaletea maisha bora kwa kila Mtanzania na badala yake kugeuka jukwaa la malumbano, mapambano, matusi na kashfa kati ya makundi yanayopigania vita vya kulipizana visasi vinavyotokana na kugombea maslahi binafsi,” alisema Lipumba.

  Aidha, baraza hilo pia lilimtaka rais kuacha kuchezea akili za Watanzania kwa kuendesha kesi za kisanii za ufisadi na badala yake kutoa maelezo na kuchukua hatua kuhusiana na kashfa nzito za Meremeta, Mwananchi Gold, Tan Gold, Richmond, fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), Kagoda Agriculture Limited ambazo Watanzania wanasubiri kuona hatua zake.
  Baraza hilo pia liliitaka serikali kutekeleza kwa ukamilifu maazimio yote 23 ya Bunge kuhusu kashfa ya Richmond na kuwasilisha bungeni katika kikao cha kwanza mwakani.

  Aidha Profesa Lipumba alisema wamesikitishwa na uzembe uliofanywa na serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, ambao umesababisha kukosa umeme wa uhakika, jambo ambalo linazorotesha maendeleo ya kiuchumi. “Ni aibu kwa serikali kutangaza kutekeleza mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA), huku ikiendelea kushindwa kuja na mipango madhubuti itakayohakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika nchi,” alisema Lipumba.

  Source: Tanzania Daima

  My take: Kama hana uwezo si asubiri 2010 ashinde kilaini kwanini anatafuta kushindani na mtu mwingine mzuri au uwoga
   
 2. Y

  Yetu Macho JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2009
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ni Kweli kabisa aliyosema Lipumba. Ila akikaa pembeni leo kuna mpinzani aliejiandaa kuchukua nchi? au akae pembeni waendelee kuchukua mafisadi wale wale?
   
 3. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #3
  Dec 11, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kwa nini yeye kama mpizani amuambie mpizani wake mwingine akae pembeni? Na je kauli hiyo ina maana anajua kwamba upinzani haiwezi kushinda kwa hiyo ni bora CCM imuandae mapema kabisa mtu mwingine kuwa raisi?

  "Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam wakati akitoa maazimio ya kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la chama hicho, Lipumba alisema kutokana na kuwepo kwa makundi ndani ya CCM ndiyo sababu kubwa ya nchi kuwa na ombwe katika uongozi."

  Hapa ndiyo sipati picha, Kwenye kikao cha kichama mtakaaje kujadili mambo ya ndani ya chama kingine na kuwaambia nini cha kufanya? Hii inaonyesha jinsi upinzani ulivyo choka kama kwenye vikao vyao wana kaa na kujadili mipasuko ya ndani ya vyama vingine. Hamna ajenda za maana? Shame!
   
 4. bona

  bona JF-Expert Member

  #4
  Dec 11, 2009
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  naanza pata wasiwasi na msimamo wa chama cha cuf jinsi wanavyotengeneza uswaiba na ccm, maswali ya kujiuliza, je wameona hawana support tena kwa iyo bora wajiunge na ccm, matukio ya hivi karibuni yamekuja kama mshangao kwa wengi wetu, makubaliano ya harakaharaka kati ya shareef na karume, shareef na lipumba kuhudhuria "graduation" ya karume, viongozi wa cuf kukaa jukwaa kuu sherehe za uhuru nk, u turn hii ya cuf ni bure? kumwambia rais amwachie anaweza kutatua matatizo uchaguzi ujao kwa cuf si ndio ingekua nafasi ya kuchukua uongozi ni kana kwamba wamekubali ccm iendelee isipokua ijirekebishe tu, upinzani wa cuf ni upi sasa au wameamua kubadilika baada ya kuona chadema inawapita kama chama kikuu cha upinzani? watanzania tuwe makini na vyama visivyo na msimamo kama ivi vinavyofuata upepo kujiendesha!
   
 5. GY

  GY JF-Expert Member

  #5
  Dec 11, 2009
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Duh kazi ipo. mi nilidhani CUF wangefurahia CCM kuwa na mgawanyiko ili ku-pave way kwa upinzani kuweza kuchukua uongozi, ye anawashauri wamalize mgogoro wao..........Hawa wakati mwingine hua wanaingia kwenye siasa kujaribu, hawajiamnini
   
 6. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #6
  Dec 11, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mimi nilidhani kifo cha panzi furuha ya kunguru. CCM ikivurugika ndio furaha ya wapinzani na wapinzani wakivurukiga ndio furaha ya chama tawala. Sasa inakuwaje CUF inasononeka kwa mtafaruku ndani ya CCM? Wazungu wanasema: To cry more than the breaved! Yaani mtu unalia kwenye msiba kuliko wafiwa! haiingii akilini.
   
Loading...