Chama cha CUF kinajiua chenyewe.
Kutafuta uhalali ili kukubalika kwa misingi ya ukabila
Kutafuta uhalali ili kukubalika kwa misingi ya udini
Kutafuta uhalali ili kukubalika kwa misingi ya usisi na wao
UBAGUZI - Haukubaliki na haunanafasi wala usipewe nafasi kutugawa watanzania kwa maana yoyote ile iwe ni, din, ukabila, wao au sisi
Hapa CUF wanajiteketeza kwa mafuta yao wenyewe Raia wanateseka kwa ugumu wa maisha, bungeni tunashuhudia waziwazi
nini kinatendeka, mitaani watu wanashuhudia kwa vitendo mfumuko wa bei, huduma mbaya za afya na elimu, viongozi wakishinda
angani kutwa kucha na safari, nani atakubali kuendelea kuwa dodoki la kusafisha mapito ya mafisadi? Kama CUF wameamua
kuendelea kuwa washika pembe ccm wakamue maziwa ni hatari kubwa, watanzania watajitenga, na CUF itapotea kabisa
kwasababu wanafaham mchawi wa maendeleo yao ni serikali Dhaifu na kujiunga nayo nikujitenga na watanzania waliowengi
yaani walalahoi.